Television yetu ya taifa TBC , ni kama mtoto ya tima kwa sasa, hii hali inasikitisha, pamoja na jitihada za kuliokoa shirika kutokana na gharama kubwa za kurusha bunge live , hali imekuwa bora kipindi cha bunge live watu walikuwa wakiitazama kuliko sasa.
Watangazaji wake hawajulikani sana na jamii, waliopaswa kuisapoti nao wameikimbia tunaona wakipiga simu kwenye vyombo vya habari binafsi, tena wakijisifu kuwa ni wasilizaji wakuu wa vipindi vya huko.
Wadau kwa umoja wetu tutoe maoni nini kifanyike ili hata watu wetu wa serikali warudi kuitazama television yetu, nini kifnyike kuzalishwe vipindi vyenye mvuto?
Nini kifanyike ili hata kwenye ziara za viongozi ziratibiwe na watangazaji na waandishi wa tbc badala ya zile zingine. Hasa radio mawingu?
Kwa mtazamo wangu fedha zinateketea zaidi sasa ambapo utazamaji umepungua, ujumbe unaotolewa utatuvutiaje tuupate.