GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 63,035
- 126,504
Huyu Mkurugenzi alikula "like" nyingi Hapa sijui Kama hazikumlevya.
Hakuanza tu kupewa " like " na nyie bali alianza kupata " likes " nyingi kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Malaika wake hivyo ameshabarikiwa na atazidi " kung'aa ". Nimefundishwa na Wahadhiri wengi tena wa kila Race hapa Duniani ila sijawahi kufundishwa na kumwelewa Mhadhiri na kulipenda Somo kama Mwalimu wangu Dkt. Ayub Rioba na namshukuru sana kwani UELEDI wangu wa leo, KUKUBALIKA kwangu na uwezo wa KUFIKIRI wa KIMANTIKI umechangiwa sana na huyu Dkt. Ayub Rioba bila kumsahau Mhadhiri wangu Kipenzi mwingine aliyenijenga na kunipa MAARIFA ya KUTUKUKA Askofu Dkt. Bernadin Mfumbusa ( sasa ni Askofu nadhani wa Jimbo Kuu la Singida kama sijakosea ) Kiburi changu chote na jeuri zangu zote nimezipata baada ya kupewa MADINI ya kutosha na hawa MANGULI wawili Dkt. Rioba na Dkt. Askofu Mfumbusa na namwomba Mwenyezi Mungu azidi KUWABARIKI, awape maisha marefu, mazuri, afya njema na awazidishie uwezo wao mkubwa wa AKILI na KUFIKIRI na naamini JEMBE lao WALILONIFUNDISHA siwaangushi kwani napita " mule mule " wanapopita wao.