Dr. Ramadhan Dau aunguruma darajani Kigamboni

Kuna watu hawana cha kufanya zaidi ya dini na sifa za kijinga. Rais kumpongeza Dau haijamfanya kuwa mwanzilishi wa Taifa hili na hata haiondoi wasiwasi wa watu juu ya tabia yake yoyote mbaya anayoweza kuwa nayo. Hata wale wanaofahamika kwa upuuzi wao ktk dunia hii walifanya makubwa kuliko hata ya Dau!

Hitler anasifika hadi leo kwa upuuzi wake lakini huwezi kumuondoa kwenye historia ya maendeleo ya ujerumani kama nchi. Sasa huyu Dau kuongoza taasisi moja tunamzungumzia utadhani kaokoa roho za watu wanaoangamia!
 
Dau yupo vzur sana hata hotuba yake alyoongea uutaona ni level nyingne kabisaaa,pigen kelele hazsaidii mpewa hapokonyek
Dau, Dau! Hotuba, Hotuba ipi hiyo? Kucheka ndo hotuba? Dak. 4 kuna hotuba ya kusifia kitu gani? Kama una elimu kidogo na kama lengo ni kuwasifia walio na dini kama yako, hebu sikiliza hotuba na mihadhara ya marehemu Ali Mazrui.
 
Umenikumbusha mbali sna sheikh Mohamed Said marehemu Baba yngu alikuwa na Rafiki kipenzi mzee wa Dar es salaam akiitwa Saad juma Mzee huyo saad Baba yke akiitwa Juma Mzee alikuwa anaishi kariakoo mtaa wa PEMBA alikuwa na mabasi yke alikuwa ameyaandika ilo jina au ni sema huo wimbo WASTARA HAUMBUKI WASTARA MJA WA MUNGU sasa sijui wanajisikiaje waliokuwa wanamuombe mabaya DK DAU bila Sababu ya msingi watanzania tuache chuki za kijinga na udini sio kuwa na sababu Ongera Dk Ramadhani Kitwana Dau
 
Nimeshindwa kuhusianisha Title na contents.
 
Wala hayuko anaye kufedhehesha umea amua mwenyewe kuji fedhehesha kwa radhi yako,na ije siku uka baini fadhila ulizo kuwa unapata zilitokana na ufisadi ni haramu nawe umesema ni mtu wa ibada sipima hata utajisikiaje,haya nikutakie kila la kheri na Uwakili ulio jivika.
 
Franco Zetta,
Unanitukana kisha unanambia nataka kutukanwa.

Hapa tulipofika panatosha hapana haja ya matusi
zaidi.
 
Diniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Mohammed Said niliingia wikipedia jana. Sikuliona kabisa jina la huyu daktari nguli wa masoko.
 
The big show utapotea humu jamvini siku si nyingi usidhani jpm kumsafisha dau kwa kashfa zingine zooote maana viwanja alivyonunua na ubia na azimio bado majibu zero,zile bilioni 179 bado majibu,nyumba anazomiliki nazo bado majibu na hayo majibu hana magufuli,kwenye kujua ya dau ni TAKUKURU na TISS,muda ukifika jipu litatumbuliwa tu,
 
Rubawa,
Hizi chuki zimeletwa kwa watu kutoijua historia ya wazee wetu.

Laiti ingesomeshwa historia ya kweli na watu wakajua mapenzi
yalikuwapo enzi zile za kupigania uhuru vipi Nyerere Mkristo kaja
kapokelewa na Waislam na wakamweka madarakani hii ingeleta
kujua tulipotoka.

Tungejua mizizi yetu ilikochimbukia.

Hii khiyana ya kutaka kubadili historia na kufanya kama vile Nyerere
alikuwa peke yake na kuleta uhuru peke yake ndiyo iliyotufikisha
hapa.

Miaka ya 1950 dini ya mtu haikuwa tatizo kwa wazee wetu hata kidogo.
Angalia mfano huu.

Wakati wazee wetu wanataka kubadilisha uongozi wa TAA baada ya Vita
Vya Pili Vya Dunia aliyekuwa mbele kutaka Dr. Kyaruzi na Abdul Sykes
wachukue uongozi kama rais na katibu alikuwa Schneider Abdillah Plantan.

Huyu Schneider ndiye akaja kuwa katibu wa Daawat Islamiyya (Wito kwa
Waislam) chini ya Sheikh Hassan bin Amir.

Na huyu Sheikh Hassan bin Amir ndiye aliyemjenga Nyerere kwa umma wa
Waislam kama kiongozi wa harakati za kudai uhuru.

Hawa Waislam wote niliowataja hapa wapi historia yao imeandikwa?
Hili ndilo tatizo kubwa.
 
Alwayz...,
Watu wengi wamefurahishwa na aya hii iliyokuwa munasab
na tukio.
Kabisa Shekhe wangu Kwenye ukweli uongo hujitenga wanamsingiza sana Dr Dau lkn wanamsingizia kwa chuki zao tu lkn mola atadhihirisha ufalme wke na uongo utajulikana tu Inshaallah
 

Masikini hawa wazee walioijenga TANU, hivi walimkosea nini Nyerere?
 
Franco Zetta,
Unanitukana kisha unanambia nataka kutukanwa.

Hapa tulipofika panatosha hapana haja ya matusi
zaidi.
Umedai awali kuwa nina kufedhehesha nime kuambia unaji fedhehesha mwenyewe,kuna tusi wapi? lugha ya matusi huipati kwangu mimi ni Mtanga kaka Kiswahili nime kishiba, maneno unayotoa mwenyewe yana kuwia Mwiba,Pumzika muungwana punguza mawazo.
 
Swali lako kalijibu Rais katika hotuba yake. Kasema gharama ziliongezeka kutokana na kutitia kwa kitanda cha bahari na kutokea kwa korongo la karibu mara mbili ya urefu walioukadiria hivyo gharama lazima iongezeke.
Kama ni kweli, basi kwa hoja yako hii naungana na wale wanaosema kuwa Tanzania hakuna haja ya feasibility study ambayo nasikia ilichukua billions kadhaa pia kwenye huu mradi.
 
Dau, Dau! Hotuba, Hotuba ipi hiyo? Kucheka ndo hotuba? Dak. 4 kuna hotuba ya kusifia kitu gani? Kama una elimu kidogo na kama lengo ni kuwasifia walio na dini kama yako, hebu sikiliza hotuba na mihadhara ya marehemu Ali Mazrui.
MuchunguZI,
Unafananisha mambo mawili yasiyo na uhusiano hata kidogo.

Lakini si kitu ikhtilafu baiana ya binadamu ndiyo inafanya dunia
izunguke.

Umemtaja Prof. Ali Mazrui.
Mimi nimejuana na Prof. Mazrui kupitia Dr. Dau.

Yeye ndiye alikuwa rafiki yake na nilipotoa kitabu changu cha
kwa ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924- 1968)
The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism
in Tanganyika,'' London 998 alimpa kitabu hiki mkononi Marekani.

Niliandika maneno haya katika kitabu: ''Kwa mwalimu wa wa
masafa marefu Prof. Ali Mazrui.''

Prof. Mazrui aliniletea barua na katika maneno aliyosema alisema
kafurshishwa na kitabu changu kwa kueleza nini Waswahili wamefanya
kupinga ukoloni.

Huu ndiyo ukawa mwanzo wetu wa kujuana.

Lakini usuhuba huu ukanoga zaidi pale Dr. Harith Ghassany
alipomweleza Prof. Mazrui kuwa mimi ni rafiki yake.


Kushoto Tamim Faraj ( Muslim University of Morogoro),
Prof. Ali Mazrui na Mwandishi Nile Hilton Kampala

Ukipenda habari zaidi ingia hapa:
Mohamed Said: TAAZIA YA PROF. ALI MAZRUI 1933 - 2014
 
Kabisa Shekhe wangu Kwenye ukweli uongo hujitenga wanamsingiza sana Dr Dau lkn wanamsingizia kwa chuki zao tu lkn mola atadhihirisha ufalme wke na uongo utajulikana tu Inshaallah
Alwayz,
Allahuma Amin.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…