- Tunachokijua
- Kumekuwepo na kipande cha video kinachosambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii kikimuonesha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Emmanuel Nchimbi akitamka kuwa kama wanataka kumtimua basi wamtimue.
Nchimbi anasikika akisema
"Na kuna mambo mengine ya msingi. Kuna wakati watu wanasema Nchimbi tatizo lake ana misimamo simamo hivi. Ni kweli, kwenye mambo ya msingi mimi nina msimamo. Na hili lazima tuelewane, ni jambo la kawaida tu. Kama mnataka kunitimua kwa msimamo, nitimueni leo leo. Kwenye mambo ya msingi lazima uwe na msimamo. Na ndiyo moja ya viapo vya chama chetu, mwana CCM mwenye msimamo ni dhumuni la pili tu, ndiyo sifa ya kuwa mwanachama. Nitasimulia hiyo mwaka 2000..."
Je, uhalisia ni upi?
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umejirirdhisha kuwa Dkt. Nchimbi aliyazungumza maneno hayo lakini hakuwa akimuambia Rais Samia kama inavyodaiwa bali aliyzungumza akiwa kwenye kutano wa hadhara kuwajibu watu wanazungumzia kuhusu misimamo yake.
Nchimi alizungumza maneno hayo muda mfupi baada ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Chama Chama cha mapinduzi January 2024, hivyo video hiyo imekuwepo mtandaoni kuanzia mwaka 2024.
Mathalani mtumiaji mmoja wa mtandao wa Youtube alichapisha video hiyo Januari 18, 2024 ikiambatana na ujumbe "HUYU NDIYE EMMANUEL NCHIMBI KATIBU MKUU CCM KAZINI". Tazama hapa