Nilikuwepo uganda usiku na siku ya tukio la ugaidi lililofanywa na kundi la Al-shabab ambalo ni la waislamu wanaojiita wenye siasa kali na wenye lengo la kuleta sharia. Nilishuhudia maiti na vipande vya miili ya marehemu eneo hilo la Kyadondo. Uwezo wa kujilinda na makundi haya Uganda kama zilivyo nchi nyingine nyingi Africa hawana. Baada ya tukio ulinzi mkali ofizi za serikali wakisaidiwa na wamarekani uliimarishwa. Sheikh Ali Mahamud Rage.
Kundi hili ambalo liko affiliated na Al Qaida ni makundi yenye mission maalumu na yenye uwezo mkubwa wa fedha, uwezo, intelijinsia, wengi wa wafuasi wao ni wasomi na wenye high qualification kwenye IT, Engineering, weapons, planning etc. Huwa hawafanyi mashambulizi bila sababu, wakifanya husema bila uwoga kwani hufanya kwa mission maalumu.
Ukisoma kwa makini sana uwezo wao na mission zao, napata wasiwasina taarifa zilizojitokeza siku za karibuni kuwa wanataka wamuue Mwakyembe na Dr. Slaa! Mwakyembe alivyosema sikushtuka wote tunamjua. Issue kama zile ni za kusema na kufanya kimya kimya kwani makundi kama Al-Shabab huwa hawana siri na huwa wana declare interest zao. Pengine ni wasomali tu na sio Al shabab, .Nimestuka na kauli ya Slaa eti haogopwi kuuawa na Al-Shabab nikacheka sana! Nilicheka sana , tena sana wauaji hawangaiki vile. Na Kama kungekuwa na failed attempt ingejulikana waziwazi! Kuna notable failed attempt ambazo huwa zinabuma na kuvuja vibaya, japo kama zile za kumuua rais zimefanywa siri sana na lakini kuna watu walikufa on spot.
Mwakyembe shughulika na polisi na maliza mambo yako na polisi bado tuna polisi wazuri wa kukusaidia. Slaa usikurupuke ulitakiwa kuwajua Al-shabab mapema na siyo kusema haugopi
huwa hawana muda na assassination ya mtu mmoja, huwa wanaua massive na unakaribisha kuuawa kwa raia wengi , kama hawa jamaa wataelekeza masikio yao kwenu .
Sijajua lengo la kuwaingiza al-shabab ni kuwatisha watanzania au kuwakaribisha, mkiwawekea njia kweli watakutana na wengine waliojichokea maisha na kutawala eneo la maziwa makuu, wanataka sharia, huku wengine wanataka kadhi, hivi hamuoni kuwa mnawakaribisha??
Hivi akina Slaa na mwakyembe hawa jamaa wakiamua kufanya mambo nani wa kuwazuia? Ya Gongo la Mboto na Mbagala yanatosha, waaacheni, msiwataje tena, hatuna uwezo wa kuwahimili na wakiingia watatuonea mpaka basi!!
I repeat kama Al-Shabab wanataka kuwaua akina Mwakyembe na Slaa wangekuwa wamefanya hivyo siku nyingi na wao wenyewe wangetuambia kwa nini wameamua wawaue! I dont think so unless kama hawa watu waliwazuia al-shabab kwenye mission zao. Kwa uwezo wao hawana muda wa kutumia magari yenye number na kujulikana na Mwakyembe! kumbuka I can prove that they are highly trained.
Sina muda kuwa kupitia kila sentensi ya taarifa ya mwakyembe, ila ina maswali mengi sana, na inaweza kumuweka kwenye kundi la kuwa naye ni mtu hatari..unafanya biashara gani??
Richmond na Dowans mpaka sasa wajuzi wa mambo wanajua imekula kwenu, mmeshindwa, tunaangalia movie inaendaje