Dr. Mkumbo aula UDSM

Ndio maana mwigulu kawa kama mtu aliyechanganyikiwa siku hizi.. Hongera Dr Kitila
 
Nadhani ni vizuri kuaminiwa na kupewa dhamana kubwa kama hiyo,lakini siamini kama UMEULA!wanotakiwa kushangilia ni wale wenye imani na uadilifu wako katika kukitendea haki kitivo cha elimu cha DUCE!Siwezi kukupongeza kwa sasa lakini nitapongeza matokeo yako mazuri ya kazi!Nakutakia kazi njema!
 
Badilisha kichwa cha habari "aula" ndiyo nini, una maana haendi kufanya yaliyotarajiwa bali kujineemesha?

njoka,ndo utaratibu tulouzoea huo,labda akabadili mfumo,,,,UKITEULIWA NAFAS ZA JUU WE SAY UMEULA,,,,,POSHO LUKUKI NA MSHAHARA UNAKUA JUU
 
Ni mwathirika wa ukanda Huyu yuko kambi ya zitto , akiamka kugombea uongozi cdm yupo hatarini. Kwa vile si wa kaskazini. Pole dr. Tuvumilie tu lakini . Mbowe atauonea huruma baada ya 2020 tutakapokuchua nchi. Uwezekano wa 2015 . Ni mdogo sana. Hatujajipanga tuna ubinafsi mno. Chama kikijitanua mpaka vitongiini hapo yawezekana.
 
Badilisha kichwa cha habari "aula" ndiyo nini, una maana haendi kufanya yaliyotarajiwa bali kujineemesha?

Hii ndio mentality ya watu wengi..... kuwa ukipata nafasi ya kutumika , basi umeula... insababisha watu kufikiria kuula kweli na kuanza ubadhirifu mara wapatapo nafasi za kutumika/kuongoza. Tubadirike kimtazamo.
 
hongera sana kwa uteuzi lakini mbona ni mtuhumiwa wa mauaji huko kwao iramba
??????????????????????????????????????????????
 
kwa sasa anajieleza polisi huko singida jinsi alivoshiriki mauaji ya mwananchi kwenye mkutano wake na mnyika
 
[h=2]Viongozi wa chadema kuhojiawa singida leo-kuhusu fujo za ndago iramba.[/h]
Tupo Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida kwa kamanda Mkoa Linus Vincent Sinzumwa, kusubiri Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika na Dr. Kitila Mkumbo kuhojiwa kuhusu fujo zilizotokea Kijiji cha Ndago, Wilaya ya Iramba wiki iliyopita. Hata hivyo baada ya viongozi hawa kufika mapema kadiri ya muda walioambiwa na RPC huyo, Polisi wameshindwa kuanza mahojiano na viongozi hawa kwa kile kilichosemwa kuwa ni kuwasubiri Makamishna na Makachero kutoka makao makuu ya jeshi la Polisi toka Dar es Salaam.​
 
Basi kuna jamaa lilisema hapa JF kuwa CDM hakuna wasomi..!! Sasa cjui, MSOMI ni mtu gani kama hata Dr. Mkumbo sio MSOMI??

Hoja yake ilikuwa ya kitoto yeye anazungumzia kuhusu kuundwa serikali kwa kuangalia wabunge waliopo badala ya kuangalia mtaji wa wanachama kwa siku zijazo
 
Kwanza nimpongeze Doctor Mkumbo hongera sana unastahili kwani kwenye uchapa kazi uzembe hujitenga;wewe ni mchapa kazi na kiongozi makini, hongera. Pili niupongeze uongozi wa UDSM kwa kuuona ukweli, kuweka kando siasa za vyama na kuangalia maslahi ya Chuo Kikuu na Taifa. Hongera Prof. Rwekaza Mukandala na timu yako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom