Dr. Magufuli tulia, utaharibu

Dr. Magufuli tulia, utaharibu

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,007
Tangu ulipoteuliwa na kuchaguliwa kuwa mgombea wa CCM, umekuwa ukihutubia kikampenikampeni. Kuanzia Dodoma, Dar es Salaam hadi Zanzibar,mikutano yako imesheheni ahadi. Kiuchaguzi,ahadi hutolewa kipindi cha kampeni.

Unapozitoa ahadi katika mikutano isiyo ya kampeni unatafsirika vibaya.Unavunja sheria za uchaguzi mchana kweupe Dr. Magufuli tulia.

Mikutano inayoratibiwa na chama kwasasa ni mikutano ya kukutambulisha. Si ya kampeni. Usiahidi. Unatakiwa ujitambulishe na kuketi.

Kama afanyavyo Mama Samia Suluhu Hassan. By the way,kumbe pamoja na 'ujembe' wako bado hautambuliki hadi utambulishwe!? Subiri wakati wa kampeni uhaidi bila ushahidi. Uwanja utakuwa wako. Si sasa. Utaharibu!

Viongozi wa chama nanyi mtulie tusubiri kumpigia chapuo mgombea wetu wakati wa kampeni. Tutamuharibia na kujutia. Wananchi wanatuchora tu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam.
 
Daraja la kuunganisha Dar na Zanzabar kasema ujenzi utaanza lini?
 
Wao wanasema huyu anatambulika kwa utendaji wake, lakini wananchi wanauliza "NDIO NANI?" na hilo ndio linawatia hofu mpaka wanavunja sheria ya uchaguzi. Ila kwa vile Tume ni yenu mzee Tupatupa usiwe na hofu hawezi kufanywa kitu ndio maana hata TFF nayo imetumika kumkampenia.
 
Kazi Yaani CCMHuwa Ni Wepesi Kusahau.

Mnakumbuka Dodoma Jk Aliposema Mbona Hamshangii.

Hii Ni Historia Kupata Makamu Wa Rais Mwanamke

Baadhi Tulishangaa Kwa Maana Uchaguzi Iweje Tupate Makamu Kwa Kutambulishwa Tu. Hiki Ndicho Kinachotokea Sasa Yaani Wanaona Kuwa Uchaguzi Tayari Na Wananchi Wamewachagua.
 
atulie....achunge kauli..mara aseme wagogo ni watani zake na kwamba usiku wa manane huwa wanafanya nini sijui....aache papara mara apige ngoma....aimbe manyimbo ya kisukuma,washauri wakae nae wampange
 
magufuli cyo mtu wa kuongoza ni wa kuongozwa na yy afuatilie tu.cyo mtulivu ana.pupa na papara hajui kuangalia side effects za mambo.hili mtalijua baadae.jk pamoja na ubovu wake wooote na uozo lkn ni mtulivu hana haraka na pupa ktk matamshi na maamuzi
 
Kazi Yaani CCMHuwa Ni Wepesi Kusahau.

Mnakumbuka Dodoma Jk Aliposema Mbona Hamshangii.

Hii Ni Historia Kupata Makamu Wa Rais Mwanamke

Baadhi Tulishangaa Kwa Maana Uchaguzi Iweje Tupate Makamu Kwa Kutambulishwa Tu. Hiki Ndicho Kinachotokea Sasa Yaani Wanaona Kuwa Uchaguzi Tayari Na Wananchi Wamewachagua.

Mkuu umesahau Nape alisema watashinda kwa bao la mkono ?
 
Kazi Yaani CCMHuwa Ni Wepesi Kusahau.

Mnakumbuka Dodoma Jk Aliposema Mbona Hamshangii.

Hii Ni Historia Kupata Makamu Wa Rais Mwanamke

Baadhi Tulishangaa Kwa Maana Uchaguzi Iweje Tupate Makamu Kwa Kutambulishwa Tu. Hiki Ndicho Kinachotokea Sasa Yaani Wanaona Kuwa Uchaguzi Tayari Na Wananchi Wamewachagua.
Uchaguzi ndo umeisha hivyo, nani wa kumshinda TingaTinga?
 
Tangu ulipoteuliwa na kuchaguliwa kuwa mgombea wa CCM, umekuwa ukihutubia kikampenikampeni. Kuanzia Dodoma, Dar es Salaam hadi Zanzibar,mikutano yako imesheheni ahadi. Kiuchaguzi,ahadi hutolewa kipindi cha kampeni.

Unapozitoa ahadi katika mikutano isiyo ya kampeni unatafsirika vibaya.Unavunja sheria za uchaguzi mchana kweupe Dr. Magufuli tulia.

Mikutano inayoratibiwa na chama kwasasa ni mikutano ya kukutambulisha. Si ya kampeni. Usiahidi. Unatakiwa ujitambulishe na kuketi.

Kama afanyavyo Mama Samia Suluhu Hassan. By the way,kumbe pamoja na 'ujembe' wako bado hautambuliki hadi utambulishwe!? Subiri wakati wa kampeni uhaidi bila ushahidi. Uwanja utakuwa wako. Si sasa. Utaharibu!

Viongozi wa chama nanyi mtulie tusubiri kumpigia chapuo mgombea wetu wakati wa kampeni. Tutamuharibia na kujutia. Wananchi wanatuchora tu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam.

kwa sababu ni CCM SHERIA ZOTE ZIPO CHINI YAKE,MAGUFURI CHAPA MWENDO.......
 
atulie....achunge kauli..mara aseme wagogo ni watani zake na kwamba usiku wa manane huwa wanafanya nini sijui....aache papara mara apige ngoma....aimbe manyimbo ya kisukuma,washauri wakae nae wampange
Kweli naona amesahau yaliyompata Lowassa. Alikuwa wa kwanza kutangza na mbwembwe nyingi lakini akaachwa na yeye Magufuli aliyekuwa wa mwisho mwisho kutangza akapata nafasi. Naona kama ana kihere here ambacho kitamponza. Hata huo ugeni rasmi wa pambano la Yanga na Gormahia angekuwa na watu wenye busara au yeye mwenyewe asingekubali kwenda kwani TFF watamponza kwani hizo ni kampeni za wazi. Aangalie atachoka mapema na kuwachosha watu kwani akitokea mwingine mwenye nguvu UKAWA watu watageuza nia zao kwake. Inaonesha wazi hii nafasi aliipata kama bahati ya mtende kutokana na msuguano mkali kati ya Membe na Lowassa. Baada ya Lowassa kukatwa wakawaweka hao akina Magufuli na wenzake kama bosheni tu lakini lengo lilikuwa Membe. Wafuasi wa Lowassa kugundua hivyo wakaamua kuhamishia kura zao kwa Magufuli wakati vibopa walitegmea kuwa baada ya kumng'oa Lowassa ingekuwa rahisi kwa Membe kupita kwa urahisi. Hivyo kura za Lowassa ndizo zilizompa nafasi hiyo Magufuli na tunaweza kusema Magufuli amshukuru na kuwashukuru wafuasi wa Lowassa. Sasa baada ya hapo ni kama mtu aliyestuliwa kwakuwa hakujipanga vizuri. Anatakiwa apate wataalamu wa kumuelekeza cha kuongea na wapi aende so kila wakati "sitawaangusha..., nitaulinda muungano..." nk Atoe hoja za kuwakwamua wananchi kwenye umasikini na unyonge. Muungano uko kikatiba hakuna mtu aliyesema anataka kuuvunja yeye aseme nitailinda au kufuata katiba humo ndimo muungano umo
 
Magufuli anatakiwa kutambulishwa Mwanza, Mbeya , Arusha na Morogoro. Wananchi wanamsubiri kwa hamu.

Mungu anaipenda sana Tanzania, watu hawakutegemea kama watapata Rais mchapakazi kama Magufuli.
 
Dr Magufuli ni scorpion(nge).ni aina ya watu wenye maamuzi ya haraka na pupa.na ni watu wa visasi usipime.pia ni watu wasiopenda kushindwa..ila ni wachapakazi wazuri mnoo.they can get things done better than any other sign.they have alot of energies..Dr Slaa nae ni scorpion..scorpion ndio inaongoza kwa kuwa na maraisi wengi walioko madarakani kipindi hichi.kwamba scorpion wana 22% ya maraisi walioko madarakani duniani,wakifuatiwa na leo 18%..
 
Tangu ulipoteuliwa na kuchaguliwa kuwa mgombea wa CCM, umekuwa ukihutubia kikampenikampeni. Kuanzia Dodoma, Dar es Salaam hadi Zanzibar,mikutano yako imesheheni ahadi. Kiuchaguzi,ahadi hutolewa kipindi cha kampeni.

Unapozitoa ahadi katika mikutano isiyo ya kampeni unatafsirika vibaya.Unavunja sheria za uchaguzi mchana kweupe Dr. Magufuli tulia.

Mikutano inayoratibiwa na chama kwasasa ni mikutano ya kukutambulisha. Si ya kampeni. Usiahidi. Unatakiwa ujitambulishe na kuketi.

Kama afanyavyo Mama Samia Suluhu Hassan. By the way,kumbe pamoja na 'ujembe' wako bado hautambuliki hadi utambulishwe!? Subiri wakati wa kampeni uhaidi bila ushahidi. Uwanja utakuwa wako. Si sasa. Utaharibu!

Viongozi wa chama nanyi mtulie tusubiri kumpigia chapuo mgombea wetu wakati wa kampeni. Tutamuharibia na kujutia. Wananchi wanatuchora tu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam.

We mtoa mada UKAWA nn???
 
Back
Top Bottom