Dr. Magufuli, tafadhali badili hotuba

Dr. Magufuli, tafadhali badili hotuba

Mh!! Unaonekana hukusoma huki Mkwawa. Boiler ndiyo nini na maana yake nini au ulikuwa unataka kusema boarer?

Hasa ni "boiler" (boila) wala sio boara. Masomo yalikuwa ya sayansi hivyo boiler ndio ule mtambo unaotoa "steam" ambao hutumika sana viwandani.
 
Mkuu,
Na hili la kila anapotaka kuhutubia ni lazima amshukuru sana JK na kuhaidi kutomwangusha unalionaje??? Hata jana kafika mbali sana kwenye hotuba yake pale kwa kusema mara nyingi JK OYEEEE!!!!!! JK Oyeee!!!!!! badala ya CCM Oyeee!!!!. Nikilinganisha jinsi anavyomuongelea JK ni kama vile yeye atamtegemea JK katika mambo mengi sana ya kuongoza nchi. Hili linanipa wasiwasi zaidi, kwani JK ni kati ya viongozi walioturudisha nyuma sana kwa kutokuwa na uongozi wenye vision na hata nia thabiti ya kumuokoa mtanzania. Na ikiwa Magufuli atafanikiwa kuwa Rais na akamtegemea JK kulingana na jinsi anavyomsifia basi watanzania tutegemee maumivu zaidi.

Jambo lingine linalonitia shaka kuhusu Magufuli ni muonekano wake, kwangu mimi simwoni kama mtu mwenye kuwakilisha presidential presence. Magufuli anaonekana kama mtendaji fulani mwenye kupewa majukumu na kuyatekeleza katika uhalisia wake na si Rais kama kiongozi wa nchi. Anyway, sijui wenzangu mnachukuliaje hili la muonekano wake na kila siku JK Oyeeeee!!!!!! badala ya CCM Oyeee!!!! au Tanzania Oyeeee!!!!!!

Nami namwomba mheshimiwa Magufuli abadilishe kauli zake kuwa amejenga mabarabara na watapita humo humo, hata jana kairudia. Hivi hizo barabara kajenga kwa hela zake au kodi zetu Watanzania? Sisi tulimpa dhamana ya kusimamia tuu na tukamlipa mshahara hivyo asitunange sisi waajiri wake
 
Tatizo lenu nini? Huyu ndiye Raisi wa nchi panga pangua hana doa sio mwizi kama raisi mteule wa chama Fulani in fact amechaguliwa na Mungu kuliokoa Taifa letu
 
Magufuli si mwanasiasa
Yeye chake ni kemia
Akijitahidi sana atasema "Vunja nyumba, choma nyavu au piga mbizi"

Baaaasiiii
 
Bukinabuza kachaguliwa na MUNGU yupi? sabb wapo wanaoabudu sanamu wengine milima wapo wa ng'ombe na yupo mkuuu wa wote aliye hai aliyeejuu palipoinuka ambaye naamini hawez kutuchagulia huyu
 
Last edited by a moderator:
Bila shaka ndicho alichokariri kwa sasa, mpeni muda atabadilika........
 
Sasa unaelekea 'kuboa'. Unarudiarudia maneno yale yale kila mahali unapohutubu,kwanini? Badili hotuba. Badili maneno. Kuanzia ukumbini Dodoma; uwanjani Dodoma, Dar es Salaam na hata Zanzibar, umekuwa ukisema: 'Sitawaangusha,nitakuwa mtumishi wa wote'. Na jana pia umeyarudia maneno hayo hapa Lumumba. Kurudiarudia kunaonesha kufilisika. Usifike huko.

Nafahamu na nakufahamu kuwa una maneno mengi. Unaweza kubadili maneno na hata kuyaleta matamu kuliko hayo. Kama huo ni msemo wako sawa.

Lakini,badilikabadilika kimaneno ili uvutie. Shauriyo, utapoteza wasikilizaji kwakuwa tu watakuwa wanasikia yale yale. Badilika Tingatinga!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Mbona ata lowasa juzi anaongea huku anatetemeka au hukuona mkuu?
 
Magufuli hakujiandaa kuwa rais na hajui kunadi sera zake.
Lowassa amejiandaa vilivyo kuwa rais ila hajui kunadi sera zake.
 
Back
Top Bottom