Kuna watu wamezaliwa kwa ajili ya kutumwa tu, ukimtuma kufanya jambo hakosei. Watu wa namna hii huona fahari kutumwa. Ni kama walivyo wanyampala gerezani. Ubaya wa watu aina hawawezi kujituma wao - hawana akili ya kubuni jambo na kulisimamia mpka likazaa matunda. Magufuli ni sample nzuri ya watu hawa. Akiwa rais sijui atakuwa anatumwa na Big Ben au yule Sungura mjanja wa msoga.
Sasa unaelekea 'kuboa'. Unarudiarudia maneno yale yale kila mahali unapohutubu,kwanini? Badili hotuba. Badili maneno. Kuanzia ukumbini Dodoma; uwanjani Dodoma, Dar es Salaam na hata Zanzibar, umekuwa ukisema: 'Sitawaangusha,nitakuwa mtumishi wa wote'. Na jana pia umeyarudia maneno hayo hapa Lumumba. Kurudiarudia kunaonesha kufilisika. Usifike huko.
Nafahamu na nakufahamu kuwa una maneno mengi. Unaweza kubadili maneno na hata kuyaleta matamu kuliko hayo. Kama huo ni msemo wako sawa.
Lakini,badilikabadilika kimaneno ili uvutie. Shauriyo, utapoteza wasikilizaji kwakuwa tu watakuwa wanasikia yale yale. Badilika Tingatinga!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Rais sio maneno ni vitendo liache jembe
Mkuu umenena vema. Nimemsikiliza Magufuri,kuhutubia mzito,nimemsikiliza Lowasa kuhutubia mzito. Wote maneno wanayatafuta. Tena kwa uchunguzi wangu,aheli ya magufuri kuliko Lowasa. Tunaenda kwenye kampeni,one mistake one goal.tatizo hilo si magufuli peke yake mpaka lowassa analo pia tatizo hilo linachangiwa na ccm yani maswala ya chama ni nape, mangula, na yule msomali ktk kuzunguka mikoani kukijenga chama ktk mikutano mbalimbali yenye watu wengi ndo unapata experience ya kuongea leo kama chama cha chadema wote wanajua kuongea coz wanafanya mikutano mingi na kupata experience ya kuongea
Hilo jina la jembe umempa nyie na likingia kutu (hasa huu ukanda wa pwani) msilaumu mtu. Wenye kumbukumbu mnakumbauka kuna mzee alipewa fagio la chuma, maji ya pwani yakalitia kutu likashindwa kufanya kazi sembuse jembe! Hata hivyo sisi tuliosoma naye (Mkwawa) tulimfahamu kwa jina la BOILER, kwa tabia yake ya kutoa maneno yasiyo na maana (aka vapour).
Hivyo kurudiarudia maneno haishangazi kwani kazi ya boiler huwa habadiliki ni kutoa uvuke uleule!