Dr. Magufuli (CCM) itashinda kwa zaidi ya 80%

sio mbaya hata wayahudi hawakumwamini YESU kama ni mwana wa MUNGU mpaka walipoona matukio mbali mbali kama giza kutanda mchana, kufufuka kwake ndivyo itakavyokuwa pindi masisiemu yatakaposhindwa
 
“Siku moja nilizungumza naye nikamuuliza wenzako wanachukua fomu za urais, mbona wewe hujaenda kuchukua, akanijibu hivi na mimi natosha kuwa Rais, nikamweleza wana CCM wenyewe wataamua kama unatosha ama hautoshi.

“Siku moja akasema ana shida ya kuja kuniona, nikamwambia njoo, alivyokuja akaniambia masuala ya madeni ya makandarasi... lakini baadaye akasema mzee nimekuja kukuaga naenda kuchuka fomu, lakini sitazungumza na waandishi wa habari... sasa nikamhoji watu watakujuaje?” alisema Kikwete.

Aliongeza kuwa kesho yake akasikia Dk Magufuli amechukua fomu; lakini amewakimbia waandishi.

Habarileo.

My take, mtu ambaye amekurupushwa hakujiandaa wala hakua na wazo la kuwa Rais tutamuamini vipi kumpa Taifa kuliongoza?



Hahaaaa ccm hawana jipya la kutuambia
 
Pamoja na joto na mihemko ya kisiasa na hiki ki changamoto ya wapiga kelel/wanywa viroba watani zetu wa jadi PAKAWA lakini CCM itashinda kwa kishindo zaid ya 80% na kupata viti vingi vya ubunge, maana wananchi wanaiamni zaid CCM kuliko SACCOS zisizo hata na Physical Address, hivi UKAWA ndo nini (kwa sauti ya Joti)
CCM mbele kwa mbele.

Utakuwa na hallucination!
 
Hata farao alijikuta mgumu mwisho wa siku atoweka juu ya uso wa nchi.na jeshi lake

Ccm jiandaeni mapemaa kuondoka madaralani
 
Jakaya akiingia madarakani tulikuway na Tembo wengi na Vifaru mpaka wanapita karibu na majumba yetu.
Leo anaondoka wanyama hao wamegeuka almasi,Ukienda kwenye hifadhi zetu bila darubini huwezi ona Tembo wala Kifaru.Utawala wa Ccm umeshindwa masikini kuwalinda.
Bado mwaka huu wanatuletea Magufuli tena wakijinasbu ikulu lazima warudi kwa njia yoyote ile,Watanzania tusikubali tena hawa watu watuongoze,This time ndio wanaenda kumalizia Vitembo na Vifaru vichahe tulivyobaki navyo.
Ikatae Ccm kwa faida ya vizazi vijavyo na rasilimali zetu.
Magufuli chini ya KINANA hata swala na Nyumbu tutawaona kwenye picha tu,October uwe mwisho wao na wanyama wetu wapone.

Cha kusikitisha na kuhuzunisha ni kuwa tembo wengi kwa sasa wanazaa wakati hawana pembe ama akiwa na pembe fupi fofauti na zamani,na hii ni kutokana na stress wanazozipata kutokana na kuwindwa na kuuawa.
Hii ni dhambi kwa watawala na viongozi wa vyama wanao fanya uwindaji na kuwaua hawa wanyama maana hapo nyuma baadhi ya tembo meno yao yalifikia uzito wa kilo 90 hadi 120/130 lakini kwa sasa sidhani kama waweza fikisha hata 50.
ONENI AIBU KUUA WANYAMA MAANA MUNGU ANA MAKUSUDI NAO.
MIJITU INA MISHAHARA MINONO LAKINI BADO INAFANYA UJANGIRI
 
Pamoja na joto na mihemko ya kisiasa na hiki ki changamoto ya wapiga kelel/wanywa viroba watani zetu wa jadi PAKAWA lakini CCM itashinda kwa kishindo zaid ya 80% na kupata viti vingi vya ubunge, maana wananchi wanaiamni zaid CCM kuliko SACCOS zisizo hata na Physical Address, hivi UKAWA ndo nini (kwa sauti ya Joti)
CCM mbele kwa mbele.

Wewe mwenzangu unaishi nchi gani ambayo ccm wanapendwa. Mbona wanazomewa kila kona.mimi ni mwana ccm lakini niliye nje ya box ushindi utapatikana baada ya kufanya kazi kubwa sana.Makundi ya urais bado yapo ili ushindi upatikane ni lazima umoja uwepo.bado kuna makundi ya ubunge na Udiwani ili ushindi upatikane ni lazima makundi hayo yavunjwe.
 
Yaani huhitaji akili kubwa kujua CCM watakufa kifo kibaya sana Oct. 2015..

Bila wasiwasi ..

Lowassa.............. 83%

Magufuli.............. 16%

Watu 95% wameshakichoka CCM... tatizo viongozi wa CCM wanapeana moyo ktk vikao na magazeti...hata wana CCM wengiii watampigia kura Lowassa Viongozi CCM hawataki kujua ukweli wa wananchi wengi...!!! watashangaaaa..
 
Back
Top Bottom