Dr. Magufuli ashindwa kuhutubia baada ya kuzomewa

Dr. Magufuli ashindwa kuhutubia baada ya kuzomewa

Hahaha Sasa mtu na akili timamu unamsikiliza magufuli akuambie nini?Hana jipya

Sasa ww tangu umeanza kumsikiliza Lowasa ameshakwambia kipi ukakielewa kama kweli una akili timamu?!
"Wanaomshabikia Lowasa wakapimwe akili"-Msigwa. Wahi wakakupime usije ukaanza kula magodoro ya sponji buree!
 
Unajua kitu nionacho ni kwamba kwa humu jf magufuli ana watu walioamua kumchukia pasipo sababu ya msingi, ingekuwa uchaguzi wanaopiga kura ni wana jf tu na madereva wa boda boda, magufuli angeshindwa kwa mbali ila ni kinyume kabisa!

Wewe subiri lowasa kuapishwa ccm huu ndio mwisho wenu
 
Sasa mitaa kama hiyo anafuata nini?? Hawana inteligensia yakuwashauri sehemu za kupita na ambazo hazifai kupita hasa kuhutubia? Hii ni kujifedhehesha kwa kweli......

Sehemu zote Tanzania hazifai kupita kwa sasa. Nilisema week iliyopita kwamba. Magufuli anaweza kuhutubia kwa amani sehemu ambayo tayari wameshaandaliwa watu ambao husombwa kwa malori na kulipwa na si vinginevyo. HAKUBALIKI MACHONI MWA WATANZANIA WENGI.
 
Tatizo la Magufuli anasimama popote kuhutubia bila kuangalia mazingira husika ili aongeze idadi ya mikutano tunayotangaziwa na Bulembo.

Mkuu ni wei kabisa....dakika kama hizi za majeruhi huwezi kufanya makosa kama haya ya kuchezea shillingi chooni......ni bora angepita kimyakimya...
 
Ni aibu! Ni fedheha! Ama kweli CCM imekufa! Watu hawataki kusikia hata harufu yake. Shuhudia mwenyewe. Hii imetokea leo hapa Dar tena zikiwa zimebakia siku 3 tu CCM iondolewa na kuzikwa!
https://youtu.be/NI_JKb9KJSc

Ndo maana chadema kimekuwa kama chama cha wavuta bangi, kwani kuzomea ni maadili ya kibangibangi kama itikadi yako haiendani na Makufuli fanya mambo yako, biashara ya kupewa pesa ili kuzomea ni tabia mbaya kwa viongozi wa chadema wanaofanya mchezo huo, kwanza wanawapa viroba, bangi na posho kidogo. kuzomea si dawa ya kupata utakacho, na kama hawa ccm wangekuwa pia na tabia za kipumbavu kama za hicho chama chenu wala kisingekuwa kimefikia hapa, ambapo nyie ss mnazomea. Lakini mjue kwamba tunahitaji rais wa watz wote pamoja na wazomeaji hao.

Naamin Mungu ni mwema, hawezi kutupatia viongozi wa kuzomeazomea wenzao.
 
Hao wahuni walioandaliwa wala kupiga kura hawatakwenda,as mwenyekiti wenu kasema kuna mkesha jumamosi wataishia kunywa viroba na jpili hawataweza kwenda vituoni,
 
Huyu Magufuli anaambiwa kabisa kuwa hupendwi na hujakidhi vigezo lkn hakomi. Haya sasa haya ndio matokeo yake kupatwa na aibu.
 
Mwingine huko Geita alifanyiwa FUJO baada ya kumtukana Lowassa.

Eti Lowassa anatoka Uchagani ya Masaini. Watu wakalianzisha ikabidi tu waweke Mziki na wakamtoa na kumleta Lowassa.

Hivi Uchagani ya Masaini ndiyo wapi? Huyu MFICCM kweli hazimtoshi....

 
Last edited by a moderator:
Sasa ww tangu umeanza kumsikiliza Lowasa ameshakwambia kipi ukakielewa kama kweli una akili timamu?!
"Wanaomshabikia Lowasa wakapimwe akili"-Msigwa. Wahi wakakupime usije ukaanza kula magodoro ya sponji buree!

Ametuambia misamaha ya kodi inayotolewa kwa Makampuni ya kigeni inatosha kutoa Elimu ya bure kuanzia chekechea mpaka Chuo Kikuu.
 
Mbona sijasikia akizomewa zaidi ya huyu mpuuzi anaechukua video na rafiki zake wakipiga kelele, tafute simu quality basi ..
 
Wahuni wale waleeeeeeee wanao lipiwaga viroba.

Unafikiri bila kusema maneno haya ungesema maneno gan ambayo yangekusuza roho? C mpige marufuku utengenezaji wa viroba? Hivi ni lazima upinge watu kulinda kura zao.
 
Jamiiforums siku hizi server ipo lumumba. Uzi huu audumu
 
Back
Top Bottom