Dr. Magufuli apiga kambi Morogoro kusimamia ujenzi daraja la Dumila lililosombwa na maji!

Lyong'o

Member
Oct 1, 2013
68
33
Dr. Magufuli aenda kupiga kambi Morogoro ama kusimamia mwenyewe ujenzi wa Daraja la Dumila lililopo mkoani Morogoro ambalo ni kiungo muhimu cha barabara ya Dodoma – Morogoro lililosombwa na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia tarehe 22.01.2014 na kusababisha magari kutopita kabisa ama yanayotoka upande wa Dodoma au Morogoro, mbaya zaidi hakuna njia nyingine zaidi ya hiyo.
Baadhi ya picha za Waziri Magufuli aliyepiga Kambi darajani hapo:

Kazi za ujenzi zikiendelea.jpg
Kazi za ujenzi zikiendelea
Waziri wa Ujenzi akikagua maeneo yaliyoharibika.jpg
Waziri wa Ujenzi akikagua maeneo yaliyoharibika
Waziri Magufuli akitoa maelekezo kwa Watendaji wa Tanroads.jpg
Waziri Magufuli akitoa maelekezo kwa Watendaji wa Tanroads
Sehemu ya barabara iliyozolewa na maji ya mto Mkundi.jpg
Sehemu ya barabara iliyozolewa na maji ya mto Mkundi
Waziri Magufuli katika mtambo.jpg
Waziri Magufuli katika mtambo
Kazi za ujenzi zikiendelea 1.jpg
Kazi za ujenzi zikiendelea
Kazi za ujenzi zikiendelea 2.jpg
Kazi za ujenzi zikiendelea

photo 1.JPG
Jamaa akielekeza tipa kumwaga mawe
photo 2.JPG
Kazi ikiendelea
photo 3.JPG
Jamaa anaonekana ameachoka, amejipumzisha juu ya gogo
photo 4.JPG
Akiwa na wananchi alipowahakikishia leo njia itafunguka

DR.MAGUFULI ALALA DARAJA LA DUMILA NA MAAFISA WAANDAMIZI WA WIZARA YA UJENZI NA TANROADS NA HATIMAE MAGARI YAANZA KUPITA BARABARA YA MOROGORO-DODOMA BAADA YA DARAJA LA DUMILA KUSOMBWA NA MVUA KUBWA JUZI (21.01.2014). GARI LA KWANZA LILIPITA MNAMO SAA NNE NA NUSU ASUBUHI YA LEO 23.01.2014

photo-2.JPG
Gari la kwanza kupita mnamo saa 4.30 leo asubuhi
photo.JPG
Hili ni gari la pili kupita Dr. Magufuli kwa mbali akielekeza lori ili lipite
photo 4.JPG
Dr.Magufuli akiongoza magari kupita
photo 3.JPG
Dr.Magufuli akiongea na kuwashukuru Wahandisi wa TANROADS na Wizara
photo 5.JPG
Akifuatilia na kuhakikisha magari yanapita
photo 1.JPG
Dr.Magufuli na Kaimu Mtendaji wa TANROADS Mhandisi Ako (Mwenye kofia Nyeupe)
photo 2.JPG
Akizunguka huku na kule





Hatimaye waziri wa ujenzi Dr. John Magufuli, ameruhusu kuanza kupita kwa malori yenye uzito wa zaidi ya tani saba,kwenye eneo la magole, katika daraja la mto Mkundi, ambalo tuta zake zilizolewa na maji kwa urefu wa mita sabini, kwenye barabara kuu ya Morogoro-Dodoma, na kusababisha magari na wasafiri wengine kushindwa kuvuka kwa siku tatu mfululizo.

 
Last edited by a moderator:
Huyu ndiye watanzania tuliyependezwa naye! Rais mtarajiwa akichukua form nitampa kura yangu, siyo wale wa Diaspora au bodaboda. Kibaya chajitembeza kizuri chajiuza, hakiitaji kufanya harambee wala kusema anammadui watakimbia nchi akiwa Rais, Bravo Magufuli.
 
Yaani Magufuli hadi kwenye maafa anapozi kupigwa picha?!!! Kwa wenzetu waliomakini barabara muhimu kama hiyo ungekuta suluhisho imepatikana ndani ya masaa sita !!! siyo mbwe mbwe za kupiga picha na kutuwekea kwenye mitandao! BTW ilikuwaje wale jamaa waliopata ajali pale Maseyu walibanwa kwa masaa 16 hadi wakafariki bila suluhisho? ... Mizigo ni Mizigo tu...wananchi hatutaki picha tunahitaji uwajibikaji....
 
Tunataka achukue hatua kwa mkandarasi wa ki-china aliyezembea kumaliza kazi hadi maafa, yuko sit toka 2009 hadi leo wanapiga deal tu.
 
Kujenga daraja ni jambo njema sana ila tuaitaji kujenga daraja la kuunganisha taaluma au utendaji wa kazi katika serekali yetu.
Mfano mzuri Mafuriko yametokea, je madaktari wanasubiri mpaka kipindipindu kitokee? wako wapi watu wamazingira au watu wakuelimisha jamii kuhusu magonjwa baada ya kutokea kwa mafuriko? magonjwa kama ya rift valley au Leptospirosis NKZ yanatokea baada ya mafuriko. kwa hiyo kikosi cha diseases preparedness kinatakiwa kishirikiane na taaluma zingine hili kuvunja (silos). watu hawana mahali pakulala, hawana chakula, mihondombinu ni shida. We need to work in team. serekali mpo au mpaka waje wazungu watuelimishe?
 
Muhongo na waliomtangulia wangelikuwa hivi, mgao wa umeme ungekuwa histori...
 
Huyu ndiye watanzania tuliyependezwa naye! Rais mtarajiwa akichukua form nitampa kura yangu, siyo wale wa Diaspora au bodaboda. Kibaya chajitembeza kizuri chajiuza, hakiitaji kufanya harambee wala kusema anammadui watakimbia nchi akiwa Rais, Bravo Magufuli.[


/FONT]



ntamshauri achukue form kwa kweli.
 
Dr. Magufuli aenda kupiga kambi Morogoro ama kusimamia mwenyewe ujenzi wa Daraja la Dumila lililopo mkoani Morogoro ambalo ni kiungo muhimu cha barabara ya Dodoma – Morogoro lililosombwa na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia tarehe 22.01.2014 na kusababisha magari kutopita kabisa ama yanayotoka upande wa Dodoma au Morogoro, mbaya zaidi hakuna hakuna njia nyingine zaidi ya hiyo.
Baadhi ya picha za Waziri Magufuli aliyepiga Kambi darajani hapo:

View attachment 134007
Kazi za ujenzi zikiendelea
View attachment 134008
Waziri wa Ujenzi akikagua maeneo yaliyoharibika
View attachment 134009
Waziri Magufuli akitoa maelekezo kwa Watendaji wa Tanroads
View attachment 134010
Sehemu ya barabara iliyozolewa na maji ya mto Mkundi
View attachment 134011
Waziri Magufuli katika mtambo
View attachment 134012
Kazi za ujenzi zikiendelea
View attachment 134013
Kazi za ujenzi zikiendelea


Dr.Magufuli pambana Mungu yupo atakuotesha na uwatumikie Watanzania ktk ngazi kubwa zaidi! Bravo Pombe!
 
Unapoona mheshimiwa waziri mzima anaongoza lorry kumwaga kifusi/mawe, ujue kuna tatizo kubwa; actually ni janga kubwa la kimfumo. This is clear indication of a system failure! Tanroads wako wapi? Kitengo cha maafa wako wapi? Very poor of us! Hatuwezi kuendesha nchi kwa mtindo wa kutegemea vipaji na juhudi za mtu binafsi! This is wrong! Suppose yangevunjika madaraja mawili au matatu, Dr. Magufuli angejigawa vipi kushughulikia yote matatu? We should think!

Watanzania wenzangu, tuyatafakari maisha yetu na maendeleo ya nchi yetu. Mtindo wa kusubiri kuongozwa na matukio hautatufikisha popote! It is tantamount to taking a good road to hell!

I submit.
 
Yaani Magufuli hadi kwenye maafa anapozi kupigwa picha?!!! Kwa wenzetu waliomakini barabara muhimu kama hiyo ungekuta suluhisho imepatikana ndani ya masaa sita !!! siyo mbwe mbwe za kupiga picha na kutuwekea kwenye mitandao! BTW ilikuwaje wale jamaa waliopata ajali pale Maseyu walibanwa kwa masaa 16 hadi wakafariki bila suluhisho? ... Mizigo ni Mizigo tu...wananchi hatutaki picha tunahitaji uwajibikaji....

Duh! Nikikumbuka ile habari baasi, kweli Magufuli na CCM yake ni wapumbavu sana, lkn hata Chadema ni wajinga tu, CUF wehu pia. NCCR Mageuzi machizi pia.

Utashangaa kwa nn wote nimewatukana yaani watu waliangukiwa na kontena masaa 16 hakuna msaada na hakuna hata mbunge aliyepeleka hii kitu Bungeni kumwajibisha waziri husika si wapumbavu wote hawa?
 
Back
Top Bottom