Rocky City
JF-Expert Member
- Nov 22, 2017
- 1,021
- 835
Nikiri kuwa Dumila ni mji mdogo unaopatikana wilaya ya Kilosa ambao kwa miaka ya hiv kalibuni umekuwa kwa kasi sana, ukichagizwa na uwepo wa kiwanda cha sukari umbali wa kama kama 30 hivi cha Mkulazi holding campany ambacho tunaambiwa ndio lengo la safari yake kule.
Wiki iliyopita nilikwenda kule eneo moja linalopatikana kule maana kuna madini eneo flani linaitwa inyunywe umbali wa km 16 kutoka dumila mjini, aise katika pitapita zangu nikapita shule moja inayoitwa Kwambe ambayo iko ndani ya kata ya Dumila, Mita 15 tu kutoka barabara kuu ya Dodoma, mita 15 hadi 20 (META).
Rais na viongozi wote wanapita hapo muda wote, yani kwa ukalibu huo hata waziri wa TAMISEMI akinywa maji ndani ya gari wanafunzi wakiwa makini wanaweza kumuona.
Jambo la ajabu mno na kushangaza nilikuta shule ile ina watoto wa kifugaji na wakulima, ndugu zangu shule ni chakavu, miundombinu mibovu, shule ina vyoo visivyo na milango wa bati, hilo halikuwa shida, shule nzima ina madawati 20.[emoji2][emoji2][emoji2].
Niliuliza kwa watu walio kuwa pale mmoja alidai shule ile ina wanafunzi kalibu 500 hivi. Nyie viongozi kuanzia wilaya nzima ya kilosa, mkoa mzima wa Morogoro na wengine shule hiyo hamuioni, au sababu ni shule ya wafugaji wengi?
Nashauri viongozi wa eneo hilo na Rais Samia utakuwa eneo hilo shule hiyo ni vyema ikalekebishwa, mazingira sio mazuri kabisa, saidieni kizazi hicho na jamii hiyo.
Magufuli alikuja na sera ya kupambana madawati nadhani alisaidia sikumbuki, SAMIA na wewe njoo na yako mama.