Dr Lwaitama: CCM wakimsimamisha Dr. Salim A. Salim watashinda Urais

Tuliaminishwa kuwa Salim ni mwarabu na hafai kuongoza Tz. Isitoshe alishiriki kwenye mauaji ya Karume. Wamteue basi halafu watuombie kabadilika lini.

'.........mh.rais wewe unajua kwamba nikwambia tusimamishe mkataba na richimond ukakataa....by El"ikifika saa kila mtu anajisafisha kivyake.
 
Katika watu wachache wenye bahati njema na vipaji vya kuongoza Dr Salim Ahmed Salim YUMO. Nimemfahamu huyu Mh. tangu nikiwa mdogo sana na yeye katika kusoma historia yake alianza uongozi kwa kuteuliwa kuwa Balozi nchini Misri akiwa na umri wa miaka 22 akiwa amehitimu kidato cha IV tu, just imagine na aliweza kumudu kazi za Balozi kama mwakilishi wa Zanzibar nchini Misri.

Iwapo CCM wakamteua kupeperusha bendera ya CCM kwenye kinyang'anyiro cha Urais MIMI NITAMPA KURA KUBWA YA NDIYO DR< SALIM AHMED SALIM

Kwanza hana kashfa yoyote ni mtu safi kisiasa, kijamii, kiuchumi na kiutamaduni nk.!!!!!
Nani alikuambia kwamba "aliweza kumudu kazi za balozi"?...katika kipindi hiki tulichopo haitawezekana kuwa na raisi kutoka Zanzibar.
 
Nani alikuambia kwamba "aliweza kumudu kazi za balozi"?...katika kipindi hiki tulichopo haitawezekana kuwa na raisi kutoka Zanzibar.

Kwanini haitowezekana kuwa na rais toka zanzibar? mkapa na kikwete si wabara si zamu ya wazanzibar au walishaacha kupokezana? au unamaanisha nini?
 
Wazanzibari hawatamkubali.
Isitoshe, ikiwa serikali ya muungano pia ndiyo serikali ya tanganyika inakuwaje kiongozi wa serikali ya tanganyika atoke zanzibar?

Tafuteni mwingine kwa ccm
Watu kama kina asha rose migiro hawajawahi kugombea hata nafasi ya ujumbe wa nyumba kumi na kushindanishwa na wagombea wengine. Tangu aingie siasa ni kubebwa kubebwa tu.
Hana jipya. Heri hata Anna Tibaijuka ambaye ameshaonyesha kuwa ana misimamo hasa kwenye mambo ya ardh.
Lakini kwani lazima rais atoke CCM?

Dr Salim kuwa Rais wa Tanzania 2015 ni KUTOWATENDEA HAKI WATANGANYIKA;2015 Rais wa TZ awe Dr Salim(MZNZ);Rais wa ZNZ awe ama Shein au Seif(MZNZ)!!Ipo wapi dhana ya balance ya uongozi kati ya nchi hizi 2!Je sio HAKI sasa kama Rais wa ZNZ katoka ZNZ basi Rais wa TZ nae atoke bara!Kwa maoni yangu Mzee Mwinyi atakuwa Rais wa mwisho kutoka ZNZ kuwa Rais wa Muungano otherwise unless ZNZ iweke kipengele kipya kwenye katiba yao kuruhusu "MMAKONDE"bila kujali kazaliwa UNGUJA AU pemba(ili mradi awe MTZ) awe na sifa kugombea U-Rais ZNZ!
 
Jamaa huyu ni mdini sana ataendeleza mbegu ya JK..Namkataa kwa 100%

mambo aliyoyakataza nyerere ndo haya mtu anasifa zote za kugombea hila haumtaki 7bu muislam kwahyo unataka mchungaji ndo awe rais,hv katika akili yako watu wanaoongoza kwa ukabila na udini ni akina nani km cyo wachaga kama hauamini nenda tra mpaka wanaongea kilugha ofisi na wote waliingia kipindi waziri wa fedha alikua mchaga,acha mawazo potofu akili zako na umri wako tofauti umri mkubwa akili kiduchu.
 
Endapo watamsimamisha kuwa mgombea basi mgombea mwenza ambae atakuwa makamu wa Rais atatoka Tz Bara. Je wakisema mgombea mwenza awe E Lowasa na ambae atakuwa makamu wa Rais na EL akalikubali hilo je hiyo 2015 itakua vipi. Tutambue kwamba tangu uteuzi wa CCM uliomwingiza Salim na kumwengua Lowasa je inawezekana kuwa wanachanga karata kwa staili ya aina yake? Kwa mtazamo wangu hapa naona makundi ndio yatakafanya kazi ya ziada kuhakikisha uteuzi wa Salim unakosa nguvu au mashiko ktk chama. Mwanzo watu walihisi Asha Rose Migiro ndie angegombea Urais 2015 kwa kisingizio cha ujinsia ndani chama kama walivyofanya kwa Spika. Vp kuhusu hili ama wameshaona Makinda amechafua anga la jinsia kwa kushindwa kusimamia uongozi madhubuti akiwa kama spika? Au nae anaandaliwa kuwa mgombea mwenza kwa kisingizio kile kile cha ujinsia(A Migiro)?. Naomba maoni yenu wadau.
Ikitokea Migiro kawa rais, na Makinda kawa makamu wa rais, nitakwenda Somalia kuomba uraia wakinipa, then nitaukana uraia wa Tanzania.
 
Utaratibu wa kupeana zamu kwa kiti cha urais aliuvuruga fastjet mwenyewe alipomkpokonya salim nafasi hiyo huku akijua hata chama chake ccm kilikuwa na kauli kwa salimu, leo akija na gia ya zamu ya wazanzibar na sisi tutasema zamu ya yao walimhonga JK
Mkuu,

Tukitaka kujadili zamu kwa kiti cha urais wa JMT ni lazima kwanza tujifanye wendawazimu. Zanzibar ni nchi, halafu nchi hiyo itoe raia wake akawe rais wa nchi nyingine tena yenye raia milioni 43 na zaidi! Unategemea hao raia milioni 43 kama wana akili timamu watampigia kura?
 
kidoogo napata picha kwamba watu wameichoka ccm na mfumo wao,na sio mtu wa ccm,nimeangalia michango ya watu humu ndani kuhusu huyu mh nahisi kama atasimama yeye kama (mgombea binafsi)anaweza kushinda maana hata watu wa vyama wanaweza kumpigia kura,sasa nimeamini watu wengi shida yao si chama bali ni mtu sahihi,ahsanten
Nadhani katiba haijaruhusu mgombea binafsi, na hata kama itaruhusu, Salim hawezi kushinda.
Salim hatokuwa na uwezo wa kuweka wakala kwenye kila kituo cha kupiga/kuhesabia kura kwa Tanzania nzima, watamuibia mpaka ashangae.

Mgombea wa CCM ambaye anaweza kuitisha CHADEMA kwenye kinyang'anyiro cha urais ni Lowasa pekee. Ili CCM ishinde, ni lazima iibe kura, na mtu shupavu pekee mwenye uwezo wa kuchora na kusimamia wizi huo ni jambazi Lowasa pekee. Kikwete atakuwa anamaliza muda wake kwa hiyo hatosaidia kwa nguvu zote kwenye wizi wa kura, na kambi yake itabaki inaning'inia hewani haina pa kusimamia.
 
ni kweli huyu jamaa na mbinu zake chafu ni wa kuangalia sana mimi naomba wamchakachue ccm wenziye huko waje na kapengele kuwa yeyote aliyewahi kuhusishwa na kashifa yeyote asigombee urais.
 
Ndugu wana JF nimekuwa na matumaini makubwa sana kwa vyama vya upinzani kuchukua madaraka 2015,ni kutokana na jinsi vyinavyoungwa mkono na wananchi hasa CHADEMA,na jinsi kilivyo na mikakati kama huu wa Movement For Change,na jinsi wanavyoanza kushirikiana na vyama vingine kama NCCR.

lakini matumaini yangu yanaanza kufifia baada ya kuona DK.Salim amerudishwa kamati kuu ya CCM!,wasiwasi wangu ni kuwa siku CCM wakiamua ndo awe mgombea wao itakuwaje?.Hofu yangu inatokana na ukweli kwamba huyu jamaa amekuwa na uzoefu wa uongozi muda mrefu hasa OAU baadaye AU,ni kiongozi asiyekuwa na makundi ndani ya CCM inamaana kuwa wana CCM wanaweza muunga mkono wote.

lakini kitendo cha rais Kikwete kumrudisha kamati kuu ni kumsafisha kuwa aliyovumishiwa wakati wa kugombea kuteuliwa mgombea CCM 2005 hayakuwa na maana ndo maana amemrudisha tena,lakini ni kiongozi ambaye hatajwi kwenye kashifa za kifisadi.

je CHADEMA kitakabiliana vipi na huyu jamaa ili asitinge ikulu,binafsi nimechoka kuiona CCM madarakani hata kama wangeweka malaika agombee nisingempa kura yangu.

ngoja nikupe shule kijana

dr. Salimu ni Mzanzibari, wenzetu hawautaki muungano.

wanataka muungano wa mkataba kama SADC,

sisi watanganyika kama wanavyotuita, tunataka serikari moja au tatu,

kama katiba mpya tutapitisha serikali moja labda anaweza awe Raisi,

au tukipitisha serikali tatu anaweza awe raisi wa shirikisho la la serikali ya Muungano.

nje ya hapo huku Tanganyika tutakuwa na raisi au waziri mkuu itategemea katiba itatamka vipi

sioni ni wapi atapata nafasi ya kuwa raisi wa Tanganyika
 
kumchagua labda ahame ccm maana hata akiwa ccm atabadilishwa tu ili kufuata taratibu za ccm sitaki kusikia ccm
 
mkuu conclusion yako na kwenye hizo bold unanichanganya
sababu umeeleza uwezekano wa yeye kuwa rais kutokana na mambo uliyotaja,halafu conclusion unasema huoni atapata wapi nafasi ya kuwa rais wa Tanganyika,si nalo mpaka katiba ijayo kama itaitambua Tanganyika yetu.vinginevyo wewe mwenyewe umeshaona uwezekano wa kuwa rais.
 
kumchagua labda ahame ccm maana hata akiwa ccm atabadilishwa tu ili kufuata taratibu za ccm sitaki kusikia ccm

........

Ni kweli wewe na mimi hatutaki kusikia ccm vipi wengine ambao bado wanasema hawachagui chama ila itategemea mgombea gani wanaye mtaka akiwa ccm au TLP,CUFnk unawasaidiaje?
 
daah huyu jamaa mimi nadhani umri wake umeenda na mikikimikiki ya urais sio mchezo hasa ukizingatia JK anaiacha nchi na chama chake vikiwa hoi hivyo twahitaji mpambnaj, sina shaka na uwezo wake wala usafi wake katika utendaji bali umri wake ndio unanipa waswasi.
 
Back
Top Bottom