Salim Ahamed Salim, yeye binafsi hana tatizo. Hata Mwalimu Julius Kambarage alimuona kama mtu amayefa kushika nafasi ya urais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania tangu 1985.
Kipindi cha Mzee Ruksa hasa kilikuwa cha Dr. Salim Ahamed Salim, lakini siasa za fitina, uzandiki na mizengwe za CCM ndizo zilizomnyima fursa ya kushika nafasi hii adimu.
CCM wakafanya fitina wakamuweka Mzee Ruksa. Kipindi cha 2005 CCM kiliendeleza siasa zilezile za uzandiki kwa kumzulia kashfa mbalimbali sio yeye peke yake aliyezulia kashfa, bali wagombea wote waliojitokeza kushindana na Kikwete, wote, walizulia jambo ama hili ama lile.
Matokea ya siasa zafitina, makundi na kuchafuana za wana CCM ndiyo zilizotufanya tukapata viongozi DHAIFU.
Tumefika mahali serikali inaua watu, wakristu na waislamu wanaanza kuuana, maandamano kila mahali na uchumi mbaya. Janga hili linawakumba hata walioliasisi na wanamtandao. Wanatamani kurudisha nyuma jua, ndipo wana mkumbuka Salimu.
Inawezekana anayekumbuka shuka kukiwa kumekucha mithili ya mlevi, ni Mwenyekiti wa CCM pekee yake kama ilivyokuwa kwa Nyerere kipindi kile cha 1985.
Kama kuna makundi mengine yenye malengo tofauti na kumpata kiongozi bora, basi hataupata uraisi. Kama wana CCM wamejifunza kwa makosa wakaamua kumchagua na kujutia dhambi zaozanyuma, basi yaweza kuwa nyota njema kwake.
Hata hivyo sasa hivi amezeeka amejaa uoga wa kuzuliwa jambo jingine baya zaidi. Kufaa kwake hata kama atafaa hawezi kufaa kwa kiwango kilekile cha 1985. Anaigopa mizengwe ya CCM hawezi kuthubutu kuleta jambo jipya.
........

Tatizo je CCM wataweza kumasafisha tope walilompaka?Ni mpaka pale wale waliokuwa kwenye mtandao watueleze ukweli na uongo juu ya matope yale waliompaka amasivyo bado hata yeye mwenyewe sidhani kama atakuwa willing kugombea nafasi hiyo.