Dr. Limbu: Ikulu Inanuka Rushwa Balaa!

Dr. Limbu: Ikulu Inanuka Rushwa Balaa!

Mlaleo

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2011
Posts
16,355
Reaction score
13,146
Ikulu inanuka rushwa

hon_dr_festus_bulugu_limbu_mp.jpg

Dr. F. B. Limbu.


img_5842.jpg



Ikulu imetajwa kuwa ni moja kati ya taasisi zinazonuka rushwa Tanzania kutokana na utendaji wake.Tuungane na Mwananchi kwa taarifa hiyo.


Hayo yamo katika mada iliyowasilishwa na Mbunge wa Magu, Dk Festus Limbu kwenye semina ya siku moja ya kuwajengea uwezo, wajumbe wa Kamati za Bunge za Kudumu za Bajeti, Hesabu za Serikali (PAC) na Hesabu za Serikali za Mitaa, (LAAC) kuhusu rushwa, iliyofanyika mjini Dodoma Ijumaa.


Katika semina hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Dk Limbu alisema: "Rushwa imeenea kila mahali, katika sekta na nyanja zote (horizontal) na kwa ngazi zote, kuanzia Ikulu hadi ofisi ya kitongoji, balozi, kaya na mtu binafsi."


Alisema kuwa rushwa hiyo inajidhihirisha kwa namna mbalimbali ikiwamo mipango mibovu ya Serikali, mashirika ya umma, mikataba mibovu, taratibu mbovu za ununuzi, ujangili, uhalifu, upendeleo na hongo.


Huku akisikilizwa kwa makini na wabunge, Dk Limbu alisema kwa mujibu wa Taasisi ya 2012 Corruption Perception Index iliyopima nchi 176 kwa rushwa, Tanzania inashika nafasi ya 102 ikiwa na alama asilimia 35, huku Rwanda ikitajwa kuwa na rushwa ndogo ya asilimia 53 duniani.


Naye Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo akiwasilisha mada yake, aliitupia lawama Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), kuwa ndiyo inayochelewesha kesi za rushwa wahusika wanaponaswa.


Alisema Takukuru hukamilisha upelelezi wa kesi kubwa tano kila mwaka, lakini hucheleweshwa na Ofisi ya DPP kutoa uamuzi wake kuwafikisha wahusika hao mahakamani, huku akiwaasa maofisa wa Serikali kutoingilia kazi za taasisi yake.


Akichangia mada hizo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utawala Bora, George Mkuchika alisema bado Takukuru haina meno katika utendaji wake na kwamba mfumo wa utawala uliopo , hauipi nguvu.
"Nimezunguka nchi mbalimbali duniani, hadi China huko kote taasisi zao ziko huru, zinamkamata mtu, zinamfungulia mashtaka na kumfikisha mahakamani bila kupitia kwa DPP, lakini mfumo wetu hauipi uhuru Takukuru," alisema akiongeza: "Takukuru inamkamata mtu kwa rushwa, inamfungulia mashtaka na baada ya hapo yanapelekwa kwa DPP, naye anaamua mtuhumiwa hana makosa,Takukuru ijitegemee, ipeleke watu moja kwa moja mahakamani."


Alisema pia kwamba rushwa imekuwa kitu cha kawaida Tanzania na kwamba watu wanaomba rushwa bila woga.
"Utakuta mtu anashughulikiwa jambo lake na watu wakimaliza wanamuuliza, sasa unatuacha-achaje?…," alisema na kuamsha kicheko kwa wabunge.


Baadhi ya waliochangia ni pamoja na Mbunge wa Ukonga, Eugene Mwaiposa aliyesema adhabu kwa wapokea na watoa rushwa ni ndogo wakati Maria Hewa alisema maofisa wa Takukuru hutoa siri za watu wanaokwenda kutoa taarifa za wanaodai rushwa kwani hata yeye yalimkuta.


Kwa Taarifa hii basi kila aliyeko Ikulu ni Mla Rushwa kuanzia getini kudadeki

DPP Hatufai maana kazi yake kuuliza ''unatuachaje achaje''

Watu wamezunguka zunguka nchi mbalimbali lakini hakika hawawezi fikia rekodi ya Mkulu wao mwenye nyumba inayonuka Rushwa....

Source Sunday Shomari Blogu



ff76State-House-Tanzania.jpg

Ikulu iliyotajwa kuwa inayonuka Rushwa
 
  • Thanks
Reactions: G11
Akichangia mada hizo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utawala Bora, George Mkuchika alisema bado Takukuru haina meno katika utendaji wake na kwamba mfumo wa utawala uliopo , hauipi nguvu.
“Nimezunguka nchi mbalimbali duniani, hadi China huko kote taasisi zao ziko huru, zinamkamata mtu, zinamfungulia mashtaka na kumfikisha mahakamani bila kupitia kwa DPP, lakini mfumo wetu hauipi uhuru Takukuru,” alisema akiongeza: “Takukuru inamkamata mtu kwa rushwa, inamfungulia mashtaka na baada ya hapo yanapelekwa kwa DPP, naye anaamua mtuhumiwa hana makosa,Takukuru ijitegemee, ipeleke watu moja kwa moja mahakamani.”

kila mtu analia na DPP, wabunge wanashindwa nini wakiwa bungeni kutunga sheria za kumpunguzia mamlaka ofisi ya DPP.?
 
Ndugu Dr.Limbu usituchanganye mimi binafsi nakukumbuka vizuri,wewe ulikuwa naibu waziri wa fedha wakati wa utawala wa Mkapa,muliuza mashirika ya uma kwa bei za kutupa na pia ulishiriki vikao vya baraza la mawaziri vilivyoamua kuwafukuza wananchi kwenye Ardhi yao uko Shinyanga,Geita na Mara kwa kisingizio cha uwekezaji.Sasa unataka kusema IKULU leo inanuka rushwa,Je maamuzi yenu ya utatautata wakati wa utawala wa swaiba wako Benjamini hayakusukumwa na rushwa?
 
once a politician felt a warm affection toward corruption,you need 100000 tanks,six fighter bombers, and a battalion of 750000 soldiers to oust him in office!
 
kila mtu analia na DPP,
wabunge wanashindwa nini wakiwa bungeni kutunga sheria za kumpunguzia
mamlaka ofisi ya DPP.?

Nchi ya kulia-lia hii... rais analia, waziri mkuu analia hadi anatoa machozi... PCCB inalia, wabunge wanalia, wananchi wanalia, mawaziri wanali etc....

Ngoja tuendelee kulia-lia labda tunawaza kupata majawabu ya matatizo yetu....
 
Hivi ile Budget ya Vitafunwa pale Magogoni Dr. Slaa alisemaga ni sh ngapi vile?
 
Itakuwa nchi ya malalamiko tu:

Mwanachi analalamika.Mtendaji wa kijiji analamika.Mtendaji wa kata analalamika.Katibu tarafa analalamika.Mkuu wa Wilaya analalamika.Mkuu wa Mkoa analamika.Waziri analalamika.RAIS naye analalamika-kwa OBAMA.

Na mimi nalalamika.
 
chama nisaidie hapa naona yako juu yangu sana.
 
Last edited by a moderator:
hapa cjaelewa nanukuu!!

" Tanzania
inashika nafasi ya 102
ikiwa na alama asilimia
35, huku Rwanda ikitajwa
kuwa na rushwa ndogo
ya asilimia 53 dunian "
 
Mi mwenyewe maeneo ya magogoni sikatizi siku hizi kutokana na harufu...
be specific...kuna watu wanaweza wakafikiri kuwa kuna harufu ya manukato...UKWELI NI KUWA KUNANUKA na hakunukii!!!
I love your creativity!!!
 
Ndugu Dr.Limbu usituchanganye mimi binafsi nakukumbuka vizuri,wewe ulikuwa naibu waziri wa fedha wakati wa utawala wa Mkapa,muliuza mashirika ya uma kwa bei za kutupa na pia ulishiriki vikao vya baraza la mawaziri vilivyoamua kuwafukuza wananchi kwenye Ardhi yao uko Shinyanga,Geita na Mara kwa kisingizio cha uwekezaji.Sasa unataka kusema IKULU leo inanuka rushwa,Je maamuzi yenu ya utatautata wakati wa utawala wa swaiba wako Benjamini hayakusukumwa na rushwa?

anaway sikumbuki vizuri katiba ya tanzania lakini nafikiri MANAIBU waziri si wajumbe wa baraza la mawaziri... I stand to be corrected!!!!
 
"Am fame on issues" by JK 2005

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Kwaufupi tu Limbu kasema Kikwetye anakumbatia RUHWA
 
hapa cjaelewa nanukuu!!

" Tanzania
inashika nafasi ya 102
ikiwa na alama asilimia
35, huku Rwanda ikitajwa
kuwa na rushwa ndogo
ya asilimia 53 dunian "

mkuu, hayo ni matokeo ya kuungaunga mambo wasiyoyajua na athari za kucopy na kupaste
 
hasa km kikwete anakumbatia rushwa unategemea kuna wanaochulia rushwa kweli? hakuna, mawaziri wanakula rushwa, wabunge rushwa, mikoa rushwa, wilaya rushwa hadi kitongoji rushwa... hv watz tumekuwaje!...
 
Back
Top Bottom