Dr. Limbu: Ikulu Inanuka Rushwa Balaa!

Dr. Limbu: Ikulu Inanuka Rushwa Balaa!

Na huyu anayelalama wakati
sheria ya takukuru inapitishwa alikuwa mbunge. Mibunge yote ya CCM hovyo
tu.

mkuu, bado hujashtuka tu? kuna watu humu jf kila kikucha wana kazi ya kuisafisha Rwanda na kuichafua Tanzania. we fuatilia tu kila siku lazima upuuzi wa aina hiyo uibuke
 
Mbona hapo ikulu panaonekana kama barabar in vi-pot hole au ni macho yangu??
 
hana lolote!ndio wale wale tu,nakumbuka mwaka 1995,alikuwa anagombea ubunge jimbo la magu,kwa tiketi ya nccr mageuzi,wakichuana na mzee Malaky levi lupondije,alikuwa anakuja pale shuleni ana tulisha wali wiki nzima na nyama,na enzi hizo wali shule za bodi ni kama kumuona mnyama kakakuona!na hata kwenze mahafari ya form 4,aligharamika kila kitu,ila alipigwa chini na mzee malaky!uchaguzi ule ulimghalimu sana.
 
hapa cjaelewa nanukuu!!

" Tanzania
inashika nafasi ya 102
ikiwa na alama asilimia
35, huku Rwanda ikitajwa
kuwa na rushwa ndogo
ya asilimia 53 dunian "

mkuu, hayo ni matokeo ya kuungaunga mambo wasiyoyajua na athari za kucopy na kupaste

Bila shaka swali lilikuwa (huwa linaulizwa in positive way) ni nchi gani yenye rushwa kwa kiwango kidogo (isiyo na rushwa)? Hivyo anayepata 100% ndiyo ambayo haina rushwa kabisa na anayepata 0.0001% ndiyo mwenye rushwa kwa kiwango kikubwa. Hivyo Rwanda (53) ni kiwango kidogo cha rushwa na Tanzania (35) ni iko juu kwa rushwa ki-ulinganisho. Hata hivyo nakubaliana na Lizaboni wanakopi na kupaste sana hawa waandishi; huenda wakati mwingine wanshindwa kujua mantiki ya anachokikopi na kuripoti.
 
chama nisaidie hapa naona yako juu yangu sana.
Mamndenyi
Hizo ni fitina za Chadema na makamanda wao; Ikulu panapigwa mzigo wa nguvu wa kuleta maendeleo ya watanzania; hizi kelele za watu ambao wameshindwa hata kujenga ofisi sisi hazituumizi kichwa!
 
Last edited by a moderator:
Wanasiasa wetu pamoja na viongozi wa serikali waandamizi wanachekesha kama siyo kushangaza.

Wabunge wanalalamika kila siku TAKUKURU haina meno na cha kushangaza hata Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utawala Bora, George Mkuchika na yeye anadai TAKUKURU haina meno!.

Haya makelele niya kujiosha na kujitakasa kisiasa huku wakikimbia majukumu yao kwa njia hii kwa vile karibia wote siyo wasafi ikichukuliwa kuwa siyo serikali pekee inayopaswa kupeleka hoja au mswaada bungeni wa marekebisho ya sheria peke yake.

Kwao wanaona bora waendelee kuwa na ofisi ya DPP kama ndiye ultimate dicider of corruption cases kwa vile wanaweza kumshake kwa njia yoyote wanayopenda na inakuwa rahisi kwake kuimaliza case iliyofika mahakamani na ambayo haijafika mahakamani bila kuulizwa kwa nini kwa vile tu ana nguvu kisheria za karibia na nguvu za 'Mungu'

Hakuna mwanasiasa au mfanyakazi wa serikali mwandamizi mwenye ubavu wa kujitia kitanzi cha kisiasa au kimaslahi mwenyewe.
 
Mi mwenyewe maeneo ya magogoni sikatizi siku hizi kutokana na harufu...

Mkuu wacha hizo sizitaki hizi mbichi zako. Sema tu haupiti Magogoni kwa sababu unaogopa kuitwa teja/mbwia unga kwani siku hizi pale pamekuwa nyumbani kwa mateja wa bongo fleva na soon machangu nao wataanza kuhamia pale. Kama mateja tu wa bongofleva wanageuza Ikulu ndiyo maskani yao unafikiri rushwa itakosekana pale? Yaani huyu Kikwete huyu jamani, kweli ni zaidi ya kituko.
 
Wanasiasa wetu pamoja na viongozi wa serikali waandamizi wanachekesha kama siyo kushangaza.

Wabunge wanalalamika kila siku TAKUKURU haina meno na cha kushangaza hata Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utawala Bora, George Mkuchika na yeye anadai TAKUKURU haina meno!.

Haya makelele niya kujiosha na kujitakasa kisiasa huku wakikimbia majukumu yao kwa njia hii kwa vile karibia wote siyo wasafi ikichukuliwa kuwa siyo serikali pekee inayopaswa kupeleka hoja au mswaada bungeni wa marekebisho ya sheria peke yake.

Kwao wanaona bora waendelee kuwa na ofisi ya DPP kama ndiye ultimate dicider of corruption cases kwa vile wanaweza kumshake kwa njia yoyote wanayopenda na inakuwa rahisi kwake kuimaliza case iliyofika mahakamani na ambayo haijafika mahakamani bila kuulizwa kwa nini kwa vile tu ana nguvu kisheria za karibia na nguvu za 'Mungu'

Hakuna mwanasiasa au mfanyakazi wa serikali mwandamizi mwenye ubavu wa kujitia kitanzi cha kisiasa au kimaslahi mwenyewe.

Ahsante kwa kuwaambia hawa Watawala,upo neutral sana kwenye masuala ya msingi kaka,KULA LIKE.
 
Si tumeambiwa CCM ni ukoo wa panya! Kwa hiyo hata yeye Dr. wangu ni hayohayo, msikie Mkuchika, kuna nini hapo? Waongeaji wote ndiyo waanzilishi pamoja na kwamba wamemkaribia Vasco da Gama!
 
Raisi mwenyewe anapokea pair sita za suti anauza nchi pande la loliondo anapewa mwarabu bila ajizi ,mara ooh anauza pande la ardhi ya bagamoyo wachina wajenge bandari na wakusanye fedha zao kwa miaka hamsini eti kuzuia motto wake anayetajwa kukamatwa china na madawa ya kulevya unategemea nini
 
kila mtu analia na DPP, wabunge wanashindwa nini wakiwa bungeni kutunga sheria za kumpunguzia mamlaka ofisi ya DPP.?

Tuwe na Independent Prosecutor kama nchi za wenzetu. Anaweza endesha mashitaka kwa matakwa ya wananchi na kwa kutumia private investigator. Anaweza hata anzisha uchunguzi juu ya Rais. Kama alivyo chunguzwa Clinton. Badala ya mfumo wa sasa ni pale serikali itapoona ina maslahi tuu ndio inafungua kesi.
 
Dr. Limbu naye ni mla rushwa mkubwa waulizeni pale bodi ya pamba anavyovuluga kwa kuajiri wafanyakazi kwa upendeleo na anavyotumia mali za bodi kwa matumizi binafsi yeye kama Mwenyekiti wa bodi ya pamba......MiCCM minafiki sana hiyo tuiondoe tuu 2015 ili kuondoa mfumu mbovu uliokaa miaka 50.
 
Nchi ya kulia-lia hii... rais analia, waziri mkuu analia hadi anatoa machozi... PCCB inalia, wabunge wanalia, wananchi wanalia, mawaziri wanali etc....

Ngoja tuendelee kulia-lia labda tunawaza kupata majawabu ya matatizo yetu....

Labda utafika wakati tutaishiwa machozi tuamua kufanya kitu cha maana badala ya kulia.
 
Mamndenyi
Hizo ni fitina za Chadema na makamanda wao; Ikulu panapigwa mzigo wa nguvu wa kuleta maendeleo ya watanzania; hizi kelele za watu ambao wameshindwa hata kujenga ofisi sisi hazituumizi kichwa!

Aaa chama, umekuwaje tena leo? Kwani Dr. Limbu kahamia chadema tangu lini? Au unamaanisha ni mamuluki wa chadema?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom