Dr. Limbu: Ikulu Inanuka Rushwa Balaa!

Dr. Limbu: Ikulu Inanuka Rushwa Balaa!

Khaa!! msemakweli ni mpenzi wa Mungu. Miye hapa ''Tanzania inashika nafasi ya 102 ikiwa na alama asilimia 35, huku Rwanda ikitajwa kuwa na rushwa ndogo ya asilimia 53 duniani'' pamenichanganya kwelikweli. Naomba wale vipanga wanieleweshe :bored:
 
hasa km kikwete anakumbatia rushwa unategemea kuna wanaochulia rushwa kweli? hakuna, mawaziri wanakula rushwa, wabunge rushwa, mikoa rushwa, wilaya rushwa hadi kitongoji rushwa... hv watz tumekuwaje!...
Katika semina hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Dk Limbu alisema: “Rushwa imeenea kila mahali, katika sekta na nyanja zote (horizontal) na kwa ngazi zote, kuanzia Ikulu hadi ofisi ya kitongoji, balozi, kaya na mtu binafsi.”
Huo ndo ukoo wa panya aliousema Mh.Nassari.. CCM ni kama ukoo wa panya; baba mwizi, mama mwizi, mtoto mwizi, kaka mwizi, dada mwizi, mjomba mwizi, shangasi mwizi, n.k, n.k
 
anza kuzibiri rushwa nyumbani kwako kisha nyoosha kidole kwa mwenzio.
 
This is pure nonsense. Limbu hana cha kutujuza kwa sasa kwani ni sehemu ya tatizo tulilonalo kwa sasa! Ni bora anyamaze!!
 
kila mtu analia na DPP, wabunge wanashindwa nini wakiwa bungeni kutunga sheria za kumpunguzia mamlaka ofisi ya DPP.?

Kwa bunge hili lililosheheni magamba haitakuja kuwa.hata hivyo mswaada wa sheri hiyo si ni lazima uwasilishwe na AG ambaye ni gamba?sasa Takukuru waanzie wapi?hata katiba haiwatambui,upo hapo?!!!
 
Ikulu inanuka rushwa

hon_dr_festus_bulugu_limbu_mp.jpg

Dr. F. B. Limbu.


img_5842.jpg



Ikulu imetajwa kuwa ni moja kati ya taasisi zinazonuka rushwa Tanzania kutokana na utendaji wake.Tuungane na Mwananchi kwa taarifa hiyo.


Hayo yamo katika mada iliyowasilishwa na Mbunge wa Magu, Dk Festus Limbu kwenye semina ya siku moja ya kuwajengea uwezo, wajumbe wa Kamati za Bunge za Kudumu za Bajeti, Hesabu za Serikali (PAC) na Hesabu za Serikali za Mitaa, (LAAC) kuhusu rushwa, iliyofanyika mjini Dodoma Ijumaa.


Katika semina hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Dk Limbu alisema: “Rushwa imeenea kila mahali, katika sekta na nyanja zote (horizontal) na kwa ngazi zote, kuanzia Ikulu hadi ofisi ya kitongoji, balozi, kaya na mtu binafsi.”


Alisema kuwa rushwa hiyo inajidhihirisha kwa namna mbalimbali ikiwamo mipango mibovu ya Serikali, mashirika ya umma, mikataba mibovu, taratibu mbovu za ununuzi, ujangili, uhalifu, upendeleo na hongo.


Huku akisikilizwa kwa makini na wabunge, Dk Limbu alisema kwa mujibu wa Taasisi ya 2012 Corruption Perception Index iliyopima nchi 176 kwa rushwa, Tanzania inashika nafasi ya 102 ikiwa na alama asilimia 35, huku Rwanda ikitajwa kuwa na rushwa ndogo ya asilimia 53 duniani.


Naye Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo akiwasilisha mada yake, aliitupia lawama Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), kuwa ndiyo inayochelewesha kesi za rushwa wahusika wanaponaswa.


Alisema Takukuru hukamilisha upelelezi wa kesi kubwa tano kila mwaka, lakini hucheleweshwa na Ofisi ya DPP kutoa uamuzi wake kuwafikisha wahusika hao mahakamani, huku akiwaasa maofisa wa Serikali kutoingilia kazi za taasisi yake.


Akichangia mada hizo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utawala Bora, George Mkuchika alisema bado Takukuru haina meno katika utendaji wake na kwamba mfumo wa utawala uliopo , hauipi nguvu.
“Nimezunguka nchi mbalimbali duniani, hadi China huko kote taasisi zao ziko huru, zinamkamata mtu, zinamfungulia mashtaka na kumfikisha mahakamani bila kupitia kwa DPP, lakini mfumo wetu hauipi uhuru Takukuru,” alisema akiongeza: “Takukuru inamkamata mtu kwa rushwa, inamfungulia mashtaka na baada ya hapo yanapelekwa kwa DPP, naye anaamua mtuhumiwa hana makosa,Takukuru ijitegemee, ipeleke watu moja kwa moja mahakamani.”


Alisema pia kwamba rushwa imekuwa kitu cha kawaida Tanzania na kwamba watu wanaomba rushwa bila woga.
“Utakuta mtu anashughulikiwa jambo lake na watu wakimaliza wanamuuliza, sasa unatuacha-achaje?…,” alisema na kuamsha kicheko kwa wabunge.


Baadhi ya waliochangia ni pamoja na Mbunge wa Ukonga, Eugene Mwaiposa aliyesema adhabu kwa wapokea na watoa rushwa ni ndogo wakati Maria Hewa alisema maofisa wa Takukuru hutoa siri za watu wanaokwenda kutoa taarifa za wanaodai rushwa kwani hata yeye yalimkuta.


Kwa Taarifa hii basi kila aliyeko Ikulu ni Mla Rushwa kuanzia getini kudadeki

DPP Hatufai maana kazi yake kuuliza ''unatuachaje achaje''

Watu wamezunguka zunguka nchi mbalimbali lakini hakika hawawezi fikia rekodi ya Mkulu wao mwenye nyumba inayonuka Rushwa....

Source Sunday Shomari Blogu



ff76State-House-Tanzania.jpg

Ikulu iliyotajwa kuwa inayonuka Rushwa

Acheni utani bana, ina maana na rais kikwete ananuka rushwa, au?
CC: njiwa, FaizaFoxy, ZeMarcopolo, Ritz, Hammy-D
 
Aaa chama, umekuwaje tena leo? Kwani Dr. Limbu kahamia chadema tangu lini? Au unamaanisha ni mamuluki wa chadema?


Hao madr. wa kuchovya hawajielewi wameshindwa kufundisha imebaki kuganga njaa tu; yeye alimpa nani rushwa hapo ikulu? na atuwekee wazi ili athibitishe maneno yake!
 
Hao madr. wa kuchovya hawajielewi wameshindwa kufundisha imebaki kuganga njaa tu; yeye alimpa nani rushwa hapo ikulu? na atuwekee wazi ili athibitishe maneno yake!

Ina maana na JK ni Dr. wa Kuchovya? maana Dr. Limbu yeye kaenda Shule...
 
Acheni utani bana, ina maana na rais kikwete ananuka rushwa, au?
CC: njiwa, FaizaFoxy, ZeMarcopolo, Ritz, Hammy-D
Wewe ndie wasema....
Mkuu ukitaka kumcopy mtu anza na herufi @ then unaandika nick name yake ndio atapata signal mfano MOSSAD II
 
Last edited by a moderator:
hapa cjaelewa nanukuu!!

" Tanzania
inashika nafasi ya 102
ikiwa na alama asilimia
35, huku Rwanda ikitajwa
kuwa na rushwa ndogo
ya asilimia 53 dunian "
Du hata mm Hesabu hiyo inanichanganya huwezi jua huyu Limbu anataka uraia wa Rwanda, maana kila kitu ni kufananisha ni hako kainchi wakati kana matatizo kibao lakini ataifa wanakaogopa.
leo tu BBC wanasema Mlinzi wa PK aliyetorokea Uganda km Mkimbizi (Innocent Kalisa) kapotea
na leo wiki 2 akiwa mikononi mwa askari
Limbi kachemsha kasahau alishakua jikoni na akapalilia Kambi ingine
 
Huyu Mbunge wa Magu hakukosea kabisa aliposema Ikulu inanuka rushwa.

 
Tanzania kwa sasa itakuwa imependa nafasi za juu baada safisha White house na Bandari
 
Back
Top Bottom