Amebaki Kingunge na Mkapa, Na yule Colonel mwenye uso wa chuma aliyekuwa mshauri mkuu wa MkapaKutuaga kwa Mzee Gama kunamaanisha "Wajamaa" wamemalizika Tanzania.
wakati ule JK alikuwa waziri wa fedha.Kuna tetesi mzee Gama alikuwa anahitaji fedha kwa ajiri ya uchaguzi wa CCM yeye akamnyima.Zikaanza bifu za chini kwa chini.RIP Dk Gama..
Namkumbuka mwaka 1995 katika mbio za uraisi CCM Muungwanaa alimlaumuu anatoa upendeleo kwa mgombea mojawapo (C.D.Msuya) na hivyoo hana imani naye.
Marehemu Gama alionekana kuupuziaa tuu hizoo tuhuma na kuwaita wagombea waliokuwepo watatu (Muungwana, Ben na Msuya) na kunywa nao chai pale ofisi zao za lumumba wakasonga na uchaguziiii....
Natumai muungwana atapeleka salamu za rambi rambi kwa kada wao huyuu mkongwee..
wenye Picha ya Dr. Gama tunaomba, maana kizazi kilicho mature wakati hayupo kwenye press arena hatumjui kwa sura isipokuwa kwa yale aliyoyatenda!
Pumzika Mzee Gama. Ulifanya kazi kubwa!
LAKINI....wakati Gama akiwa Mkuu wa JKT na Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, alishindwa kudhibiti ukabila:
Ktk Jeshi la kujenga Taifa aliajiri vijana wengi kutoka Mkoa wa Ruvuma wengi waliomaliza Darasa la Nane na kuwafanya ma-Afande. Kazi yao kubwa ikawa ni "kujenga" tabia ya ngono na wasichana wadogo waliomaliza Darasa la Nane waliojiunga na na JKT.
"Gama, huko kwako Jeshini, mabinti zetu hatuwaleti kuolewa na hao Maafande wako!"
Gama alishindwa kudhibiti tabia hiyo.
"Basi tutakubadilisha kazi."
Akapewa Ukurugenzi wa Usalama wa Taifa. Na badala ya kuajiri watu wenye elimu na uzalendo wa hali ya juu, Gama kawaleta ma-Afande wake, wengii wenye elimu duni! Utendaji kazi na hadhi ya idara hiyo ikadorora!
Hii haikumpendeza Rais Nyerere...ikabidi kufanya marekebisho makubwa na kumteua Hasnu Kitine aliyeajiri wasomi wenzake wengi.
Mtandao wa Gama ulisambatatishwa; ukaondoka na magari mengi ya Volkswagen ndogo - mengi yalikuwa, pengine, hayakuandikishwa!