Dr.Kitine ulimaanisha Omary Chambo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr.Kitine ulimaanisha Omary Chambo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by apolycaripto, Apr 29, 2011.

 1. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #1
  Apr 29, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 636
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Katika kipindi cha mahojiano mnamo tarehe 24/03/2011,Dr Hans Kitine mbali na mambo mengine alidiriki kuangazia ndani ya serikali hii kwa sasa na kusema moja kati vitu vinavyochangia ukosefu wa maadili ni pamoja na kuwapa watu vyeo bila kuwafanyia vetting kupitia vyombo vya usalama. Alidai kuna Katibu Mkuu mmoja ni mchafu kwa maana ya fisadi na watu wanamlalamikia japo hakumtaja jina lakini bado amepewa Wizara tena nyeti zenye fedha nyingi na anaendelea kufisadi kama kawaida.

  Tutambue maneno haya ya Dr. Kitine si ya kupuuzwa kwani ni Mzee na Bosi Mstaafu wa Usalama wa Taifa. Nimefanya uchunguzi kupitia kwa baadhi ya watu waliotizama na kumsikia katika mahojiano yale, wengi wamedai Katibu Mkuu anayezungumziwa ni Eng.Omary Chambo. Sina uthibitisho kwa maana ya ushahidi lakini ndiye anayetajwa.

  Nashauri suala la kujivua gamba kama inavyosemekana,kuelekee pia kwa hawa Makatibu Wakuu (ambao ndio technical figure na watendaji wakubwa ndani ya Serikali). Haiwezekani Mawaziri wao wachafuke kisha wao wakabaki salama hata kidogo. Kuyumba kwa Serikali kunachangiwa na hawa kwa kiasi kikubwa na si kuishia kwa Wanasiasa pekee. Kikwete hawa watu wanakutafuna hawa!
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Nilimsikiliza tena hiki kipindi kilirushwa mara mbili.

  Kitine alisema huyo katibu mkuu si wa wizara ya fedha (akaongeza kuwa wizara ya fedha haina uchakachuaji/pesa nyingi kama aliyoificha)

  Akasema ni wazi huyo katibu mkuu anajulikana A-Z na idara ya usalama na anashangaa kivipi anadumu mpaka leo.Aliongeza pamoja na waziri na naibu wake kuwa mzuri ila ni mzigo kuwa na huyu katibu mkuu)
   
 3. manenge

  manenge JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 280
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hata bila kumtaja jina lakini kutokana na ukweli kwamba taarifa zake zote zinajulikana na usalama wa taifa na bila shaka hata Mkulu anafahamu tabia yake na bado anampa hayo madaraka inaacha maswali mengi kuliko majibu juu uadilifu wa taasisi zetu zilizopewa madaraka ya kuteua wateule hao. kwa haraka utaona sio mtu mbaya ni mfumo mzima ni mbovu unahitaji mabadiliko makubwa.
   
 4. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 180
  Ingawa nakubaliana na ukweli kwamba wateuliwa wa Raisi ni lazima wafanyiwe 'veting' nasikitika kwamba kwa Tanzania hatua hii imetumiwa ipasavyo na wafanya 'veting' yaani maafisa wa usalama wa taifa kwa kupendekeza majina ya wenzao (Colleagues ) kiasi kwamba asilimia 90 ya viongozi tulionao (mawaziri, makatibu wakuu, wakuu mikoa n.k) ni maafisa wa usalama wa taifa. Wanatumia taarifa walizonazo kujinufaisha kwa kujipanga katika kila nafasi ya uongozi. Athari yake ni kuwa na watu 'Mabogus' kila kona ya uongozi wa nchi.
   
 5. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  usalama wa taifa ulikuwa enzi za mwalimu nyerere (Malehemu-Mungu amulaze pema). Kwa sasa kuna usalama wa masilahi ya watu; hivyo hoja ya kitine inakosa nguvu kwa maana ya usalama wa taifa wa sasa.
   
 6. m

  mkulimamwema Senior Member

  #6
  Apr 29, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani tusiyalaumu matawi na majani kwa kundondasha majani na matunda yaliyooza bali tulikate shina la mti husika,hivi inakuja akilini kuwalaumu makatibu wakuu na kusema aliyewateua ni safi ila wao ndio wachafu hapana kwani kabla ya kuwateua anapata taarifa zao na wakikosea anatakiwa kuwawajibisha.Tumelalamika mara ngapi pasipo bosi wao kuwakemea
   
 7. m

  mkulimamwema Senior Member

  #7
  Apr 29, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lakini naye Dk KITINE mwoga anashindwa nini kusema ukweli kwa kumtaja jina mbona akina Slaa hawaogopi,kama alikuwa hajajipanga asingeongea na kutuletea usumbufu kujua ni nani"there is no great wisdom like silence even fools are considered to be wise when they keep quet
   
 8. Silas Haki

  Silas Haki JF-Expert Member

  #8
  Apr 29, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 368
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwa haraka haraka ukiangalia wizara inayotia fora kwa ufisadi sasa hivi ni ya Nishati na Madini. Nafikiri hata Katibu wake ndo aliyekuwa anazungumziwa na Kitine. Angalia; Dowans + Richmond, IPTL, Songas, Buzwagi, North Mara, Mirerani, Golden pride, Tanesco. Kote huko ni mikataba hewa tu.
   
 9. k

  kabombe JF-Expert Member

  #9
  Apr 29, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 15,578
  Likes Received: 8,518
  Trophy Points: 280
  Apolycaripto unamjua DR.HASSAN KITINE?

  Ana kashfa ya kugushi risiti za matibabu hewa dola 30,000 kwa ajili ya "matibabu"ya mkewe mzungu walipokua Canada.
  Serikali ilifuatilia ikakuta hakuna mtu alietibiwa kwa jina na tarehe hiyo.
  Jamaa ana hasira tu,lakini ni fisadi wa kutupwa,anaswali sana siku hizi pale bakwata kinondoni,lakini ana kampuni linakopesha kwa riba 30%.

  Kwa imani yake haruhusiwi kula riba.

  Kitine hana moral authority ya kulipua watu,yeye mwenyewe bado ananuka
   
 10. k

  kayumba JF-Expert Member

  #10
  Apr 29, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Katibu mkuu wa wizara hii ni mpya na amepewa ukatibu mkuu juzi tu baada ya mikataba yote hiyo uliyotaja mkuu!

  Ukiongezea maelezo ya ziada yaliyotolewa "Wizara ina waziri na naibu wake mashuhuri" hapo utajua kuwa ni wizara ya Ujenzi.
   
 11. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #11
  Apr 29, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0

  Mfano rahisi wa hata hivyo vetting ni changa la macho ni pale hata yeye KITINE mwenyewe alipotumia nafasi yake kufoji mambo na matibabu ya mkewe sijui huko Canada na US.

  mambo yanabumbuluka wanaaanza kutajana safi sana waendelee hivyo hivyo kuonyosheana vidole. mwsiho wa siku wananchi tumeshaua CCM sio chama cha wananachi.
   
 12. J

  JokaKuu Platinum Member

  #12
  Apr 29, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,953
  Trophy Points: 280
  Kabombe,

  ..sasa hivi kuna ufisadi uliopita kiasi na kuvunja rekodi kiasi kwamba hata Kitine ambaye tunaelewa ana madudu yake anapata ujasiri wa kuukemea.

  ..hata Abdulrahman Kinana ambaye tunajua ni fisadi ktk uuzwaji wa Loliondo, ktk vikao vya CCM amekuwa na moral authority ya kuwakemea mafisadi wa awamu hii.
   
 13. k

  kabombe JF-Expert Member

  #13
  Apr 29, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 15,578
  Likes Received: 8,518
  Trophy Points: 280
  Joka Kuu,
  Fisadi ni fisadi tu hata akiiba mia.
  Tupe details za Kinana kuhusu ufisadi wa Loliondo
   
 14. J

  JokaKuu Platinum Member

  #14
  Apr 29, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,953
  Trophy Points: 280
  Kabombe,

  ..Muarabu aliyeuziwa Loliondo ni waziri wa ulinzi wa falme za Kiarabu. wakati mbuga ile inauzwa Kinana alikuwa yuko wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa. yeye alikuwa ndiyo kama agent wa hao waarabu in their dealings na serikali ya wakati ule.

  ..enzi zile kina Kinana ndiyo mawaziri, Tanzania ilikuwa imekosa heshima kiasi kwamba mawaziri[with diplomatic passports] walikuwa wanapekuliwa kabla ya kupanda ndege wakishukiwa kuwa wanabeba madawa ya kulevya.

  ..sasa leo hii ukiona Kinana au Kitine "wanawalipua" wana ccm wenzao, halafu hao wanaolipuliwa hawawezi kuwa-call out[kinana/kitine/..] kwa ufisadi waliopata kufanya huko zamani, ujue ccm imejaa uozo mtupu.
   
 15. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #15
  Apr 29, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Huyu mtoa mada wa ajabu sana!; kutoka katika maneno ya Kitine hadi kuchukua jina la Chambo mbona hamana 'connection' hii peke yake kwa watu wanao chuja na kufikiri lazima wahisi una-ugomvi na Omary Chambo tena unachuki naye, au la kunajambo lina maslahi kati yako na na yeye.

  Hii hoja yako haina namna yoyote hile jinala Chambo linaweza kuingia kama siyo matumizi mabaya ya JF kwa manufaha binafsi, kama hoja yako ni wizara yenye fedha nyingi, mbona Bajeti haionyeshi kama Wizara ya Chambo ndiyo iliyopewa fedha nyingi kuliko Wizara zingine! Kuna Wizara zilitengewa fedha nyingi zaidi ya Ujenzi na kupewa kipaumbele au hujui? Mbona hukuwazia Wizara ya fedha ambayo ndiyo inamiliki Hazina ya kaya?

  Ebu lete ushahidi Mkuu hapa unapiga soga tu!
   
 16. Mvuni

  Mvuni JF-Expert Member

  #16
  Apr 29, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mkuu, uko sahihi kabisa juu ya suala hili la watu wanaoitwa eti usalama wa taifa. Naomba ikumbukwe kuwa siku hizi hao jamaa wapo wapo tu kwa masilahi ya mtu, siyo Taifa kama wengi munavyo fikiri. Usalama wa Taifa ulikuwa enzi zangu mimi JKN, wandugu si-munakumbuka idara hii ilivyo kuwa adilifu enzi zangu? Nafadhaika na kusikitika sana pindi nisikiapo neno hili likitajwa eti "USALAMA WA TAIFA" Taifa lipi hilo wakati mambo yanaenda hovyo hovyo nao wamekodoa macho yao tu! Ningeishauri idara hiyo ibadilike na kurejesha maadili kama yale ya wakati wangu mimi JKN.
   
 17. J

  Jizalendo Member

  #17
  Apr 29, 2011
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tukisema tunaambiwa tumesema. Ukweli ni kuwa wachangiaji wa jamiiforum hawana jipya, wameishiwa sasa wanahaha tu.

  Kwanza kutangaza kuwa aliyelengwa na Kitine ni Omary Chambo ni maonevu na chuki kwa mtu. Kitine yupo, hivyo badala ya kuropoka muanzisha mada hii angemuuliza ili amueleze amemlenga nani.

  Pia amuulize Kitine maswali mengine ya msingi. Je ni kweli au la kuwa mkewe alihushi gharama za hospitali akisaidiwa naye. Jibu litakuwa ni kweli.

  Wanaosema Kitine ni CCM wamuulize je yeye ni mwanachama wa CCM hii leo? Jibu atasema hapana. Huyu bwana kwa hili hana kigugumizi.

  Kama si CCM anashamiria chama kipi? Atajibu CHADEMA. Kwa hiyo huyu ni mwanachama mwenzenu CHADEMA kisha anawapigia debe kwelikweli.

  Je inaipenda serikali inayoongozwa na JK. Haipendi hata kidogo kisha anawachukia sana akina Membe ambao walimlipua kwa uli wizi wake na wa mke wake.

  Msiropoke tu chunguzeni muyajuwe.
   
 18. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #18
  Apr 29, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Wao wasemana..sisi twalia
   
 19. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #19
  Apr 29, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Nafikiri ndugu yangu una maslahi binafsi na Omary Chambo, kwani wewe unataka kutuambia ni wizara ipi iliyopewa pesa nyingi zaidi ya miundombinu? Au unataka kusema ni wizara gani kwa sasa yenye waziri na naibu wake mashuhuri, panachuki gani hapo kama si kutetea ufisadi kama ilivyo kawaida ya wabongo hasa akiwa na maslahi?
   
 20. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #20
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  We ndio umegoma kufikiri kabisa!

  We unaweza kueleza hilo jina lilivyoingia hapo? Kama unaweza mbona hukufanya hivyo badala ya kunirushia lawama na kuengeza utata mwingine ambao huwezi hata kuuthibitisha? Eti nina maslahi na Chambo! Kati yangu na wewe kunagiza tororo, sikujui nawe hunijui, hivyo ni lazima ufahamu kuwa maelezo yako na ushawishi wako lazima utokane na taarifa yako ambayo inajieleza na kujithibitisha yenye pasipo mashaka yeyote, siyo Ubishi na ulazima kwa nguvu bila hoja na ushahidi.

  Pia, ufahamu kuwa kama hujui wizara zilizona bajeti kubwa kuliko hiyo ya chambo sasa unataka kuchangia nini na watu humu JF! maana hii ni sawa na mtoto wa darasa la pili ambaye hata 2x2 ni miujiza kwake! anaweza vipi kushiriki mijadala ya Calculus! au hesabu za kugawa sehemu! Mi sipo hapa kubishana bali kuelimishana lakini ni wajibu wako kufahamu kuwa lazima uwe na uwezo na uelewa wa msingi kabla ya kutaka au kujaribu kuchangia mawazo katika jamii yeyote.

  Uelewa wa msingi ni muhimu sana na ni vitu vya msingi ambavyo hata mtoto mdogo anaweza kuvielewa na haviitaji Elimu zaidi ya Elimu ya Msingi, vitu kama ni Wizara zipi au ipi ina bajeti kubwa kuliko zingine sitegemei kuwa kazi ya kumfundisha mtu humu JF maana Bunge la bajeti hufanyika hapa Tanzania kwa uwazi bila siri juu ya vipaumbele vya bajeti hivyo kutokujuwa ni dalili tosha ya uzembe na mtu wa namna hiyo sijui anatafuta nini hapa JF!

  Kuhusu uhusiano wa taarifa hii na ile ya Kitine na jinsi Jina Omary Chambo lilivyoainishwa hapa kama wewe uoni hakuna uhusiano basi jaribu kujiuliza wewe mwenyewe na jipime mwenyewe ulipo!
   
Loading...