Dr.Kitine ulimaanisha Omary Chambo?

Dr.Kitine ulimaanisha Omary Chambo?

:bored:
We ndio umegoma kufikiri kabisa!

We unaweza kueleza hilo jina lilivyoingia hapo? Kama unaweza mbona hukufanya hivyo badala ya kunirushia lawama na kuengeza utata mwingine ambao huwezi hata kuuthibitisha? Eti nina maslahi na Chambo! Kati yangu na wewe kunagiza tororo, sikujui nawe hunijui, hivyo ni lazima ufahamu kuwa maelezo yako na ushawishi wako lazima utokane na taarifa yako ambayo inajieleza na kujithibitisha yenye pasipo mashaka yeyote, siyo Ubishi na ulazima kwa nguvu bila hoja na ushahidi.

Pia, ufahamu kuwa kama hujui wizara zilizona bajeti kubwa kuliko hiyo ya chambo sasa unataka kuchangia nini na watu humu JF! maana hii ni sawa na mtoto wa darasa la pili ambaye hata 2x2 ni miujiza kwake! anaweza vipi kushiriki mijadala ya Calculus! au hesabu za kugawa sehemu! Mi sipo hapa kubishana bali kuelimishana lakini ni wajibu wako kufahamu kuwa lazima uwe na uwezo na uelewa wa msingi kabla ya kutaka au kujaribu kuchangia mawazo katika jamii yeyote.

Uelewa wa msingi ni muhimu sana na ni vitu vya msingi ambavyo hata mtoto mdogo anaweza kuvielewa na haviitaji Elimu zaidi ya Elimu ya Msingi, vitu kama ni Wizara zipi au ipi ina bajeti kubwa kuliko zingine sitegemei kuwa kazi ya kumfundisha mtu humu JF maana Bunge la bajeti hufanyika hapa Tanzania kwa uwazi bila siri juu ya vipaumbele vya bajeti hivyo kutokujuwa ni dalili tosha ya uzembe na mtu wa namna hiyo sijui anatafuta nini hapa JF!

Kuhusu uhusiano wa taarifa hii na ile ya Kitine na jinsi Jina Omary Chambo lilivyoainishwa hapa kama wewe uoni hakuna uhusiano basi jaribu kujiuliza wewe mwenyewe na jipime mwenyewe ulipo!

Kwa aliyemsikiliza kwa makini Dr. Kitine alipokuwa akizungumzia suala la vetting na uadilifu wa watendaji wetu wakuu serikalini , na hasa uadilifu wa viongozi wetu hutapata shida ya kumfahamu mtu anayezungumziwa hapa ni nani! Aliyeanzisha uzi huu alitaka kutufikirisha bongo zetu tutafakari na kuoanisha maelezo ya Dr. Kitine, bosi wa zamani wa usalama wa taifa na alichomaanisha.

Hapa hatuangalii Dr. Kitine aliboronga wapi, alichemsha, alifoji....sisi tunachoangalia kwa kushikana uchawi na kutajana wao kwa wao tunafaidikaje ktk kuwa-identify mafisadi na wenye magamba yao? Acheni watajane na wanapomwaga mchele hadharani sisi tunauchakura na kuutumia.

Binafsi naungana kabis na mtoa hoja hii kwani mlengwa hapa ni Eng. Omari Chambo, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Miundombinu na sasa Uchukuzi. Jamaa ni fisadi aliyekubuhu, uwezo wake wa kazi ni mdogo mno! Nafanya naye kazi namfahamu! Wakati mwingine huwa tunajiuliza JK alimpa madaraka makubwa kwa lipi????? Alipoteuliwa kuwa Naibu Katibu mkuu wa Miundombinu alikuwa akitokea Wizara ya Nishati na Madini. Utendaji wake na nafasi aliyopewa ulizua mjadala kwani wengi tuliamini ni kutokana na kulipa fadhila. Watu wamediriki hata kusema kwa kuwa ni mtoto wa fundi wa JK (baba yake alikuwa mganga maarufu) na JK hakuona namna nyingine ya kulipa fadhila ila kumpa cheo hicho.

Kuteuliwa kwake kuwa Naibu Katibu Mkuu watu walipigwa mshangao, maana hawakumtegemea kwa waliomjua vema kupewa nafasi hiyo. Bado tukiendelea kushangaa ktk kipindi kifupi Dr. Bukuku aliyekuwa Katibu Mkuu Miundombinu aliteuliwa kuwa Naibu Gavana BOT na nafasi yake ikashikwa na Chambo. JK kumteua Chambo kuwa Katibu Mkuu kulizidisha mshangao kwa baadhi yetu. Hivi inakuwaje mtu ambaye ameonyesha uwezo mdogo akiwa Naibu Katibu mkuu ktk wizara nyeti anapewa Ukatibu mkuu wakati issue za migogoro ya Bandari, TICTS, TAZARA, TRL, ATC etc imepamba moto! Viatu vya Bukuku vilikuwa vikubwa sana kumtosha Bw. Chambo!

Bw. Chambo alizidi kulikoroga, alivuruga wafanyakazi pale wizarani, hakuwa msikivu wala hakushaurika. Ni mtu mwenye kiburi na majivuno, akiwatishia walio chini yake kuwa yeye ni mteule wa Rais na amekula kiapo ikulu hivyo kama wao hawajateuliwa na Rais na hawajala kiapo ikulu hawana ubavu kwake. Kwa kuwa ni mtu mvivu, hajuwi kazi na asiyekuwa tayari kujifunza kazi aliwagawa wafanyakazi kwa vitisho, kuwahamisha na kuwa minyia asiowataka. Lakini mbaya zaidi anatumia muda mwingi kufukuzia miradi yenye pesa.

Kumbukeni wizara ya Miundombinu ni mojawapo kati ya wizara zinazotengewa fedha nyingi ktk bajeti ya serikali. Naomba nitoe mfano mmoja tu, Bw. Chambo alikuwa rafiki wa karibu na mtendaji mkuu wa TANROADS aliyepita, Bw. Ephraem Mrema, ambaye kuna wakati vyombo vya habari vilikuwa vikimuandika sana kuwa ni mbadhirifu, hana utawala wa sheria, anafukuza watendaji wakuu wa Wakala huo n.k. Lakini Wa-TZ wengi hawakujua kiiini cha mgogoro huo.

Bw. Chambo alichangia kwa % kubwa mno. Akijua fedha nyingi za barabara zinapita TANROADS ambako alizoea kula bila kunawa, alitaka kuwa na control ya kila kitu na ndipo ulipoanza kufukuta mgogoro wa chini kwa chini kati ya Chambo na Mrema, ambaye alianza kumwekea ngumu Chambo asiendelee kufisadi fedha za miradi ya barabara. Kwa kuwa Bw. Mrema alikuwa ni mtu jasiri asiyetikiswa hata ukiwa na mapembe alithubutu kumwonyesha Chambo mipaka ya kiutendaji inapoanzia na kuishia ili asimwingilie wakati akitekeleza majukumu yake.

Eng. Chambo kwa udhaifu wake na ukaribu wake na JK aliukuza mgogoro kati ya wizara na TANROADS, zaidi alianza kutumia magazeti na vyombo vya habari akiungana na mahasimu wa Mrema, ambao walikuwa wamesimamishwa kazi kwa kutokuwa na sifa ili kummaliza Mrema. Bila kuangalia kazi nzuri iliyofanywa na Bw. Mrema ktk kipindi chake zikaenezwa sifa mbaya kwa sababu tu aliwazibia mianya ya ulaji wa fedha za TANROADS kama walivyozoea.

Bw. Chambo hakuishia hapo, amekuwa akikwamisha miradi mingi inayosimamiwa na Mashirika, Taasisi na Wakala zilizo chini ya wizara yake. Hatowi maamuzi kwa masuala yanayohiyaji approval yake kwa wakati, hana muda wa kupitia mafaili ya ofisi kwa wakati hivyo kuchelewesha kazi za ofisi, amekuwa akiwa-frustrate wawekezaji hasa ktk sekta za bandari, viwanja vya ndege, reli, ATC n.k. amekuwa akikwamisha pia uteuzi wa wajumbe wa Bodi mbalimbali na mbaya zaidi kutothamini maoni, michango ya Watendaji wakuu wa Mashirika, Taasisi na Wakala zilizo chini ya wizara yake. Kuwatishia kuwafukuza kazi na kukatisha mikataba ya viongozi hao – kikubwa anataka kukatiwa pesa kwenye kila miradi inayoendelea.

Baadhi yetu tunajiuliza, tabia za mtu huyu na mapungufu yake yameshalalamikiwa sana na hata uteuzi wake umekuwa wa kubebwa kulinganisha na uwezo wake lkn hakuna kinachofanyika. Wafanyakazi wa wizarani wamechoshwa na mtu huyo lkn kwa kuwa ni mtoto wa fundi haguswi na mambo yanaenda shanghala baghala yet nobody cares! Awamu ya pili ya JK baada ya kupangua wizara na kuigawa wizara ya Miundombinu kutenganisha Ujenzi na Uchukuzi, Bw. Chambo alipoona Bw. Magufuli na Mwakyembe, ambao ni wachapa kazi hodari wameteuliwa kuongoza wizara ya Ujenzi, kabla hata hajateuliwa alianza mwenyewe kiaina....alijing’atua na kujipeleka Uchukuzi kukimbia kasi ya Bw. Magufuli ambayo kwa namna yoyote ile kasi yake asingeiweza! Sasa bw. Chambo yupo Wizara ya Uchukuzi ambako kuna mawaziri pia very weak (Kuna Nundu na Mfutakamba). Huko anapumua na akiendelea na tabia zake za kuwavuruga watendaji wakuu.

Wengine sisi tunajiuliza watendaji mabomu kama akina Chambo kukalia wizara nyeti kama hizo na huku hakuna delivery yoyote, ni kwa namna gani JK atatekeleza ahadi alizotumwagia wakati wa kampeni???? Ahadi za kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa Sijuwi Bukoba, Kigoma chini ya akina Chambo zitawezekana? Ahadi za kununua meli mpya na vivuko zitawezekana wakati watu wanaangalia matumbo yao zaidi? Lini tutanzisha shirika letu imara la ndege huku akina Chambo wanawadharau wataalamu na maoni na mapendekezo yao?

Dr. Kitine alimlenga Eng. Chambo kama mmoja wa Makatibu wakuu bomu, fisadi na uteuzi wake umelalamikiwa sana. Kuthibitisha haya tafuteni watu wa wizara ya Miundombinu (sasa Ujenzi na nyngine Uchukuzi) mtapata data za Eng. Chambo ni nani? Halafu tunashangaa kwanini mambo hayaendi? Nchi tajiri kama Tanzania haina hata reli ya kujivunia, ndege yetu yenye kupeperusha bendera na nembo ya TZ iko wapi? Bandari za uhakika zitakazotuingiza ktk soko la ushindani la pamoja la A. Mashariki (East African Common Market) ziko wapi?

Ili nchi iendelee inahitaji ardhi, watu siasa safi na uongozi bora. Kwa wa-TZ vyote vipo isipokuwa Uongozi bora ni zero!
 
:Baadhi yetu tunajiuliza, tabia za mtu huyu na mapungufu yake yameshalalamikiwa sana na hata uteuzi wake umekuwa wa kubebwa kulinganisha na uwezo wake lkn hakuna kinachofanyika. Wafanyakazi wa wizarani wamechoshwa na mtu huyo lkn kwa kuwa ni mtoto wa fundi haguswi na mambo yanaenda shanghala baghala yet nobody cares! Awamu ya pili ya JK baada ya kupangua wizara na kuigawa wizara ya Miundombinu kutenganisha Ujenzi na Uchukuzi, Bw. Chambo alipoona Bw. Magufuli na Mwakyembe, ambao ni wachapa kazi hodari wameteuliwa kuongoza wizara ya Ujenzi, kabla hata hajateuliwa alianza mwenyewe kiaina....alijing'atua na kujipeleka Uchukuzi kukimbia kasi ya Bw. Magufuli ambayo kwa namna yoyote ile kasi yake asingeiweza! Sasa bw. Chambo yupo Wizara ya Uchukuzi ambako kuna mawaziri pia very weak (Kuna Nundu na Mfutakamba). Huko anapumua na akiendelea na tabia zake za kuwavuruga watendaji wakuu.
Kama ni mteule wa Rais.. atajihamisha vipi mwenyewe? mbona haijakaa vizuri hii?
Out of curiosity!
 
....................Kumbukeni wizara ya Miundombinu ni mojawapo kati ya wizara zinazotengewa fedha nyingi ktk bajeti ya serikali. Naomba nitoe mfano mmoja tu, Bw. Chambo alikuwa rafiki wa karibu na mtendaji mkuu wa TANROADS aliyepita, Bw. Ephraem Mrema, ambaye kuna wakati vyombo vya habari vilikuwa vikimuandika sana kuwa ni mbadhirifu, hana utawala wa sheria, anafukuza watendaji wakuu wa Wakala huo n.k. Lakini Wa-TZ wengi hawakujua kiiini cha mgogoro huo.

Bw. Chambo alichangia kwa % kubwa mno. Akijua fedha nyingi za barabara zinapita TANROADS ambako alizoea kula bila kunawa, alitaka kuwa na control ya kila kitu na ndipo ulipoanza kufukuta mgogoro wa chini kwa chini kati ya Chambo na Mrema, ambaye alianza kumwekea ngumu Chambo asiendelee kufisadi fedha za miradi ya barabara. Kwa kuwa Bw. Mrema alikuwa ni mtu jasiri asiyetikiswa hata ukiwa na mapembe alithubutu kumwonyesha Chambo mipaka ya kiutendaji inapoanzia na kuishia ili asimwingilie wakati akitekeleza majukumu yake..........................

Hapo juu ndipo umeharibu mazee..........Mrema, Chambo wote ni bogus and disastrous..........wote wameliingizia Taifa hasara kubwa sana sana..................na madeni makubwa ajabu....kutokana na maamuzi yao..........
 
:bored:

Kwa aliyemsikiliza kwa makini Dr. Kitine alipokuwa akizungumzia suala la vetting na uadilifu wa watendaji wetu wakuu serikalini , na hasa uadilifu wa viongozi wetu hutapata shida ya kumfahamu mtu anayezungumziwa hapa ni nani! Aliyeanzisha uzi huu alitaka kutufikirisha bongo zetu tutafakari na kuoanisha maelezo ya Dr. Kitine, bosi wa zamani wa usalama wa taifa na alichomaanisha.

Hapa hatuangalii Dr. Kitine aliboronga wapi, alichemsha, alifoji....sisi tunachoangalia kwa kushikana uchawi na kutajana wao kwa wao tunafaidikaje ktk kuwa-identify mafisadi na wenye magamba yao? Acheni watajane na wanapomwaga mchele hadharani sisi tunauchakura na kuutumia.

Binafsi naungana kabis na mtoa hoja hii kwani mlengwa hapa ni Eng. Omari Chambo, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Miundombinu na sasa Uchukuzi. Jamaa ni fisadi aliyekubuhu, uwezo wake wa kazi ni mdogo mno! Nafanya naye kazi namfahamu! Wakati mwingine huwa tunajiuliza JK alimpa madaraka makubwa kwa lipi????? Alipoteuliwa kuwa Naibu Katibu mkuu wa Miundombinu alikuwa akitokea Wizara ya Nishati na Madini. Utendaji wake na nafasi aliyopewa ulizua mjadala kwani wengi tuliamini ni kutokana na kulipa fadhila. Watu wamediriki hata kusema kwa kuwa ni mtoto wa fundi wa JK (baba yake alikuwa mganga maarufu) na JK hakuona namna nyingine ya kulipa fadhila ila kumpa cheo hicho.

Kuteuliwa kwake kuwa Naibu Katibu Mkuu watu walipigwa mshangao, maana hawakumtegemea kwa waliomjua vema kupewa nafasi hiyo. Bado tukiendelea kushangaa ktk kipindi kifupi Dr. Bukuku aliyekuwa Katibu Mkuu Miundombinu aliteuliwa kuwa Naibu Gavana BOT na nafasi yake ikashikwa na Chambo. JK kumteua Chambo kuwa Katibu Mkuu kulizidisha mshangao kwa baadhi yetu. Hivi inakuwaje mtu ambaye ameonyesha uwezo mdogo akiwa Naibu Katibu mkuu ktk wizara nyeti anapewa Ukatibu mkuu wakati issue za migogoro ya Bandari, TICTS, TAZARA, TRL, ATC etc imepamba moto! Viatu vya Bukuku vilikuwa vikubwa sana kumtosha Bw. Chambo!

Bw. Chambo alizidi kulikoroga, alivuruga wafanyakazi pale wizarani, hakuwa msikivu wala hakushaurika. Ni mtu mwenye kiburi na majivuno, akiwatishia walio chini yake kuwa yeye ni mteule wa Rais na amekula kiapo ikulu hivyo kama wao hawajateuliwa na Rais na hawajala kiapo ikulu hawana ubavu kwake. Kwa kuwa ni mtu mvivu, hajuwi kazi na asiyekuwa tayari kujifunza kazi aliwagawa wafanyakazi kwa vitisho, kuwahamisha na kuwa minyia asiowataka. Lakini mbaya zaidi anatumia muda mwingi kufukuzia miradi yenye pesa.

Kumbukeni wizara ya Miundombinu ni mojawapo kati ya wizara zinazotengewa fedha nyingi ktk bajeti ya serikali. Naomba nitoe mfano mmoja tu, Bw. Chambo alikuwa rafiki wa karibu na mtendaji mkuu wa TANROADS aliyepita, Bw. Ephraem Mrema, ambaye kuna wakati vyombo vya habari vilikuwa vikimuandika sana kuwa ni mbadhirifu, hana utawala wa sheria, anafukuza watendaji wakuu wa Wakala huo n.k. Lakini Wa-TZ wengi hawakujua kiiini cha mgogoro huo.

Bw. Chambo alichangia kwa % kubwa mno. Akijua fedha nyingi za barabara zinapita TANROADS ambako alizoea kula bila kunawa, alitaka kuwa na control ya kila kitu na ndipo ulipoanza kufukuta mgogoro wa chini kwa chini kati ya Chambo na Mrema, ambaye alianza kumwekea ngumu Chambo asiendelee kufisadi fedha za miradi ya barabara. Kwa kuwa Bw. Mrema alikuwa ni mtu jasiri asiyetikiswa hata ukiwa na mapembe alithubutu kumwonyesha Chambo mipaka ya kiutendaji inapoanzia na kuishia ili asimwingilie wakati akitekeleza majukumu yake.

Eng. Chambo kwa udhaifu wake na ukaribu wake na JK aliukuza mgogoro kati ya wizara na TANROADS, zaidi alianza kutumia magazeti na vyombo vya habari akiungana na mahasimu wa Mrema, ambao walikuwa wamesimamishwa kazi kwa kutokuwa na sifa ili kummaliza Mrema. Bila kuangalia kazi nzuri iliyofanywa na Bw. Mrema ktk kipindi chake zikaenezwa sifa mbaya kwa sababu tu aliwazibia mianya ya ulaji wa fedha za TANROADS kama walivyozoea.

Bw. Chambo hakuishia hapo, amekuwa akikwamisha miradi mingi inayosimamiwa na Mashirika, Taasisi na Wakala zilizo chini ya wizara yake. Hatowi maamuzi kwa masuala yanayohiyaji approval yake kwa wakati, hana muda wa kupitia mafaili ya ofisi kwa wakati hivyo kuchelewesha kazi za ofisi, amekuwa akiwa-frustrate wawekezaji hasa ktk sekta za bandari, viwanja vya ndege, reli, ATC n.k. amekuwa akikwamisha pia uteuzi wa wajumbe wa Bodi mbalimbali na mbaya zaidi kutothamini maoni, michango ya Watendaji wakuu wa Mashirika, Taasisi na Wakala zilizo chini ya wizara yake. Kuwatishia kuwafukuza kazi na kukatisha mikataba ya viongozi hao – kikubwa anataka kukatiwa pesa kwenye kila miradi inayoendelea.

Baadhi yetu tunajiuliza, tabia za mtu huyu na mapungufu yake yameshalalamikiwa sana na hata uteuzi wake umekuwa wa kubebwa kulinganisha na uwezo wake lkn hakuna kinachofanyika. Wafanyakazi wa wizarani wamechoshwa na mtu huyo lkn kwa kuwa ni mtoto wa fundi haguswi na mambo yanaenda shanghala baghala yet nobody cares! Awamu ya pili ya JK baada ya kupangua wizara na kuigawa wizara ya Miundombinu kutenganisha Ujenzi na Uchukuzi, Bw. Chambo alipoona Bw. Magufuli na Mwakyembe, ambao ni wachapa kazi hodari wameteuliwa kuongoza wizara ya Ujenzi, kabla hata hajateuliwa alianza mwenyewe kiaina....alijing'atua na kujipeleka Uchukuzi kukimbia kasi ya Bw. Magufuli ambayo kwa namna yoyote ile kasi yake asingeiweza! Sasa bw. Chambo yupo Wizara ya Uchukuzi ambako kuna mawaziri pia very weak (Kuna Nundu na Mfutakamba). Huko anapumua na akiendelea na tabia zake za kuwavuruga watendaji wakuu.

Wengine sisi tunajiuliza watendaji mabomu kama akina Chambo kukalia wizara nyeti kama hizo na huku hakuna delivery yoyote, ni kwa namna gani JK atatekeleza ahadi alizotumwagia wakati wa kampeni???? Ahadi za kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa Sijuwi Bukoba, Kigoma chini ya akina Chambo zitawezekana? Ahadi za kununua meli mpya na vivuko zitawezekana wakati watu wanaangalia matumbo yao zaidi? Lini tutanzisha shirika letu imara la ndege huku akina Chambo wanawadharau wataalamu na maoni na mapendekezo yao?

Dr. Kitine alimlenga Eng. Chambo kama mmoja wa Makatibu wakuu bomu, fisadi na uteuzi wake umelalamikiwa sana. Kuthibitisha haya tafuteni watu wa wizara ya Miundombinu (sasa Ujenzi na nyngine Uchukuzi) mtapata data za Eng. Chambo ni nani? Halafu tunashangaa kwanini mambo hayaendi? Nchi tajiri kama Tanzania haina hata reli ya kujivunia, ndege yetu yenye kupeperusha bendera na nembo ya TZ iko wapi? Bandari za uhakika zitakazotuingiza ktk soko la ushindani la pamoja la A. Mashariki (East African Common Market) ziko wapi?

Ili nchi iendelee inahitaji ardhi, watu siasa safi na uongozi bora. Kwa wa-TZ vyote vipo isipokuwa Uongozi bora ni zero!

Mkuu nilikuwa nataka kuchangia kwenye thread hii lakini baada ya kusoma ulichoandika imebidi niache kwa kuwa ulichokisema ni kweli na kweli tupu. Umeingia deep kisawasawa mkuu. Big up
 
Kama ni mteule wa Rais.. atajihamisha vipi mwenyewe? mbona haijakaa vizuri hii?
Out of curiosity!

Imekaa hivi mkuu, baada ya wizara ya miundombinu kugawanywa kuwa Ujenzi na Uchukuzi ilibidi Watendaji na wafanyakazi wajigawe ili majukumu yaendelee. Wakati wakisubiri instrument toka juu, ilibidi Katibu Mkuu na naibu katibu Mkuu wagawane, mmoja abaki Ujenzi mwingine aende Uchukuzi. Hata wafanyakazi wengine walikwenda ujenzi na wengine Uchukuzi, ni utaratibu wa kawaida ili shughuli ziendelee. Bw. Chambo option yake wakati wanasubiri uteuzi alikimbilia Uchukuzi, naibu Katibu Mkuu akaenda Ujenzi. Kwa wanaomfahamu Chambo asingekwenda Ujenzi piga-ua maana huko ni moto na Bw. Magufuli. Hivyo Bwana Mkubwa alipofanya uteuzi wa Makatibu Wakuu wa wizara hizo, aliwathibitisha kama walivyojipanga. Chambo - Uchukuzi na Naibu wake Bw. Balozi Mrango akawa Katibu Mkuu. It is simple arithmentics ndg yangu!
 
Back
Top Bottom