Nimeshaanza kuwa na wasiwasi na uelewa wa hawa wasomi wetu ambao ndio tunaowategemea,ndugu umeeleza vizuri sana ,huyu Dr Kitila kaonyesha umbumbumbu wa hali ya juu,na nakubaliana na mdau kuwa kuingiza hilo kwenye mambo binafsi huo ni ufinyu wa akili,hasa kwa mtu msomi kama Kitila(?)nafikiri pia huyu Dr wakati alitaka tu kujionyesha kuwa anamjua Mbeki ndani nje na mwishowe kaharibu wakati ambao wengine wangetumia kuuliza maswali,unapomuuliza mtu kwa kurejea mambo yake binafsi ana haki ya kuhamaki ,na sawa hata yeye Kitila umuulize swali na kwa kufuata mambo yake binafsi tena yanayohisi kifo sijui kama angefurahi.Kwa mila mambo ya vifo yanayomhusu mlengwa hayaletwi kwenye mijadala,huo ni kukosa heshima na adabukitila alipaswa kujua kwamba Mbeki alivyosema ukimwi ni ugonjwa wa maskini alisema kwa muktadha gani.kwa mfano; wakati mtu anakemea uzembe wa madereva, anaweza kusema "ajali barabarani husababihwa na uzembe wa madereva" sasa hapa haina maana kwamba ni kila ajali itakayotokea itakuwa ni usembe wa dereva lakini kulingana na mazingira ya kauli;kauli inakuwa ni sahihi.Sasa mbeki alipo sema vile. alitaka kuonyesha kwamba umaskini una mchango mkubwa katika kuenea kwa ukimwi;kitu ambacho kina ukweli.
Mtoto gani wa Mbeki aliyekufa kwa UKIMWI?
*Kama Mkumbo ameuliza kweli suala kwa namna hiyo, ninaelewa kwa nini Mbeki amekataa kulijibu, kwa sababu limekaa kusuta zaidi ya kutaka ufafanuzi........Ila sidhani kuwa Mkumbo ameuliza suala hilo, hivyo lilivyo
"Mbeki aliacha kujibu hilo swali. 'I will not respond to that pinching question' alisema Mbeki."
Mbeki knows the answer. Issue yangu hapa ni kuwa viongozi wengi wamekuwa wakitoa kauli ambazo impact yake ni mbaya sana.
Sababu ya kushamiri ulimwi Botswana ni wafanyakazi wa kwenye migodi hawakupewa elimu ya kutosha na mila na desturi zao zilichangia sana
Chama
Gongo la mboto DSM
Hapo Kitila alichemsha. Report ya world bank iliyotaka mwaka huu inaonyesha kuwa kuna correlation kati ya kipato na ugonjwa wa UKIMWI.
Inawezekana hata huyu alotuletea hapa hii habari kachapia na watu tunamshabikia, tunaondoka na habari kana kwamba ni ukweli usio shaka
Na suala la msingi limelalia hapo kwenye mtoto wa Mbeki aliyekufa kwa UKIMWI.....
Kama hakuna huyo mtoto, hadithi yote hii tuliyoletewa hapa inaweza kuwa ni ya uongo mwanzo hadi mwisho wake
Mkuu,
In real sense, Kitilya alimuattack Mbeki personally, ambayo si nzuri. Mbeki ni binadamu mwenye nyama na damu. Pamoja na hayo siamini kama Kitilya anaweza zusha uongo mkubwa hivyo, kuna sehemu kasimama na ndo maana alitaka Mbeki aseme ukimwi unasababishwa na shida na umasikini tu? Its real a pinching question.
Tatizo langu lipo kwa viongozi ambao hawajui kuwa kila kauli inayotoka midomoni mwao inachukuliwa kwa uzito mkubwa sana sana tu!
Huyu jamaa ni muoga maswali kama Sultani Kikwete anavyo ogopa midahalo alikuwa radhi kumfukuza mchapakazi kama Tido kuliko kusikia neno mdahalo
kitila hapo kweli alikosa busara na alihuliza swali kama sifa flani hivi aonekane nae kahuliza swali ,pia hakukuwa na haja ya yeye kumtaja mtoto wa mbeki kwani ni masuala ya kifamilia...hekiama hana akili finyu huo udokta kapewa kwa njia za panya yaelekea....mgeni akija kwake anaweza kumuhuliza vitu kama hivyo?
SASA BOTSWANA NI NCHI TAJIRI?YAANI MFANO WANGU NILOTOA HAPO JUU HUJAUELEWA?Kwa hiyo wewe na kitila mnataka kutuambia ukimwi ni ugonjwa wa matajiri kuliko ilivo kwa masikini?Botswana ni nchi maskini? mbona ukimwi umeshamiri? Wacha kumshabikia Mbeki.
Mimi nna shaka kuwa hajauliza hili swali kama lilivyoanishwa hapa
Dk. Kitila Mkumbo tafadhali njoo utupe swali ulilouliza tulijadili.
#Mentiontagmgogoro
Acha chuki za kisiasa KongoziNaona huyo muuliza swali aliuliza tu kujionesha kwamba anafuatilia sana mambo ya Mbeki hakuwa na nia yeyote ya kupata clarification kwa faida ya wote.
Mhadhiri Mwandamizi wa UDSM, Dr. Kitila Mkumbo jana alimpa wakati mgumu Rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki.
Hiyo ilikuwa ni katika wakati wa maswali kwa Mbeki baada ya hotuba yake katika ukumbi wa Nkrumah wa UDSM.
Swali la Dr. Kitila lilijikita katika kauli ya Mbeki, wakati akiwa madarakani, kuwa UKIMWI hauenezwi na ngono ila shida na umaskini wa wananchi. Dr. Kitila alimkumbusha Mbeki juu ya kifo cha mtoto wake (wa Mbeki) kilichosababishwa na UKIMWI. 'Unaendelea kusimamia kauli yako?' aliuliza Dr.Kitila
Mbeki aliacha kujibu hilo swali. 'I will not respond to that pinching question' alisema Mbeki. Na hapo ndipo ukawa mwisho wa maswali kwa Mbeki ingawa swali la Dr.Kitila lilikuwa la pili tu.Prof. Mukandala alimaliza muda wa maswali ghafla
Mkuu umenikuna hapa!!Mbeki ni mchumi. Na alitazama vitu kutokana profession yake. Watu walimpinga sana aliposema maneno hayo. Sababu kubwa ya kumpinga huko ilitokana na kuwa science ya kutibu magonjwa iliyokuwa mstari wa mbele kwenye kampeni.
Mpaka sasa hakuna vaccine. Lakini matumizi ya pesa yameonyesha kuwa yanapunguza kwa kasi kubwa kusambaa kwa ugonjwa huu. Na unapozungumza pesa, uzungumzi umasikini.
Kwa mfano serikali ya Marekani ilitoa mapesa mengi kusaidia nchi za kiafrika kununua madawa (antiviral). Matumizi ya madawa haya yanapunguza usambazaji wa ugonjwa.
Kwa mtaji huu sio vaccine na wanasayansi wanaoweza kutatua tatizo hili pekee yao. Ni mchanganyiko wa mambo mengi, yakiwemo mambo ya kuinua uchumi.