Dr. Kitila ampa tabu Thabo Mbeki

Nadhani umuhimu wa swali hili ulikuwa ni kuhusu umuhimu wa viongozi kuwa makini na matamko yao kwani wakati mwingine yanaleta madhara kwa raia wao kwa kiwango kikubwa sana. Tamko hilo la Mbeki kuhusu ukimwi lilisababisha watu wengi wa Afrika ya kusini kufa kwa ukimwi bila kupata ARV ambazo nchi yao ilikuwa na uweo wa kuzipata.
 
Wakati mwingine chuki na kutokujua hutufanya kushindwa kuhukumu kwa haki;

Mwanzo ilikuwa Kitila ameuliza mtazamo wa Mbeki kuhusu maambukizi na kwamba mtoto wake alikufa kwa sababu ya ugonjwa huo.
Baadhi humu wakashikilia "habari ya mtoto wa Mbeki", kwamba Kitila amekurupuka Mbeki hana mtoto aliyekufa kwa ugonjwa huo.

Ilipoelezwa kwamba Kitila hakumzungumzia mtoto wa Mbeki, mada ikageuzwa ikawa "AIDS sio tishio kwa bara la Afrika na kwamba muulizaji hakupaswa kuuliza swali la aina hiyo!!" kwamba Afrika ina matatizo mengi na msomi huyo hapaswi kuuliza swali la aina hiyo!!

Sasa hivi mwelekeo utakuwa ni wa ukosoaji kwa Kitila kwenye muundo, lugha na ufundi wa kuuliza swali!!

Seriously tumesoma swali la Kitila kwa moyo safi na kulielewa?

 
Authority ni kwenye kasa na kobe sio kwenye Kiswahili cha kuwaelezea kasa na kobe.
Huwezi kuwa mamlaka "isiyokisia" ya kitu ambacho huwezi kukielezea, nyinyi ndio mamlaka za kibongo, mtu anakwambia mimi ni authority ya kasa na kobe lakini sijui jinsi ya kuwaelezea kasa na kobe! Sasa utaalam wako utasaidia vipi jamii kama huwezi kutuelezea unachokijua?

Na alichonacho kobe jee?
Umetuambia kwamba wote wana miguu/mikono/magome na magamba ila tofauti ni katika miundo yao, sasa utatuulizaje sisi tena kama Kobe ana mikono au nini? Hahahaaa.... (Gaijin: "Tofauti nyengine ni kwenye muundo wa magamba (magome?) na miguu (mikono?) yao.") Wewe ndio umetuambia wote wanayo, tena umeogelea nao na kuwapanda kasa na kobe! Ghafla umegeuka eti hujui Kiswahili cha mikono na miguu, khaa! Hujui Kiswahili kwani we wa wapi, Mnyarwanda?

Siku ingine kama hujui kuelezea kitu na unabahatishabahatisha kati ya miguu na magome na mikono na magamba basi usituambie "mimi huwa sikisii"! Tumia maelezo modest yanayoacha nafasi ya makosa ya kibinadamu pamoja na kukisia. Hujui Kiswahili? Ushindwe na ulegee!
 
Ngoja data mpya za Tanzania zitoke hivi karibuni, then nitakukumbusha. Halafu utaniambia, hiyo awareness ya vijarida vya WHO, UNICEF n.k. imekusaidia nini? Please watch this space!!

Mkuu vita dhidi ya ukimwi vinaanzia kwa mtu binafsi elimu ya ukimwi ipo nje nimekwambia acha kuokota mizoga utakuwa salama 99.9% njia kubwa ya maambukizo ya ukimwi ni ngono hilo nalo pia unataka kubisha?

Chama
Gongo la mboto DSM
 

Mkuu Kiranga
unakuja na hoja nyepesi sana suala la Mbeki lipo wazi tafiti zipo zilizothibitisha yote dawa za wakati ule zilikuwa ni toxic na upo utafiti ambao hata WHO walikiri idadi ya watu waliokuwa wakitumia dawa walikuwa wanakufa haraka kuliko wasiotumia SA imepiga hatua kwenye tafiti usifikri wao walikuwa wapumbavu; kama wao walikuwa wapumbavu mbona hata hapa USA wamebadili taratibu za matibabu? wanaanza na nutrition kabla hawajaanza kukupa ARVS? Yale yale walioyokuwa wabisha ndiyo wanayoyafanya sasa hivi kwa mantiki hiyo upo ukweli mkubwa; unajidhalilisha sana waafrika si wapumbavu kama unavyotaka kuamini; hata hapa USA waafrika wengi waliadhirika na ukimwi baada ya serikali kwa makusudi kutowaeleimsha kama waliyafanya hapa USA je huko Afrika walifanya managapi?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Last edited by a moderator:
Huwezi kuwa mamlaka "isiyokisia" ya kitu ambacho huwezi kukielezea, nyinyi ndio mamlaka za kibongo, mtu anakwambia mimi ni authority ya kasa na kobe lakini sijui jinsi ya kuwaelezea kasa na kobe!

Una matatizo ya ufahamu au ndio kujitia unjufu bila ya sababu?

Kwanza wapi niliposema sikisii kwenye kuwaelezea kasa na kobe?

Nimesema "Huwa sikisii" nikijibu shutuma kuwa nimekosea kwa kuweka picha ya kobe badala ya kasa. Key words: kuweka picha

Naelewa kuwa Kiswahili ni kigumu ila sikudhani kama mtu anaweza kushindwa kuelewa tofauti ya "sijui kuwaelezea kasa na kobe" na "sijui kipi ni Kiswahili muafaka cha kuelezea viungo vya kasa na kobe"



Umetuambia kwamba wote wana miguu/mikono/magome na magamba ila tofauti ni katika miundo yao, sasa utatuulizaje sisi tena kama Kobe ana mikono au nini?

Sijawaambia kitu hicho kamwe na kama nimewaambia zile alama za kuuliza zina kazi gani? Elewa tofauti ya kusema na kuuliza.



Hujui Kiswahili kwani we wa wapi, Mnyarwanda?

Wewe ndo unaonekana hujui Kiswahili sawa sawa mpaka kushindwa kuona mantiki ya mtu kuuliza kama kasa ana miguu, mikono au mapezi.



Siku ingine kama hujui kuelezea kitu na unabahatishabahatisha kati ya miguu na magome na mikono na magamba basi usituambie "mimi huwa sikisii"!

Inasikitisha kuwa mtu mzima na shughuli zake hawezi kusimamia hoja zake mpaka atunge na uongo, ikisha akosoe huo uongo alioutunga ili tu apate cha kukosolea mwengine.....SMH



Tumia maelezo ya staha yanayoacha nafasi ya makosa ya kibinadamu pamoja na kukisia.

Sawa nitajirekebisha
 

Mkuu Chama, nina mfano hai wa madawa hayo ambayo hayakuwa na ubora wowote, kuna jamaa yangu wa karibu tulikwenda kumununulia dawa hizo ambazo zilikuwa zinauzwa bei mbaya - laki nane kwa dozi!! Baada ya kuzitumia kwa muda kidogo afya yake ilibadirika ghafla 4 worst, haikuchukuwa muda akafariki dunia!!!

Mwanzo alikuwa anakataa kata kata kutumia dawa hizo, alipendelea kutumia dawa za kienyeji alipo kuwa Mwanza, kuja Dar tukamlazimisha atumie dawa hizo za kizungu, baada ya kushuhudia hali yake ya afya inabadirika kwa kasi ya ajabu tulijilahumu sana.

Mzee Mbeki alikuwa jasiri sana kuwasema wazungu bila simile na hii ilisaidia sana katika kuwarudisha kwenye mstari na kuacha kuwachukulia Wafrica 4 a ride, mambo aliyo kuwa anasisitiza ndio yana tekelezwa moja baada ya jingine - lakini waswahili wenzetu wamekalia kumbeza beza tu!

Tusisahau kwamba katika harakati za Mh.Mbeki za kuwapasha watu wa magharibi alikuwa anashirikiana na waziri wake wa afya mwanamke alikuwa na taaluma ya UDAKTARI yaani Dr.Manto Tshabalala-Msimang (mama huyo alisha fariki) but she was equally vocal kama MBEKI; mama huyo aliwahi kuishi Tanzania wakati wa vita vya ukombozi, alifanya kazi pale Muhimbili kama daktari.

Vyombo vya habari vya magharibi vilikuwa vinamzulia mambo chungu nzima mama wa watu, walifika hatua ya kusema eti ni mwizi aliwahi kushikwa akimwibia mgonjwa saa ya mkononi huko Botswana!! Hii inadhilisha kwamba kulikuwa na mipango kabambe ya kuwa-discredit Mzee Mbeki na Waziri wake wa Afya wa zamani.
 
Kwanza wapi niliposema sikisii kwenye kuwaelezea kasa na kobe?

Nimesema "Huwa sikisii"
Well, "huwa sikisii" is universally inclusive, inamaanisha wewe hukisii period! Ndio matatizo ya kutumia lugha za jumla jumla kama hizo. Ni wapi uliposema kutokukisia kwako ni katika kubandika picha tu? (Gaijin: "Huwa sikisii. I have swum with kasa and rode a kobe")... Umesema huwa sikisii, nukta! Kwa hiyo usiruke makosa ya matumizi yako mwenyewe ya maneno. Au mwenzetu huwa hukosei?

Sijawaambia kitu hicho kamwe na kama nimewaambia zile alama za kuuliza zina kazi gani? Elewa tofauti ya kusema na kuuliza.
Alama za kuuliza kazi yake ni kutuonyesha kwamba hujui kama ni mikono au miguu, au magamba au magome lakini wote wanayo, tofauti ni muundo wa hivyo viungo vyao. (Gaijin: "Tofauti nyengine ni kwenye muundo wa magamba (magome?) na miguu (mikono?) yao.") Notice hilo neno "yao." Ina maana unatuambia wote wanavyo viungo hivyo. lakini kama ulikuwa hujui bali unauliza swali tu, kwa nini ulianza na "Tofauti nyengine ni..." Kwa hiyo ulitaka kutufundisha kwamba wanayo tofauti nyingine lakini wewe mwenyewe ndio unatuuliza sisi swali tofauti yao ni nini? Haileti maana! hahahahaaaaa...

Wewe ndo unaonekana hujui Kiswahili sawa sawa mpaka kushindwa kuona mantiki ya mtu kuuliza kama kasa ana miguu, mikono au mapezi.
Si umekiri mwenyewe kwamba hujui kiswahili fasaha cha kuelezea miundo ya kobe na kasa, sasa unanishambulia mimi kwamba sijui Kiswahili tena? Umepoteza mamlaka ya kukosoa kiswahili cha wengine kama umeshakiri hujui Kiswahili cha kuelezea viungo vya kasa na kobe ilhali unasema umeogelea nao na kuwapanda. Halafu hata kama sijui kiswahili mimi sifungwi na matamshi kama ya "huwa sikisii" ambayo hayaachi nafasi ya kukosea kama mtu yeyote. Wewe ndio umejikuza kupita uwezo wako halisi wa kuelezea kasa na kobe!

tofauti ya "sijui kuwaelezea kasa na kobe" na "sijui kipi ni Kiswahili muafaka cha kuelezea viungo vya kasa na kobe"
that's trivial semantics, maana ni ile ile! Hujui kiswahili muafaka cha kuelezea viungo vya kasa na kobe lakini unaweza kuwaelezea kasa na kobe, kwa hiyo unaweza kuwaelezea kwa lugha gani muafaka, Kilingala? Haya waeleze Kilingala au lugha yeyote ile, au la kama hujui lugha muafaka yeyote ambayo unaweza kuwaelezea basi maana yake hujui kuwaelezea, nukta.

Inasikitisha kuwa mtu mzima na shughuli zake hawezi kusimamia hoja zake mpaka atunge na uongo, ikisha akosoe huo uongo alioutunga ili tu apate cha kukosolea mwengine.....SMH
Hapana, mie sitakuita muongo kamwe, sidhani kama ulikusudia kupotosha, bali ni saratani yetu kama jamii, ya kutokuwa makini na Kiswahili chetu, huwezi kutumia lugha za jumla jumla za "huwa sikisii" halafu sekunde mbili baadae unaanza kubahatishabahatisha na kukisia viungo vya wanyama ambao umejinadi umeogelea nao na umewapanda. Ukishajinadi hukisii na umeogelea nao na umewapanda huwezi kuja tena kutuuliza sisi kama wana miguu ama wana mikono ama wana magome!

Sawa nitajirekebisha
Hahahaaaaa.... such disciplined modesty is more Gaijin-esque than the vainglorious "huwa sikisii"! Reminded me of a most respected general of his generation succumbing to hunky punky indiscipline. In any event, it was penultimate fun picking the brains of one of the most illustrious person of letters on the board.

Alamsik.
 

Well said mkuu
 
si jambo zuri kumuuliza mtu mambo binafsi hasa yanayo husu misiba iliyompata kwenye mkutano wa hadhara halafu wa kisomi.

Just for An interpretation that removes obstacles to understanding
 

Bukyanagandi; Tatizo letu tumebweteka sana katika nyanja zote ndio maana kunafanywa wa majaribio. Serikali yetu haina hata vifaa bora vya kuchuguzia bidhaa zinazoingizwa nchini achilia mbali rushwa iliyopo. Hatuwezi kujitegemea kabisa. Dr. Kitila Mkumbo alitakiwa ajue kabisa kwamba SA kama nchi tajiri imeendela kwa sababu ya tafiti zinazojitegemea kama nchi na serikali inazitumia. Rais kama Mbeki ni moja ya maraisi ambao walikuwa wanafanya kazi kwa kupitia tafiti ndo maana alikuwa na ijasiri wa kusema hivyo.
 

Alipopotoka Mbeki, ni kukataa kuwa AIDS inasababishwa na HIV, na kukataa dawa.
Pamoja na kuwa immunodeficiency ina sababu nyingi km lishe duni, dawa i.e steroids, kansa ya damu (Leukemia), ila HIV ndo leading cause, na makali yake yanapunguzwa na ARV, ambazo Mbeki alizikataa!
 

Thanks 4 the info mkuu, sina shaka kwa taarifa hii wengi wetu tutafunguka macho na kuanza kumuona Mh. Mbeki in his true colour, kwamba hakuwa na nia mbaya. Watu wanacho sahau ni kwamba vyombo vya habari vya nchi za magharibi ni mahili sana katika nyanja za propaganda, watasema chochote kukidhi malengo/matakwa yao - Tusichukue habari RAW kutoka CNN, FOXNEWS, The Sun nk bila ya kuzi-digest vizuri kwanza.

Nataka nikili kwa mara ya kwanza kwamba upenda sana kusoma post zako na jinsi unavyo wajibu wenzako, nikisema you are gifted na a brilliant analytical mind sidhani kama ntakuwa nimekosea - honestly.

Nimalizie kwa kusema wana JF ni watafiti sana na weledi wa mambo mengi sana ya kusaidia katika ujenzi wa TAIFA letu, kama wangekuwa wanasikilizwa na kuchukuliwa seriously katika uchambuzi wao, mbona Taifa letu lingesonga mbele kwa kasi yakutia moyo - lakini hata hili la magazeti kuwa na courtsey ya kukili kwamba habari nyingine wanazi copy kutoka Jamii Forums siyo ya kupuuzia, we count a lot behind the scene I guess.
 

Dr. umeanza kuongea vyema ila ukaishia weka maelezo nunsu nusu kama Mbeki.hapo kwenye red .Unachokisema kimekuwepo kwa miaka kdhaa nchini , kimefanywa sana na waandishi na watangazaji km akina Juma Nkamia, na huyu ,jamaa yetu wa dkk 45.Ila hakun alaiyewahi warekebisha kwa hilo.Pia wewe ukiwa kama mwalimu sijui kama ktk darasa lako umekuwa ukiwakumbusha watu kuhus hilo.

Hata presidaa wetu anapenda sana longolongo kwa kurefusha maelezo na kuanza describe maneno anayotumia kw akiafi ch akupotosha au amplify vitu vidgo sana.Juzi nimesikia J makamba akiongelea security na auditing na watu walioandaa mkutano kama wanaandaa dinner tuu.Wameongea vitu dhaifu sana kuhusu hiyo security ila wame amplify kama vile wanchofanya ni kitu kikubwa sana ktk ukubwa wa tatizo.Kwa watanzania "what matters is not the size of fight on a dog but the size of dog."

Walikuwa wakiongelea security km vile issue ya migambo na police wetu huku mitaani na wanachokiita mitego.Wanaongelea auditing kama ndio security, hawaongelea kuhusu kukaza nuts and bolts, best practices, hawaongelei technologies na mitigation.Ni yale yale ya TBS kuangalia bidhaa iliyo tayari na kusema inafaa au haifai.Ila hawajui kuwa bidhaa iliyozalishwa nchini inahitaji kuangaliwa ubora tangu materials zikiandalia .Km ni za kilimo tangu ardhi inapoandalia hadi kuvunwa mazao kunachangia sana ubora wa bidhaa, na mara nyingine kunaweza ficha madhara yake haki pale inapotumika.

Dr. michezo ya kuigiza ndiyo imetufikisha hapa, na imechezwa sana pale UDSM, na watu hawajaafundishwa kuwa makini ktk mambo yao.Ndio maana watu wapo very shallow ktk mambo mengi.
 
 
Mkuu Nguruvi3
Napingana na kauli yako; hakuna mwenye kumfanyia personal attack Dr. Kitila hapa kinachojadiliwa je ilikuwa sahihi au sio sahihi kwa yeye kuuliza swali lile; nimepingana Dr. Kitila kwasababu ambazo zipo wazi na nazisimamia; mpaka sasa hivi si Dr. Kitila au wale wenye kumuunga hawajaweza kutoa kauli zenye ushawishi kuunga mkono hoja zao. Naamini wewe upo kwenye taaluma ya afya labda nikuulize kabla hujakuja jamvini kumtetea Dr. Kitila na kumtuhumu Raisi Mbeki umefanya kajiutafiti gani; hii habari si kuichulia juujuu. Mkuu Nguruvi3 naamini umepitia mahojiano na ya Mbeki na BBC; wengi mmejaribu kutia maneno ya sumu kwenye kinywa cha Mbeki; naamini nafsi zenu zinawasuta sana; ni aibu kubwa kuona waafrika tunavyokuwa na mawazo duni na wavivu wa kufikiria; Raisi gani angependa kuwaona raia wake wanakufa kama kuku? Mbeki angepata faraja gani hilo? Wanasayansi wa Afrika walichopigania wakati ule ndio kinachofanyika hivi sasa; je kama wao walikuwa si sahihi wakati ule kwanini iwe sahihi hivi sasa? Je ni nani alikuwa mkweli katika hili? Mkuu Nguruvi3 hapa USA kabla hujaanza kupatiwa matibabu VVU wanaangalia mambo mengi; kwanza wanafanya tathmini ya mgonjwa wanafanya blood work kuangalia kama una infections; Labs Liver function test (LT`s); Complete metabolic panel (CMP) hapo ni kuangalia je figo na ini zitakuwa na uwezo wa kuchuja na kutoa toxic ndani ya mwili; proteins, vitamins yote ni katika kuangalia mwili wa mgonjwa; kutegemea na lab results hapo ndipo wanapokupangia ule nini; haya yalionekana si sahihi wakati Mbeki anahoji lakini mkuu haya ndiyo yanayofanyika sasa hivi; mkuu labda umesahau kitu kimoja VVU havina uwezo wa kuua; kwa hapa wakiona kuna tatizo kwenye hizo major organs wanachofanya ni kukuweka kwenye reverse isolation huku waliendelea kutafuta dawa itakayokusaidia; mkuu walichotaka watu wakati ule ni kuuza dawa na haikuwa vinginevyo; walishikiniza Mbeki ananunue AZT hata kabla ya kuidhinishwa matumizi yake; mkuu najaribu kuileza hali halis kwa ufupi ili kila mtu apime mwenyewe; mkuu waafrika ni watu wenye akili na tuna uwezo kuchambua mambo si kila asemalo mzungu ni sahihi; wazungu siku zote ni ambao hawataki kuzidiwa hapa USA wapo waafrika hawajui kama ni mwafrika ndiye aliyechora ramani ya Washington DC; ni mwafrika ndiye aliyegundua namna ya kuweka trafic lights kuongoza magari; nenda kasome historia ya mti anaitwa Vivien Thomas itakuonyesha kumbe waafrika akili tunazo nyingi na wazungu wakiona mtu ni tishio kwao watatafuta kila njia kumpaka matope; swali alilouliza Dr. Kitila ni jepesi sana kwa mtu wa kaliba yake.

Chama
Gongo la mboto DSM
 

Mkuu chama,
Tatizo sisi tumejaa ushabiki, jambo akilifanya mtu ambaye unayempenda basi watu wanakuwa na upofu hawawezi hata kuhoji. Mkuu endelea kutoa elimu ya uraia na kuwafahamisha tatizo la HIV/IDS.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu chama,
Tatizo sisi tumejaa ushabiki, jambo akilifanya mtu ambaye unayempenda basi watu wanakuwa na upofu hawawezi hata kuhoji. Mkuu endelea kutoa elimu ya uraia na kuwafahamisha tatizo la HIV/IDS.

Mkuu Ritz
Ndiyo sababu tupo JF hapa tunaongea kweli hata kama inauuma; watu wanataka kupindisha hoja kwa mapenzi

Chama
Gongo la mboto DSM
 

Kuna tofauti kati ya AIDS and HIV. Nadhani hamjaelewa huyu mtu anauliza nini hasa. Kilichopo hapa ni msimamo wa huyu jamaa uliosababisha ARVs kuachwa kupelekwa South Africa. Kwa ufupi tu ebu angalia hizi definitions;

HIV-It is a virus that attacks the human immune system. Someone infected with the virus can live with HIV or be HIV positive for many years without becoming ill or showing symptoms. During this time however, HIV remains in the body damaging the immune system and the person remains infectious; able to spread the virus to others if a few simple precautions are not followed.

Being HIV-positive, or having HIV disease, is not the same as having AIDS. Many people are HIV-positive but don’t get sick for many years. As HIV disease continues, it slowly wears down the immune system. Viruses, parasites, fungi and bacteria that usually don’t cause any problems can make you very sick if your immune system is damaged. These are called “opportunistic infections.” The illness alters the immune system, making people much more vulnerable to infections and diseases. This susceptibility worsens as the disease progresses.
Over time, HIV can damage the immune system to such a degree that infections may begin to occur as a result of a weakened immune system. Eventually, one may acquire various illnesses due to the damage done by the virus. When this happens this is called AIDS or Acquired Immune Deficiency Syndrome. That is, a collection of illnesses.



Mkumbo anajua vizuri sana Area anayoongelea kwani second Degree yake amesoma HIV/AIDS kwa kiwango kikubwa. Anaelewa anachosema na kuuliza. Ila nadhani tusichukue neno mojamoja na kujenga hoja. Ndio maana muulizwa swali alihitaji reference zaidi ili aweze kujibu. Hivyo nasi tusitoe conclusion tu.Soma swali la Mkumbo between and within lines!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…