HKigwangalla
JF-Expert Member
- Feb 6, 2008
- 722
- 971
Brothers and Sisters,
Nawashukuru walioponda na waliofagilia, nyote mna haki ya kusema na kutazama mambo kama mnavyoona inafaa.
Haki mliyonayo nyie na mimi pia ninayo.
Naomba sasa niwaambie tu kuwa, kwa kutumia haki yangu, na nafasi niliyopewa na wananchi wa Nzega, ninafanya kazi yangu kwa nguvu zangu zote kwa kadri ninavyoona inafaa. Mnayo haki ya kuona vinginevyo, lakini nadhani wananzega wanajua zaidi kama kazi yangu inawalipa au la, na wataniambia wiki ijayo nikirudi nyumbani na kuongea nao. Nzega tumekuwa na kawaida ya kukaa kwenye vijiwe formal na informal na kuhojiana mustakabali wa maendeleo ya jimbo letu na nini wanachokitaka wananzega Mbunge wao akifanyie kazi. mengi ya mnayoyaona ninayafanya ni zao la mapendekezo yanayotokana na wananchi wa Nzega, kwa maandishi, kwa vikao, kwa sms na hata kwa email.
Naomba pia mfahamu tu kwamba, mimi kama mimi nafanya kazi yangu ya leo, ya 2015 anajua Mungu.
Siwezi kusema hapa leo kuwa mimi ni Mbunge bora kabisa kuliko wote, nafahamu wazi kabisa kuwa pengine mimi si mjinga kuliko wote, lakini najifunza kwa bidii sana kuwawakilisha wananchi wa Nzega na watanzania kwa ubora wanaostahiki na wanaoutarajia.
Hata hivyo, ninawashukuruni nyote kwa kunipa feedback. kwa wapenzi wa maandiko ya Hayati baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere, ni lazima viongozi wajikosoe na wakubali kukosolewa, na mimi ni muumini wa yote mawili, hivyo nawashukuruni kwa kunikosoa wale wote mlioniponda ....kama inavyosomeka kwenye kitabu cha 'Kujikosoa na Kukosoana'
Wakatabahu,
HK.