Huyu Dr. Kigangwala sio mtu mwema, chambo tu, amewekwa hapo kwa maslahi ya serikali.
Kama mnakumbuka wakati bajeti ya kilimo inapitishwa, aliwakera wabunge na wananchi wa kanda ya ziwa, bahada ya kuondoa shillingi na kuungwa mkono na wabunge wengi, kusema ukweli wananchi wengi walitegemea pale ndipo wabunge wao pa kuibania serikali ili itoe majibu yanayoeleweka kuhusu bei ya pamba.
Lakini alichofanya Dk Kigangwala, kama kawa akatoa shillingi, na akaungwa mkono na wabunge kibao, mpaka wakateua bahadhi ya wabunge wakakaa kikao kujadili hili swala.
Bahada ya hapo Waziri Mkuu akasimama kutetea bajeti ya wizara ya kilimo, Bahada ya hapo akaulizwa mtoa shillingi "vipi Dk bahada ya maelezo hayo ya waziri mkuu, bado unaendelea na msimamo wako wa kutoa shillingi"
Dk Kigangwala akacheka alafu akatamka "nairudisha shillingi yangu"
Tangu siku hiyo mpaka hivi leo wafanyabiashara wanajinunulia pamba kwa bei wanayoitaka, ma DC walikuwa wanawatetea wakulima wameacha, wanasema kama wabunge wenu wameshindwa kuwatetea, na ndio mliowapigia kura sembuse sisi.
Pale Dr Kigwangala alikuwa anawazingua wabunge ili wamuunge mkono alafu awatose, na ndivyo alivyofanya.
Nionavyo mimi ni kuwa, huyu ameandaliwa na serikali ili atoe shillingi watu wamuunge mkono alafu awatose, kama alivyowatosa wazee wa pamba, mpaka leo umeshasikia kelele za kwenye pamba. Serikali imetangaza bei 1100 na watu wananunua 600, hapo mpo?