Dr. Kafumu awa mwindaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Kafumu awa mwindaji

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mku, Oct 9, 2011.

 1. mku

  mku Member

  #1
  Oct 9, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  1. Dk kafumu akislaimia. Kushoto ni mkewe Maria Magdalena na kulia ni Nchemba.jpg

  Ndugu wanajamvini!

  Napenda kumfananinisha Dr. Kafumu na mwindaji aliyeenda kutafuta kitoweo na baada ya kupata kitoweo kalejea nyumbani. Zamani enzi zile za gari la moshi la kuchochea kwa kuni, na zile enzi za mashirika ya usafiri kama ya KIRETCO, AMTCO nakadharika kijana au baba mwenye mji ulikuwa ukitoka nyumbani asubuhi na mbwa wako kama sio kumi basi kumi na tano na mishale mikali yenye sumu kwenda kuwinda. Siku ikiwa njema na ukaja na swala nyumbani au kama sio pofu basi watu walikuwa wanasimama njiani wanakushangilia kama mwindaji hodari na wanakupa sifa kedekede. Sherehe ilikuwa inafanyika nyumbai kwako maana ndo hapo utakapolia nyama yako na nyama inaakuwa vizuri kama mnakula na watu wa nyumbani ukiwa unasimulia jinsi ilivyokuwa. Ni jambo liliwazi kuwa wana Igunga wamelamba dume maana kitendo cha CCM kumfanyia sherehe ya kumkaribisha na kumpongeza Kafumu dar ni kiashiria kuwa alienda kuwinda kura na kazipata na kaja kulia nyumbai kwake na ndugu na jamaa. Alienda kuwinda porini(Igunga) na karudi na nyama(Ubunge) kwenye bega nyumbani(Dar)..

  Hakuna mantiki ya kufanya sherehe na kutumia pesa mingi dar na huku wananchi waliokupa kura leo pale choma chankore hawana maji na wanalia na shida zao....Ila mwishowe huwa nawaza kuwa ngoja wakome maana hawataki kubadirika ila huwa siamini hili maana najua huwa wanalazimisha kwa njia moja au nyingine......Nawasilisha

   
 2. Mufiyakicheko

  Mufiyakicheko JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 893
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  Mkuu usiwaukumu wanaigunga ccm wenyewe wamesema hawakusitaili kushinda wamepenya kwenye tundu la shindano mazingila ya ushindi umeona wamebaka ushindi hujumarukuki zimefanyika kufanikisha ushindi wanaigunga tuwape moyo tupo pamoja kazi muliyoifanya nikubwa hongela wanaigunga
   
 3. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #3
  Oct 9, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Siyo kosa lao, kosa ni la yule aliyewanyima watanzania elimu.
   
 4. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #4
  Oct 9, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  tusiwalaumu wana Igunga jamani wao wamepigana na wameonyesha nia safi ya kutaka kuondokana na CCM lakini CCM wametumia kila wanalojua ili waendelee kubaki madarakani...
  Ngoja tuone hayo maendeleo yatakayoletwa na huyu Kafumu maana hizo pesa zilizotumika nio sawa na Posho ya Chama kwa miezi mitano. Sasa zitarudi vp???
   
 5. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #5
  Oct 9, 2011
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  CHADEMA wanaanza lini mikutano ya kuwashukuru wana igunga?
   
 6. COMPLICATOR2011

  COMPLICATOR2011 JF-Expert Member

  #6
  Oct 9, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 33
  Acha yawe hivyo hivyo hivyo labda mitanzania itajifunza. Aaagh!
   
 7. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #7
  Oct 9, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,970
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  Tatizo la Igunga linayakabili maeneo mengi ya Tanzania, hasa vijijin.
   
 8. g

  gkalunde Senior Member

  #8
  Oct 9, 2011
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 108
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WanaIgunga hawana namna ya kukwepa lawama hizi kwana wanaijua fika CCM tabia zake na kama wangekuwa hawawataki kweli ccm kwa namna yoyote ile wasinge ruhusu ccm kushinda mosi kwakuinyima kabisa kura lakini pili kudhibiti kabisa uchakachuaji matokeo na mwisho kuondoa kabisa amani kwa watakaotangaza matokeo ambayo wao hawakuyachagua yote haya uwezo walikuwa nao mimi kila siku huwa nasema kiongozi anaongoza kulingana na aina ya watu walivyo na wanavyotaka kuongozwa,hivi ndivyo watanzania wanavyotaka kuongozwa.
   
 9. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #9
  Oct 9, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wanajua kuwa wanaigunga bado wanamachungu kwahiyo hiyo sherehe isingefana kama ingefanyikia Igunga.
   
 10. A

  AMKA Member

  #10
  Oct 9, 2011
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mi sioni cha kuwashukuru wana igunga mana wamerudia tena kula matapishi kwa kuirudisha magamba madarakani igunga wametuongezea msumari wa maumivu tunayoendelea kupata watanzania kwa sababu tu ya kuwacha magamba waendelee kutuburuza. Mi najiuliza watz tutabadilika lini?? hii kulalamika haitoshi tufanyemabadiliko ya kweli tuache unafiki
   
 11. N

  Njopa Senior Member

  #11
  Oct 9, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Msiwalaumu wana Igunga Wamefanya kazi kubwa, Msiwalaumu watanzania! Wazambia hawana CCM NEC, CCM Police, CCM Usalama wa Taifa. Jamani tusitoke kwenye fikra sahihi. Unajua hawa mafisadi ccm wanatubana mpaka they suffocate our thinking ability its like what bob sang "They made the world so hard everyday we got to keep on fighting" x1 "They made the world so hard everyday the people are dying" Unajua wamayafanya mambo magumu mpaka bunge likafiri kuwa hatuwezi kuwa na umeme wa maji tena yote haya ni kibano cha mafisadi ccm. Jamani let us not swing but remain firm over the facts!!! its not the Igunga people nor Tanzania but CCM NEC, CCM Police, CCM Usalama wa Taifa, ccm TAKUKURU..............but never give up! we keep on fighting and we ll win the devil philosophy!!!!
   
 12. JIULIZE KWANZA

  JIULIZE KWANZA JF-Expert Member

  #12
  Oct 9, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 2,573
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nyerere au?


   
Loading...