Tatizo kule kwa waliotangulia wanaunda nchi moja ambayo itakuwa ni 'correction' ya hii hapa duniani, ndio maana vitu vizuri vyote wanataka wao.
1. Mzee akifikisha umri mkubwa, amejaa hekima na busara na uzoefu wa kutosha ambapo tungeweza kumtumia kutusaidia duniani, wanampunguza nguvu wanamchukua...wanatudanganya kazeeka kwa hiyo aondoke
2. Wachezaji mpira wote wazuri wako kwao, tukicheza nao leo matokeo ni wao 100 sisi 0.( wamewahi kuichukua KK 11 yote) wakatuachia kalusha tu.
3. Wanamuziki wote wazuri wanao wao. Hivi tungefanya Kili Awards na wale jamaa huyu 20% wetu angefua dafu kwa kina cool james mtoto wa dandu kweli? Kina Inspekta Esir? TX wamebeba, cheki Remmy wamepiga fitina mpaka wamembeba. Mbaraka Mwinshehe ndo walimuwahisha mapema, Issa Matona ndo kabisaa, Niko Zengekala je? Lwambo je? 2Pac je? Pepe kale? Bob Marley? Michael Jackson? Nasma Kadogo je? Halafu juzi tu hapa wamebeba bendi nzima ya 5 stars jamaniiii!!uuuuuuwiiiii!!!
4. Wamembeba Nyerere wakatuachia hawa jamaa zetu, Wanae Martin Luther King jr, Wanae JF Kennedy wakatuachia akina Bush wapenda vita, wakabeba Sokoine, Wakabeba Chacha Wangwe, Wamepora viongozi woote bora wakatuachia bora viongozi.....uwiiiiii
5. Newton wanaye wao, Kina Chachage wametupora, Kina Mwaikusa wametupora, Kina Harub Othman je......
Sasa tena na Katunzi, uwiiiiiiiiiii uwiiiiiiii hiiiiiiiiiiiiiiii Mnatuonea yaani kila kizuri mbebe nyieeee,
Nyie mnalo jambo nyie!!!! tumechoka kuonewaaaa,
Kwa nini mliotangulia mnataka mchukue wazuri wote kwani tunashindana jamaniiiiiiii MIE LEO NAANDAMANA MWENYEWE, NIMECHOKA UWIIIII MSINIFUTE MACHOZIIIIIIII WAMENINYANGANYA MWALIMU WANGU WA MENEJIMENTIIIIIIII RIPIIIIII RIPIIIIIII RIPIIIIIIIIII KATUNZIIIIIIIII DOKTAAAAAAA UWIIIIII