Leo Taifa letu limepoteza mwanazuoni mahiri wa shule ya Biashara ya Chuo kikuu cha Dar es salaam (UDBS).
Taarifa zinasema,kifo hicho kilitokea baada ya kuanguka ghafla na baadaye kupoteza maisha kabla hata ya kufikishwa Hospitali,tukio hilo limetokea wakati alipokuwa akifundisha wanafunzi wa MBA (2nd Year mwaka 2011) jioni ya leo.
Pole sana familia ya marehemu Dr Katunzi, wanajumuiya wa UDSM,wanafunzi wenzangu wa MBA,wanafunzi wote walihitimu Bcom kutoka UDSM kwa miaka aliyokuwepo mhadhiri huyu machachari na mcheshi sana!inauma sana.
Taifa litakumbuka mchango wako mkubwa katika Fani ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu,hakika tutakumbuka na kuyafanyia kazi yale yote uliyotuasa kwa manufaa ya Taifa letu Tanzania.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa,jina la Bwana libarikiwe!
Amina