Dr. John Pombe Magufuli & Morgan Tsvangirai Wahudhuria Uzinduzi Kampeni za ODM Kenya

Nasikitika kusema why don't we dig the contents than wasting time on theme!!!!!!
Ok, hata contents ni hovyo kabisa. This is personal between Raila and Magufuli. Anaichomekaje CCM kwenye huo mwaliko? Kama ungeihusu CCM, mwaliko ungetumwa kwa chama, na chama ndicho kingemteua Magufuli au mwakilishi mwingine yeyote. Kumbe hili jaluo halina tofauti na Lyatonga mukichwa.
 
huyu gamba nilimdharau alipoiba nyumba za serikali,alipopiga kampeni za kiwehu igunga,aliposema wakazi wa kigamboni tupige mbizi,aliposema safari za jk zinasababisha tupate barabara and on and on and on
he is irrelevant
 
Mh! Hapa protocol inakwendaje?! Nadhani mwaliko ungekwenda kwa Mwenyekiti au Katibu Mkuu wa CCM! Sasa kumwalika mwanachama wa kawaida hata akiwa waziri ni kuwaponda viongozi wake. JK na Kinana watajisikiaje?
 
Ok, hata contents ni hovyo kabisa. This is personal between Raila and Magufuli. Anaichomekaje CCM kwenye huo mwaliko? Kama ungeihusu CCM, mwaliko ungetumwa kwa chama, na chama ndicho kingemteua Magufuli au mwakilishi mwingine yeyote. Kumbe hili jaluo halina tofauti na Lyatonga mukichwa.
Hata mimi nashindwa kuelewa kwanza ni kwa nini Odinga ndio aandike Mwaliko huu na siyo Genaral Secretary, na Party Leader ndio cheo gani? usanii mtupu, lakini msisahau Odinga ndio mmiliki wa Uchumi Super Market pale kwa Manji. he is after his Interest.
 
Wana JF habari za uhakikia nilizozipata hivi punde ni kuwa Waziri wa Ujenzi kutoka Tanzania Mh Dr.John Magufuli na Waziri Mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai wamekaribishwa na Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga
kuhudhulia uzinduzi wa Kampeni uchaguzi mkuu wa Kenya utakaofanyika mwanzoni mwa mwaka 2013.Uzinduzi huo unaitwa " 2nd National Delegates Convention" 7th December 2012.

Ila kikubwa zaidi inasemekana Raila Odinga kawaalika hawa wawili tu ( Dr. Magufuli na Tsvangirai) na jana jioni walikaribishwa nyumbani kwa Odinga na kufanyiwa bonge la pati/mnuso wa kufa mtu.

Ili kijiridhisha na taarifa hii nimeweza kupata nakala ya mualiko wa Dr. John Magufuli. Nakala ya barua ya mwaliko na ajenda za uzinduzi zimeambatanishwa.

Mtizamo wangu ni kuwa Dr. Magufuli anakubalika hata nchi jirani ya Kenya ambapo rafiki yake mkubwa kisiasa Raila Odinga ktk kura za maoni anaongoza na huenda akashinda uchanguzi mkuu wa Kenya na ikampa nguvu Dr. Magufuli na mbio za uchaguzi mkuu ujao wa TZ.

Wana JF naomba kuwakilisha

NB: Nitatoa taarifa zaidi kadri nitakavyozipata!

...Magufuli na Tsvangirai watakuwa wameenda kuuza sura tu coz wakenya huwa hawataki kujua wewe ni nani na umefanya nini,wao wanataka kujua wewe ni kabila gani ili wakupigie kura ya ndio au hapana...
 
Nachojua mie ni kwamba John na Raila ni marafiki wa muda mrefu sana.. Na baadae wakawa mawaziri kwenye wizara zinazofanana tz na kenya.. wakazidisha uswahiba wao.. So kama Raila amemkaribisha John sababu kubwa itakuwa ni uswahiba na sio nafaci ya kisiasa..
 
Hawa jamaa ni mabest (John na Raila) kweli kweli, nakumbuka mwaka 2008 Raila alialikwa na Magufuli akaja hadi jimboni Chato, cha ajabu hakukuwa na kiongozi ye yote mkubwa kiserikali zaidi ya best wao mwingine Rais mstaafu Ben Mkapa, hivyo naamini Magufuli hakualikwa kama waziri wa ccm. Huyu mtaalam wa kemia ni mchapakazi kweli kweli ila tatizo yuko ktk kundi baya (magamba).
 
Deja vu, Namkubali Odinga kama Mzalendo wa kenya mwenye vision na Taifa lake, sio Magufuli yupo ktk Genge la Wahuni ni kweli kuna boom ya ujenzi wa road but kwa kasi ndogo sana sasa ni foleni zimezidi na usumbufu usio wa lazima kwa ujenzi wa barabara dar ulivyo haribika usimamizi ni mdogo wa utendaji kazi wa Magufuli
 
TNA kumewaka moto. Coalition for reform and democracy( CORD) inaimarika kila kukicha. Raila is headed for ikulu.
 
Kama nilivyo ahidi nitaupdate kinachoendelea, nimejulishwa mwenye access angali Citizen TV ya Kenya live mkutano wa ODM!
 
Huyo Magufuli hafai kabisa kuwa rais kwa kuwa ni mtu asiyeheshimu Katiba na Sheria za nchi kabisa. kwa kifupi ni dikteta.

Mfano halisi ni kuwa hadi sasa 2012 anatumia"ordinance" zilizorithiwa kutoka kwa wakoloni katika maamuzi yake mbali mbali ilihali hizo ordinances zilishapoteza uhalali toka Tanzania iwe nchi huru na kuwa Jamhuri kwa maana ya kuwa na bunge lenye mamlaka ya kutunga sheria.

Kutokana na ordinances kupoteza uhalali, 2002 Serikali ililazimika kutunga sheria ya mabadiliko ya sheria mbali mbali iliyoitwa "Revised Edition 2002" ambapo ordinance zote zilipitishwa na bunge kuwa sheria zinazoweza kutumia ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hii ilikuwa ni miaka 27 baada ya Serikali ya awamu ya kwanza chini ya Mwalimu Nyerere kuwahamisha wananchi kutoka katika ardhi zao na kuwalundika mabarabarani katika vijiji vya ujamaa chini ya "Operesheni Vijiji". Kwa kuwa wakati Serikali ya Nyerere inawahamishia wananchi mabarabarani ":Ordinance" zilishapoteza uhalali wa kutumika hapa nchini, wananchi wana haki kamili ya kumiliki aradhi waliyogawiwa kuhalali na Serikali hihi anayoitumikia Mhe John Magufuli.

Kutokea 2002 Mhe Magufuli amekuwa akitumia madaraka yake vinaya kuwabatiza wananachi waliohamishiwa mabarabarani na Setikali hii hii kuwa ni wavamizi wa hifadhi za barabara, kuwabomolea makazi yao na kwawekea nyumba za alama za X hali inayowaathiri kijamii, kisaokolojia na kiuchumi.

Katika kuwaathiri hawa wananchi kijamii, kisaikolojia na kiuchumi Mhe Magufuli amekuwa akiipuuza Sheria ya Ardhi ya Vijiji 1999 iliyotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1999 miaka mitatu kabal ya yeye kupata wadhifa wa uwaziri kwa mara ya kwanza. Katika kifugu na cha 15 Sheria hiyo inatamka kuwa “Ugawaji wa ardhi uliofanywa kwa mtu au kundi la watu waishio au waliotakiwa kuhamia na kuishi katika kijiji wakati wowote kati ya 01 Jan 1970 hadi 31 Des 1977 , kama ugawaji huo ulifanywa kwa mujibu wa sheria au kinyume cha sheria au bila kuzingatia sheria yoyote, sasa inathibitishwa kuwa ugawaji huo ni halali na kwamba daima ni wenye nguvu ya kutoa haki na wajibu wa kisheria kwa kundi la watu waliogawiwa ardhi hiyo....." Aidh kifungu cha 16 kinatamka .......... masharti ya kifungu 15 yatatumika kila mara ugawaji wa ardhi ya kijiji ulipofanywa na halmashauri ya kijiji au mamlaka nyingine yoyote mnamo na baada ya 01 jan 1978 hadi tarehe ya kuanza kutumika kwa sheria hii".

Katika kuthibitisha udikteta wake Mhe Magufuli ameendelea kutumia ordinance zilizorithiwa kutoka kwa wakoloni na kupoteza uhalali wa kutumika ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kudharau sheria kama hizi zilizotungwa na bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Katika kuthibitisha udikteta wake pia Mhe Magufuli anapuuza hata Sheria ya mpya barabara Namba 13 ya 2007 iliyotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama ilivyotafsiriwa na Barua ya Meneja wa Tanroad Mkoa wa Pwani ya tarehe 21 Okotoba 2010 yenye Kumb Namba TRD/CR/R.10/13/Vol.III/34 kwenda Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha (imeambatanishwa pamoja na sheria husika) inayotaja upana wa hifadhi ya barabara ya Morogoro kuwa Mita 60 toka katikati ya barabara kila upande na ikaelekeza namna ya kuzipima hizo Mita 60 kwa mujibu wa Sheria hiyo.

Badala yake Mhe Magufuli amemlazimisha Meneja mpya Tanroad Mkoa wa Pwani kubandika mabango kuwa Sheria hiyo mpya itasomwa pamoja na ordinance iliyopoteza uhalali wa kutumika ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa hifadhi ya barabara ni Mita 120 toka katikati ya barabara kila upande. Je huu sio udikteta?
 

Attachments

  • Tanroad Letter and Highway Act Regulation.pdf
    729.2 KB · Views: 108
Leo nimekuwa nafuatilia kupitia Qtv ya Kenya matangazo yao ya moja kwa moja nikaona watu mashuhuri waliofika ktk kuwaunga mkono ODM yupo Magufuri,Tsvangirai wa Zimbabwe,viongozi toka Uganda,Sudan kusini.Wote hao wameonekana kumuunga mkono Raila awe Raisi wa Jamhuri ya Kenya. Napenda mwana jukwaa yoyote anayejua uhusiano wa hawa viongozi wawili atujuze nasi angalau tujue.Kuna wakati Magufuri alifiwa Raila akaja kwenye mazishi kwa helkopta pale Mwanza.Pia mara kadhaa Magufuri amekuwa akienda Kenya kwa Enjinia Raila kumtembea. Tafadhali wanajukwaa karibuni tuelimishane.
 
Leo nimekuwa nafuatilia kupitia Qtv ya Kenya matangazo yao ya moja kwa moja nikaona watu mashuhuri waliofika ktk kuwaunga mkono ODM yupo Magufuri,Tsvangirai wa Zimbabwe,viongozi toka Uganda,Sudan kusini.Wote hao wameonekana kumuunga mkono Raila awe Raisi wa Jamhuri ya Kenya. Napenda mwana jukwaa yoyote anayejua uhusiano wa hawa viongozi wawili atujuze nasi angalau tujue.Kuna wakati Magufuri alifiwa Raila akaja kwenye mazishi kwa helkopta pale Mwanza.Pia mara kadhaa Magufuri amekuwa akienda Kenya kwa Enjinia Raila kumtembea. Tafadhali wanajukwaa karibuni tuelimishane.

Sasa mkuu unataka kujua uhusiano upi? ujue Magufuli ni binadamu kama binadamu mwingine, ana marafiki na ana maadui pia,ukiona hivyo ujue wale ni marafiki, au mkuu unapenda kusikia mambo ya udaku?
 
Mkuu mayeka simon ukweli ulio wazi sihitaji udaku wowote zaidi wanaowajua wawili hawa aidha mfano walisoma pamoja nakadhalika.Maadui au marafiki ni sehemu ya maisha yote unapoishi Duniani.
 
Back
Top Bottom