Dr. John Pombe Magufuli & Morgan Tsvangirai Wahudhuria Uzinduzi Kampeni za ODM Kenya

Mahebe

JF-Expert Member
Feb 7, 2009
319
63
Wana JF habari za uhakikia nilizozipata hivi punde ni kuwa Waziri wa Ujenzi kutoka Tanzania Mh Dr.John Magufuli na Waziri Mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai wamekaribishwa na Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga
kuhudhulia uzinduzi wa Kampeni uchaguzi mkuu wa Kenya utakaofanyika mwanzoni mwa mwaka 2013.Uzinduzi huo unaitwa " 2nd National Delegates Convention" 7th December 2012.

Ila kikubwa zaidi inasemekana Raila Odinga kawaalika hawa wawili tu ( Dr. Magufuli na Tsvangirai) na jana jioni walikaribishwa nyumbani kwa Odinga na kufanyiwa bonge la pati/mnuso wa kufa mtu.

Ili kijiridhisha na taarifa hii nimeweza kupata nakala ya mualiko wa Dr. John Magufuli. Nakala ya barua ya mwaliko na ajenda za uzinduzi zimeambatanishwa.

Mtizamo wangu ni kuwa Dr. Magufuli anakubalika hata nchi jirani ya Kenya ambapo rafiki yake mkubwa kisiasa Raila Odinga ktk kura za maoni anaongoza na huenda akashinda uchanguzi mkuu wa Kenya na ikampa nguvu Dr. Magufuli na mbio za uchaguzi mkuu ujao wa TZ.

Wana JF naomba kuwakilisha

NB: Nitatoa taarifa zaidi kadri nitakavyozipata!
 

Attachments

  • Letter addressed to Hon. Magufuli.jpg
    Letter addressed to Hon. Magufuli.jpg
    766.8 KB · Views: 4,939
  • Agenda - ODM NDC.pdf
    1.4 MB · Views: 456

Mjuni Lwambo

JF-Expert Member
Apr 25, 2012
7,347
5,219
Magufuri ndio yule jamaa aliyesema atakayeshindwa kulipia ongezeko la bei ya kivuko kule kigamboni apige mbizi?
 

Nyange

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
3,493
1,839
Watu tunapata shida kutoka majumbani kwenda sehemu za kazi, majamaa yameharibu barabara na ujenzi haueleweki na barabara zilizobomolewa ujenzi hauendelei. Mi namuona magufuri kama mtu asiye jua kupambanua mambo! nyie mnao muona wa maana nanyie mko kama yeye.
 

Precise Pangolin

JF-Expert Member
Jan 4, 2012
12,898
6,422
Watu tunapata shida kutoka majumbani kwenda sehemu za kazi, majamaa yameharibu barabara na ujenzi haueleweki na barabara zilizobomolewa ujenzi hauendelei. Mi namuona magufuri kama mtu asiye jua kupambanua mambo! nyie mnao muona wa maana nanyie mko kama yeye.
Mkuu nakuunga mkono asilimia mia moja huyu jamaa anatafuta sifa za kijinga sana yupo kama chizi ni mropokaji na muongo wa kutupa
 

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
44,160
50,566
Yani ma-lock amealikwa kama member wa ccm na sio kama waziri wa serikali ya tz....kwahyo ameenda kuiwakilisha ccm daaaaa hatareeee!!
 

Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
46,044
57,360
Moderators tunaomba muondoe hilo neno Breaking News tutaonekana wote hamnazo humu.
 

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
44,160
50,566
Watu tunapata shida kutoka majumbani kwenda sehemu za kazi, majamaa yameharibu barabara na ujenzi haueleweki na barabara zilizobomolewa ujenzi hauendelei. Mi namuona magufuri kama mtu asiye jua kupambanua mambo! nyie mnao muona wa maana nanyie mko kama yeye.

Magufuli amechemka sana na huu ujenzi wake wa kasi barabara nyingi zimearibiwa na hata hizo alternative roads walizojenga hazifai kabisa mbovu kweli......
 

DSN

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,837
1,667
Mwaliko wa PILI itakuwa ni ndani ya IKULU ya KENYA!!!! TIME WILL TELL.And now one will stop these!!!
True Friends-John & Raila !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom