Elections 2015 Dr. John Pombe Magufuli achaguliwa kuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM 2015

Upende usipende Lake Zone ndani ya MAGOGONI na sio MANVI wako tangulia kujiua ufe haraka kabla ya Boss wako hajafa maana afya yenyewe mbofumbofu

Kwa akili hizo hutakaa ujue hata jinsi siasa za nchi hii zinavyofanywa. Kwa akili yako unadhani kama sio Lowassa kuruhusu kambi yake na wajumbe waaminifu kwake toka kanda ya ziwa kujiunga kambi ya Magufuli angepenya?.Wala sidhani kama Magufuli alikuwa na kambi yoyote aliyowekeza na inayoeleweka. Ashukuru tu vita ya Lowassa na Membe,nduguye,dada yake na pia mwanao ndio iliyompa ulaji Magufuli na wala sio kutokea kwenye tano bora.
 
[/LIST]

Kwa sababu ya ujinga tu. Otherwise how else would you explain it? Watu wana maisha magumu, kero chungu nzima, na kila aina ya adha ambazo zimekua na kushamiri chini ya uongozi wa chama hicho hicho tokea tupate uhuru lakini hata siku moja hawafikirii kubadili walau na kujaribu huko kwingine kuona kuna nini.

Na CCM wameshalijua hilo [na wala hauhitaji kuwa genius kulibaini hilo] na wameshaugeuza huo ujinnga kuwa ndo mtaji wao wa kisiasa.

Inasikitisha sana kuona watu ambao unadhani labda wamefanikiwa kufuta ujinga kwa kiasi fulani wakiingia mkenge na kuhemka kisa tu eti Magufuli ndo atakuwa rais.

Kwamba kwa sababu huwa anatamka takwimu za madaraja na sijui mabarabara yale [ambazo hata huwa hazithibitishwi na yeyote yule kama zina ukweli au la] basi eti jamaa ni jembe, ni kichwa, na kila aina ya sifa za kipuuzi puuzi.

Na katika uchaguzi wowote ule ambao mwamuzi/ msimamizi wake ni makada wa CCM [tume ya uchaguzi] wapinzani wasahau kabisa kuiondoa CCM madarakani.

Kwa sababu nimeshashawishika kuamini kwamba njia pekee ya kuiondoa CCM madarakani ni kupitia maasi ya umma kama ilivyotokea kule Misri na Tunisia. Lakini najua kabisa hilo hapa kwetu ni ndoto za alinacha.

100% on point.

Yani watanzania tunahitaji some nature intervention to set us free of CCM, maana kwa kudra zetu wenyewe haitakuja kutokea.

Yani CCM wamekuwa kama gari bovu linalouzwa kwa bei mpya kila uchaguzi mkuu kwa kubadilisha dereva, huku akimwagiwa sifa kedekede. ghafla bin vuu watu wanasahau kabisa gari ni bovu na limepakwa rangi tu.na cha ajabuwakati linapakwa rangi wanalitazama.wapinzani wanatazama, badala ya kuwaambia watu gari mbovu hiyo wako bize kusema dereva huyu ana mashaka.CCM wanasema tumjaribu tuone, na sie tunaingia laini.

Viongozi wa Upinzani Tanzania, ni kati ya watu wanaonikera kuliko wote. Wana platform nzuri ya kuibana CCM,lakini miaka nenda rudi bize wanacheza santuri za CCM. sasa hata wao wameingia kwenye komedi za kushambulia chupa za CCm badala ya kushambulia mvinyo.Mvinyo ambao ladha yake kila mmoja wetu anaijua.

Niliwahi kuwashauri, kwa kuwa mvinyo wa upinzani haufahamiki,na chupa zao haziuziki, kwani hazirembwi kama za chama tawala, basi waanzishe utaratibu wa kuwa-onjesha wananchi huu mvinyo wao BURE. Ili wakinogewa na ladha wasisite kununua.

Lakini wao wako bize na kutaka kuuza wholesale chupa nzima bila kuonjesha, wakati wanajua hilo linahitaji nguvu kubwa zaidi.
 
Kimweri,

..siasa za tz ni ngumu kuliko nchi nyingine.

..kwa mfano hakuna labor unions ambazo zingeweza kuichallenge Ccm.

..pic haiwezekani kucheza siasa za kikabila nchi huku tanganyika. Numbers just don't add up. Kenya unaweza kuanzisha cha ma cha kikabila na within a year ukashinda uchaguzi.

..vilevile ccm imeweza kuzuia kumeguka na wanachama na viongozi wake kuanzisha chama kip ya.

..Kwamba Ccm haikumeguka imesababisha Vyama vya upinzani vianzishwe na watu ambao si wanasiasa au wanasiasa ambao wamechuja au wako past their prime. Kwa mfano Mtei, Makani, na wenzao walioasisi Cdm hawakuwa wanasiasa. Pita prof.lipumba wa cuf siyo mwanasiasa ndiyo mañana unaona uchaguzi mkuu ukiisha anarudi kwenye taaluma yake badala ya kujenga chama.

..kwasababu ya kukosekana kwa watu ambao wana WITO wa kweli wa siasa ktk vya upinzani kumepelekea vyama hivyo kudumaa kwa muda Mrefu.

..Cdm wamebahatika kwa na kiongozi kama Dr.Slaa ambaye ameweza kuchukua jukumu la kazi ngumu ya kujenga chama ktk mazingira magumu ya hapa nyumbani. Huyu mzee naweza kusema ni mmoja wa wanasiasa wa aina yake kupata kutokea tanzania. Kama huamini jiulize Kama kuna mwanasiasa yeyote yule wa rika lake angeweza kujenga chama kama alivyofanya Dr.Slaa.

..kuhusu uchaguzi wa mwaka huu ndiyo mara ya kwanza vyama vya upinzani vina nafasi ya kushinda.

JokaKuu, uliyoandika yana ukweli mkubwa, na mimi binafsi sina mashaka hata kidogo na dhamira ya Dr.Slaa. Siku zote i fault collecive fight they put. Yani Game ya Upinzani is simply too weak.

Tazama vitu vifuatavyo. Upinzani wamepewa majimbo,halmashauri kadhaa kwa muda wa miaka karibu 10 sasa. Hii wangeweza kuitumia kama roadshow ya kutangaza masoko ya mvinyo wao. Walitakiwa watuoneshe kwa vitendo utamu wa mvinyo wao, kwa kuwaonjesha watanzania ladha yake.

Wangeweza kulifanya hili kwa kuwa tofauti na CCM, kwa kuwa bora zaidi, lakini nasikitika kusema kuwa hawajatumia nafasi hii vizuri.ama kwa kutokujua au kwa kutokujiandaa vizuri.

Pili, wapinzani siku zote wanayajua mapungufu ya CCM, lakin ibadala ya wao kufanya bora kuliko CCM wanafanya kama CCM halafu wakikemewa na kina siye wanajitetea mbona CCM nao wanafanya?

Mfano mmoja mwepesi. Kuna tatizo kubwa sana la demokrasia na uwazi kwenye uendeshaji wa siasa za Tanzania. Kama umefuatili amchakato wa CCM, wakati pekee mambo yaliwekwa wazi ni wakati wa porojo. wakati wa maamuzi zinaletwa kauli za ,tunajifungia kushauriana.kwa lugha isiyo na chenga wanamaanisha tunajifungia kuzika demokrasia.

Tumeona pia wakati wa upigaji kura kuanzia CC,NEC hadi mkutano mkuu, Uhesabuji wa kura umekuwa wa siri,kwa maana ya kuwa watu kura wanapiga lakini wakati wa kuhesabiwa wanaenda kujificha,sasa hii inamaanisha nini?inamaanisa demokrasia tunayooneshwa ni ya maigizo tu.

Huu ulikuwa wakati muafaka na kabla ya hapo pia kwa UKAWA na vyama vinavyoshiriki kuonesha tofauti yao. Wafanye kila kitu kwa uwazi, kuanzia vikao vya kawaida hadi vikao vya maamuzi, ili watanzania waone ni jinsi gani maamuzi ya kuwaongoza yanavyofanyika. Na wakati wa kura, pia zihesabiwe kwa uwazi, live on TV, ili wananchi wajue ni jinsi gani KURA zinatakiwa kuhesabiwa hasa kwa uchache wa hii mikutano yao.

Huwezi leo hii ukaniambia eti kura 2,000 ni nyingi sana basi watu wakakeshe wanazihesabu. HUU NI UTAPELI. sasa cha ajabu UKAWA watarudia komedi hizihizi za CCM, watajifungia wakati wa vikao vya maamuzi, watajificha wakati wa kuhesabu kura. Halafu wakiibiwa kura uchaguzi mkuu wanalalamika. sasa unalalamikaje wakati hujawaonesha wananchi makosa ya CCM kwa vitendo?hujaonesha wananchi KURA Zihesabiwaje?

Mifano ya aina hii ni mingi sana, upinzani, ndio maana kila siku mimi huwakosoa. CCM is having it way too easy. Yani upinzani Tanzania ni shida tu za watanzania. SIO upinzani kwa maana ya vyama, siku shida zikiisha kuna vyama vitafunga ofisi zao.kwani hakuna mwenye maono ya mbele kukoje, wote wanasubiri kiongozi wa chama tawala aboronge ili waanzie hapo kujenga hoja.
 
Katika hali isiyotarajiwa, majina matatu yanawapasua vichwa vigogo Nani awe mgombea Mwenza, ambao ni Shamsi Vuai Nahodha, Hussain Mwinyi na Seif Khatib, huku spika Makinda akimpendekeza Amina ili kupata kura za Zanzibar. Karume hataki jina la Nahodha na Dr Shein anaomba Bilal aendelee ili kupunguza uzito wa kampeni Zanzibar.

Source : Mlinzi wa kiongozi mwandamizi.

Update zitakuja baada ya muafaka.
Huyo mlinzi amekosa weledi kama ni kweli
 
Hapana, umekosea.

Influence ya Lowassa iliishia nje ya vikao vya chama.

JK kamuweka mtu wake, aliyemuongezea ulinzi na kumpa right hand man mwezi mzima. wagombea wote wa-5 wa CCM jana walikuwa watuwa JK hand picked.

Poleni sana kwa kuchezewa shere na JK.

Hakuna fujo za team Lowassa ndio sababu ya kuibuka magufuli. Tuliokuwa ndani ya vikao ndio tunafahamu kilichotokea. Zilikuwa hesabu tu.
 
Tatizo la Watanzania ni usahalifu walio nao. Pia hawajali kuhusu wenyewe na nchi yao. Upepo kidogo tu wa kitu unawabadilisha mawazo mfano Magufuli ongea yake tu basi wameshamuona anafaa.
Ujinga wa wengi nao ni mtaji wa Watanzania kubadilishiwa mvinyo na kuwekwa chupa mpya.
Uoga wa mabadiliko kwa Watanzania nayo inachangia wakiambiwa tu labda wapinzani hawafai sijui vita vurugu basi wanaogopa.
Ukosefu wa uzalendo na kutokujali future ya nchi na vizazi vijavyo. Hadi wasomi nao wananunulika hadi watu wa kawaida kiurahisi.
Hii ya Magufuli haina tofauti na Jk 2005 watu walidaganyika kiurahisi, matokeo yake tumeyashuhudia.
 
Njia ya kuzuia huu ulaghai ni ku-disect hoja na kauli zinazotolewa kwa hoja na majibu yenye kufikirisha. Kama anasema akija yeye atafanya hivi, Upinzani unatakiwa useme kwa nini hatafanya.

Huwezi kusema utakuza demokrasia kwa mfano wakati umechaguliwa kupitia uchaguzi ambao kura zimehesabiwa kifichoni tena usiku kucha.kura 2,000.

Upinzani wanatakiwa waanze kujifunza ku-attack mapungufu ya CCM, na sio wagombea wa CCM. Upinzani unatakwa ku-perfect art ya kuonesha kuwa tatizo la CCM ni system nzima CCM iliyopo, inayozuia wachaguliwa kupitia CCM kufanya mambo bora tofauti na System.

Hii focus ya individuals, sijui flani fisadi, sijui flani ana kashfa, ndio maana kila uchaguzi Upinzani unarudi back to square 1 kwa kuwa CCM wamebadili mgombea.

Kwa mfano, kama hoja ya Upinzani ilikuwa JK dhaifu, ndio imesha-expaya tena, kwa kuwa kaingi amagufuli mtumia mabavu. ukiitumia hoja ya mabavu kwa miaka 10, magufuli akitoka wanamleta mpole, unarudi tena upya. hivyo inakuwa mambo ya kujaza maji kwenye pakacha.

Lakini System ya CCM ni ile ile, na ina mapungufu makubwa mno, lakini hakuna anayehangaika kuyaweka hadharani.

Mbaya zaidi, wapinzani nao wanakopi system hii mbovu na ya hovyo ya CCM,hivyo kujifunga hata kuikemea inapoboronga.
 
Tatizo la Watanzania ni usahalifu walio nao. Pia hawajali kuhusu wenyewe na nchi yao. Upepo kidogo tu wa kitu unawabadilisha mawazo mfano Magufuli ongea yake tu basi wameshamuona anafaa.
Ujinga wa wengi nao ni mtaji wa Watanzania kubadilishiwa mvinyo na kuwekwa chupa mpya.
Uoga wa mabadiliko kwa Watanzania nayo inachangia wakiambiwa tu labda wapinzani hawafai sijui vita vurugu basi wanaogopa.
Ukosefu wa uzalendo na kutokujali future ya nchi na vizazi vijavyo. Hadi wasomi nao wananunulika hadi watu wa kawaida kiurahisi.
Hii ya Magufuli haina tofauti na Jk 2005 watu walidaganyika kiurahisi, matokeo yake tumeyashuhudia.

Yaani kuna Watanzania wananisikitisha sana.

Adui ujinga bado kabisa hatujamshinda na CCM wanamtumia vyema sana huyo adui kwa manufaa yao.

Eniwei, nisiseme sana....yangu macho.
 
Kimweri,

..siasa za tz ni ngumu kuliko nchi nyingine.

..kwa mfano hakuna labor unions ambazo zingeweza kuichallenge Ccm.

..pic haiwezekani kucheza siasa za kikabila nchi huku tanganyika. Numbers just don't add up. Kenya unaweza kuanzisha cha ma cha kikabila na within a year ukashinda uchaguzi.

..vilevile ccm imeweza kuzuia kumeguka na wanachama na viongozi wake kuanzisha chama kip ya.

..Kwamba Ccm haikumeguka imesababisha Vyama vya upinzani vianzishwe na watu ambao si wanasiasa au wanasiasa ambao wamechuja au wako past their prime. Kwa mfano Mtei, Makani, na wenzao walioasisi Cdm hawakuwa wanasiasa. Pita prof.lipumba wa cuf siyo mwanasiasa ndiyo mañana unaona uchaguzi mkuu ukiisha anarudi kwenye taaluma yake badala ya kujenga chama.

..kwasababu ya kukosekana kwa watu ambao wana WITO wa kweli wa siasa ktk vya upinzani kumepelekea vyama hivyo kudumaa kwa muda Mrefu.

..Cdm wamebahatika kwa na kiongozi kama Dr.Slaa ambaye ameweza kuchukua jukumu la kazi ngumu ya kujenga chama ktk mazingira magumu ya hapa nyumbani. Huyu mzee naweza kusema ni mmoja wa wanasiasa wa aina yake kupata kutokea tanzania. Kama huamini jiulize Kama kuna mwanasiasa yeyote yule wa rika lake angeweza kujenga chama kama alivyofanya Dr.Slaa.

..kuhusu uchaguzi wa mwaka huu ndiyo mara ya kwanza vyama vya upinzani vina nafasi ya kushinda.

Aminaa.
 
Last edited by a moderator:
Kimweri nakubaliana na wewe hasa hapo kwa wapinzani inabidi wabadilike na Ku change approach yao. Mana ka ni matatizo Watanzania wanayajua sana wanataka mtu wa kuyatatua na sio blah blah.
Hasa hlo la Ku attack mapungufu ya CCM sababu system nzima yao ni mbovu na ni corrupted hakuna mwenye unafuu, na tatizo la CCM sio mtu mchapakazi au bora ni system yao mbovu ambayo imekita mizizi iliyojizatiti na kwa kulinda masilahi yao by any means. Na kwa Ku employ new methods ili waendelee kutawala. Upinzani inabidi wawe makini na kuja na mbinu mpya zaidi ya mapambano. Hivi hivi ni ngumu sana tu.
Tena hoja ya ufisadi nadhani sasa imechuja kwa wananchi, watuambie mambo mapya bila hvo mchezo utakua ule ule tu siku zote.
Hata tume ya uchaguzi isipo kuwa huru wapinzani watakua wanapoteza mda, wasitegemee jipya ka system nzima inaendeshwa na watawala hata kama ikitokea wameshinda hawawezi kutangazwa washindi, under system hyo hyo.
Wawe creative waje na new strategy.
 
Last edited by a moderator:
Yaani kuna Watanzania wananisikitisha sana.

Adui ujinga bado kabisa hatujamshinda na CCM wanamtumia vyema sana huyo adui kwa manufaa yao.

Eniwei, nisiseme sana....yangu macho.
Zaidi ya kusikitisha sana tu ujinga ni tatizo linalokwamisha maendeleo ya hili taifa. Na ukitaka kuwatawala watu kiurahisi basi wanyime elimu iliyo bora, na tatizo lingine ubinafsi mtu akipata anajifikiria mwenyewe.
Kuna na wasomi wanajua hali halisi lakini nao wamejitoa ufahamu kisa masilahi.
Tunahitaji ukombozi wa kifikra na tukubali mabadiliko ya kweli.
 
Njia ya kuzuia huu ulaghai ni ku-disect hoja na kauli zinazotolewa kwa hoja na majibu yenye kufikirisha. Kama anasema akija yeye atafanya hivi, Upinzani unatakiwa useme kwa nini hatafanya.

Lakini Kimweri, sawa, nakubali kwamba wapinzani nao wana mapungufu yao. Lakini pia let's cut them some slack. They are not competing on a level-playing field. The odds are overwhelmingly stacked against them.

I mean, it's joke that the members of the election committee [at least the top brass as far as I know] are selected by the president who is a chairman of the ruling party. Who do you think they will be beholden to? No-brainer! They will beholden to whoever hooked them up. It's a big 'ol joke that ain't even funny.

Huwezi kusema utakuza demokrasia kwa mfano wakati umechaguliwa kupitia uchaguzi ambao kura zimehesabiwa kifichoni tena usiku kucha.kura 2,000.

Halafu, kabla hata ya hao tatu bora....wale wengine 35 walikatwa katwaje? Walipigiwa kura? Huo mchakato wa kuwaengua ulikuwa huru, wa haki, na uwazi kiasi gani?

Au walienguliwa tu at the whims of the powers that be? It still boggles my mind how J. Makamba and Amina Salum Ali made it to the top 5 and Mark Mwandosya and Augustine Mahiga didn't.

How did that happen?

Upinzani wanatakiwa waanze kujifunza ku-attack mapungufu ya CCM, na sio wagombea wa CCM. Upinzani unatakwa ku-perfect art ya kuonesha kuwa tatizo la CCM ni system nzima CCM iliyopo, inayozuia wachaguliwa kupitia CCM kufanya mambo bora tofauti na System.

Huo ni ushauri mzuri ila huoni kwamba hata wakifanya hivyo kelele zao zita fall on deaf ears kutokana na ujinga wa masses?
 
Lakini Kimweri, sawa, nakubali kwamba wapinzani nao wana mapungufu yao. Lakini pia let's cut them some slack. They are not competing on a level-playing field. The odds are overwhelmingly stacked against them.

I mean, it's joke that the members of the election committee [at least the top brass as far as I know] are selected by the president who is a chairman of the ruling party. Who do you think they will be beholden to? No-brainer! They will beholden to whoever hooked them up. It's a big 'ol joke that ain't even funny.

This i agree, wapinzani hawako kwenye level playing field,which means they should work ten times harder. I work around privileged white chaps, and as a colored person, i usually have to work 3 times harder to get half the recognition, i don't blame them, i simply just work harder.

Hapo kwenye Tume ndio hasa nia ya mie kusema, waoneshe mfano. Maana huwezi kusema CCM wanapendelewa, wananchi wakakuelewa ,akama upinzani kwenyewe kuna manung'uniko. Inabidi wajitoe uchizi, na kuachana na hii michujo ya ki-ccm ccm, wamejitokeza watu 50, wote wapewe nafasi sawa, wasikilizwe sawa, wapigiwe kura kwa uwazi. Kama mtu anatuhumiwa kama njia ya kumuengua tuhuma zithibitishwe mara moja kwa ushahidi ulio public ili wananchi wajue.

In my opinion, this could have been a powerfull stratergy to teach watanzania vichwa vizito ni jinsi gani uwazi unatakiwa kuwa.

Sasa nikisikiaga kuwa UKAWA wanajadiliana nani sijui awe mgombea behind closed doors hapo ndio nachoka kabisa.

Upinzani have a dear task to fight CCM, but waache kujiongezea kazi.

Halafu, kabla hata ya hao tatu bora....wale wengine 35 walikatwa katwaje? Walipigiwa kura? Huo mchakato wa kuwaengua ulikuwa huru, wa haki, na uwazi kiasi gani?

Au walienguliwa tu at the whims of the powers that be? It still boggles my mind how J. Makamba and Amina Salum Ali made it to the top 5 and Mark Mwandosya and Augustine Mahiga didn't.

How did that happen?
Ndio komedi zenyewe. Kinachonikera kuhusu CCM ni kuwa wote wanageuka kuwa a bunch of corrupt group as long as wakiahidiana vyeo.watch this space, asilimia 80 ya waliokatwa utawakuta kwenye serikali ijayo. hawa hawa tulioambiwa wachafu hawafai, wametoa rushwa, hawajakomaa etc etc. Vigezo vya CCM kesho unasikia wameteuliwa. Kina chenge CC nzima iliwaita magamba, kesho yake wakawaaamini waandike katiba. Lowassa katukanwa na kila mwana CCM kuwa naagawa rushwa apate uongozi, leo hii wanamuweka High table,halafu anaitwa mchapakazi wakati raisi akifunga bunge na anashukuriwa kwa kazi nzuri.

Uchaguzi wa CCM,yalikuwa maigizo,zile komedi za kutafuta wadhamini ni kampeni zilianza kwa kuwa wadhamini walitafutwa na makatibu wa CCM wa sehemu husika kwa kila mgombea, so inshort CCM ilituma makada wake 40 kuzunguka nchi nzima kupata publicity.

January hawezi kupitishwa mbele ya mtu kama jaji ramadhani au Mahiga sehemu yoyote ile duniani, unless kigezo kilikuwa kimoja tu, umri mdogo.Huwezi ukatengeneza list ya wanasayansi mahiri duniani, halafu list yako ukamuweka mwanafunzi wa chuo kikuu halafu ukamweka pembeni mtu kama Einstein au Newton, list inakosa maana,kama haijabadilishwa jina.

Huo ni ushauri mzuri ila huoni kwamba hata wakifanya hivyo kelele zao zita fall on deaf ears kutokana na ujinga wa masses?

True, but angalau mapungufu ya CCM na serikali yataendelea kubakia consistent baada ya kila uchaguzi.kwa mfano, kama CCM ina utaratibu wa hovyo wa kupata kiongozi, utaendelea kubakia hivyo, unless waubadilishe, which is going to be a win-win for all.

Tunataka Tanzania ili yo bora, sio hii make-believe ya CCM kila baada ya miaka 5 kuwa all is merry, halafu wakitoka hapo hotuba ya kwanza tu bungeni wanaanza kuorodhesha matatizo mengi kuliko ahadi zao.
 
Kingine kinachonitatiza kuhusu upinzani ni ukosekanaji wao wa mbinu za kutengeneza leadership base kwa dhati kabisa.badala ya kuwaza mbele, kuwazamiaka 20 mbele, vyama vingi vinawaza leo na kesho. CCM hapa wanawashinda sana, ni pa kupaangalia. Hakikisheni mna-suffocate CCM out of the best brains, this way you have the best strategies.
JokaKuu
 
Last edited by a moderator:
Ninaona shamrashamra za wapenzi wa chama chama pinduzi wakishangilia kumpata mgombea wa uraisi bila kulinganisha sifa na uwezo wa Magufuli katika nafasi ya uraisi.

Hii ninaina ni ya kishabiki zaidi ya uhalisia kama vile kila bibi Arusi hushangiliwa kuwa "anameremeta", hata kama amekaa kama jioni. Hii ni sawa na vile wanaccm wengi wanamhurumia lowasa eti katumia muda wake mwingi, na fedha zake, afadhali ccm wangempa ili kumsaidia asipate hasara, eti wamjaribishe pengine angefanya kitu!. Ninaona haya mawili yakifanana kwamba watu hawajui raisi wa nchi ni nani na anatakiwa awe mtu wa namna gani au bado ni majuha kiasi cha kutokuwa na ufahamu wa maana halisi ya kuwa na raisi na umuhimu wake. Kwa mantiki hiyo, nafasi ya raisi imechukuliwa kama ushereheshaji kwenye harusi ambapo yeyote akiitwa bibi Arusi, basi anameremeta au mtu anapokuwa basi alazwe pema sijui wapi wapi.

Magufuli ni mtendaji mzuri kwa kuwa ni mfuatiliaji na anaelewa umuhimu wa viwango japo mara nyingi katika kazi zake pamoja na kuonyesha uchapakazi, ameshindwa kufikia viwango sahihi. Kwa hapo alitakiwa awe na team ya watu wenye uelewa kama wake ambao kwa pamoja wangefanya kazi kwa malengo na viwango na vipaumbele vimoja. Lakini kwa uongozi wa Magufuli katika wizara zake zote, hajawahi kuunda team ya namna hiyo na hivyo kila alilotaka kulisimamia likaonekana ni la kwake na wala si la wote. Na kila alikoondoka, aliyojaribu kuyaasisi yalikufa. Huyo ni Magufuli na CCM yake.

Raisi anahitajika kuwa zaidi sana ya hulka na sifa za Magufuli. Ninaungana na Prof. Baregu japo alimung'unya lakini alionyesha sana kwamba Magufuli siyo candidate sahihi kwa Uraisi kwa kuwa uraisi ni zaidi ya utendaji na ufuatiliaji. Magufuli ni mtendaji mzuri na angefaa kuwa waziri Mkuu ili awe chini ya mtu mwingine anayeweza uongozi ili asimamie utendaji wa serikali lakini hafai kuwa juu ya hapo kwa hulka zake. Kwa kumpendekeza Magufuli awe raisi ni sawa na kumpa shehe kazi ya ku communisha watu kanisani kitu ambacho hawezi kukifanya na hata akijaribu lazima ibada iwe mtafaruku!.

Kwa mantiki hii, magufuli atawafaa ccm katika kufufua chama chao maana wamemwona anafaa kule lakini sisi Watanzania tunahitaji kiongozi wa taifa. Atakayeongoza nchi kwa kujenga mifumo imara yenye ufanisi katika maendeleo ya taifa siyo hii ya ccm iliyoshindwa siku zote. Kumpendekeza Magufuli kuwa raisi wa nchi ni zaidi ya udhihirisho wa uchovu na kushindwa kwa ccm ambapo kwa muda mrefu sasa imekuwa ikiteua watu kwa kubahatisha na kujuana. Sote tunajua Magufuli ni matokeo ya hadaa na kukomoana ndani ya ccm ambapo hatutakubali ya spill over hadi kwenye taifa. Huyo Magufuli ni raisi wa ccm na atabaki ccm lakini kwenye Serikali ya Tanzania, hatakuwa.

CCM kaeni kando mjipange upya. Tanzania hatutaki purukushani zenu!.
 
Back
Top Bottom