Dr Hamis Kigwangala ahoji tatizo la ajira nchini

Dr Hamis Kigwangala ahoji tatizo la ajira nchini

Naibu waziri aingii kwenye baraza la mawaziri,angekuwa anaingia angetuchamba mitandaoni watafuta ajira mpaka tukome
 
juzi alikuwepo kwenye kikao cha baraza la mawaziri alishindwaje kuanzisha hiyo hoja huko ndani.

JWTZ ianzishe mashamba ya kisasa ya umwagiliaji kila mkoa - hapo tayari tutakuwa tumezlisha ajira kadhaa.
NSSF, PPF wanunue meli za uvuvi wa samaki deep sea, waanzishe viwanda vya samaki -AJIRA HAPO TAYARI.
NAFCO ifufuliwe, mifugo iko mingi sana Tanzania, waanzishe kiwanda kikubwa cha maziwa - AJIRA TAYARI HAPO.
JESHI La polisi liko nyuma kiteknolojia, liajiri vijana wasomi wabuni mifumo ya kisasa - AJIRA TAYARI HAPO.
Serikali ianzishe migodi 3 chini ya AGENCY itakayojitegemea (iachane na mishahara ya TGS) - AJIRA TAYARI HAPO.
General tyre ifufuliwe, matairi ya mtumba yapigwe marufuku - AJIRA TAYARI HAPO.
Serikali itafute masoko ya mazao nje, ihimize kilimo cha biashara kwa watanzania, tuna ardhi kubwa sana yenye rutuba,inunue madege ya mizigo yale ya kirusi tusafilishe mazao yetu kila asubuhi -AJIRA TAYARI HAPO.
Serikali inunue meli tano za mizigo, zianzie safari Tanzania kwenda kokote kule - AJIRA TAYARI HAPO.
nk nk nk nk nk nk nk nk k nk nk nk nk nk nk nk nk nk nk nk nk nk nk nk nk nk nk nk nk nk nk nk.

TUNASOMA KUTATUA MATATIZO, HATUSOMI KUONGEZA MATATIZO.. VIONGOZI WETU WASOMI MNATAKIWA MTATUE MATATIZO NDIO MAANA YA KUWA VIONGOZI. HAYO HAPO JUU NA MENGINE MEEEENGI MKITUMIA AKILI YANATOSHA KABISA KUMALIZA TATIZO LA AJIRA TANZANIA NA KUINGIZA KIPATO KIKUBWA KWA NCHI AMBACHO KITAIFANYA TANZANIA KUWA TAIFA LENYE MAGUVU..
 
Kwani kwenye baraza lao hawayaongei haya
 
Anayo namba ya Kairuki kwanini asimpigie? Anayo namba ya maneja wa TRA kwanini asimuulize? Wananchi wa kawaida ndio watampa majibu?
 
Kwa kweli Kigwangalla wewe ni mmoja wa mawaziri wapumbavu kabisa! Unashangaa nini hapo? Kwani hujui tatizo la ajira nchini?
Pengine ulitakiwa kumuuliza Kairuki kwanza kabla ya kukimbilia kwenye mitandao...
Ajira za TRA ni 4000 na walio itwa usaili wa awali ni 29 ,000.
Usaili unafanyika kwa kanda na hapo Kigamboni wameeda wenye makazi Dar na Pwani....
Kigwangalla punguza kukimbilia kwenye mitandao.....
 
Kuongoza Serikali si sawa na kuongoza jahazi
 
Hahaha kilo sita imekutosha sio

Sent using Jamii Forums mobile app
Nishanunua kiwanja na nimejenga room 2 na sebule. Soon nitahamia tatizo vijana mnapenda starehe mnafikiri mkimaliza chuo kuna mahali pa kwenda kuchota pesa au Kazi za millions of money. Wake your asses up hiko kidogo unachopata kitumie kwa akili kikuvushe sehemu Moja kwenda nyingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kweli Kigwangalla wewe ni mmoja wa mawaziri wapumbavu kabisa! Unashangaa nini hapo? Kwani hujui tatizo la ajira nchini?
Pengine ulitakiwa kumuuliza Kairuki kwanza kabla ya kukimbilia kwenye mitandao...
Ajira za TRA ni 4000 na walio itwa usaili wa awali ni 29 ,000.
Usaili unafanyika kwa kanda na hapo Kigamboni wameeda wenye makazi Dar na Pwani....
Kigwangalla punguza kukimbilia kwenye mitandao.....
Mkuu nakumbuka Kama walitangaza ajira 400 na wala si 4000; au nazeeka?
 
Nishanunua kiwanja na nimejenga room 2 na sebule. Soon nitahamia tatizo vijana mnapenda starehe mnafikiri mkimaliza chuo kuna mahali pa kwenda kuchota pesa au Kazi za millions of money. Wake your asses up hiko kidogo unachopata kitumie kwa akili kikuvushe sehemu Moja kwenda nyingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
Upo sawa kabisa kaka. ..niliuliza tu though

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magufuli kwake ajira anaona siyo TATIZO Kabisa, ili mradi yeye na wanaomzunguka wanaenjoy KEKI YA TAIFA, Wenzangu na mimi NDOTO ZETU ZINAFIA Kabatini ( TUNAWEKEWA VIKWAZO VIZITO KAMA TUKO JELA )
 
Kuna mtu ananiambia hii ni maeneo ya TRA ambapo wataalamu walijitokeza kwa usaili wa ajira.

Maswali yameniijia kichwani;

1. Ni kwamba kuna nafasi chache sana za ajira nchini ama watu wetu wanachagua sana kazi za kufanya?

2. Je, hakuna utaratibu bora zaidi, wenye staha na heshima, unaoweza kutenda haki kirahisi zaidi kuliko huu?

View attachment 578093




Chanzo : ukurasa wake wa facebook
Mpumbavu mmoja. Sasa kama yeye ambaye ni sehemu ya serikali inayotakiwa kuwa na sera ya ajira itakayohakikisha tatizo la ajira linapungua au kwisha kabisa anakuwa hana majibu anataka nani ajibu? Au ni maoni ya kiaina kwa bosi wake kwamba hakuna dawa mujarabu ya tatizo hili. Pumbavu zake sana, kuna nyakati shibe hulevya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
katika serikali hii kila mmoja analalamika. mawaziri waumize kichwa namna ya kutatua tatizo hili badala ya kulalamika...
 
sasa yeye ndo wakutupa majibu alafu anatuuliza tena ovyooo
 
Naibu waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Kigwangala amesikitishwa na kitendo kilichofanywa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma katika kuwafanyia usaili baadhi ya wataalamu waliojitokeza kwenye usaili. Kilichojiri interview ya TRA - Dar katika picha, huu ndo mtihani wamepewa

TRA.jpg

Baadhi ya Wataalam mbalimbali wakihangaika kutaka kusoma majina yao kabla ya kuanza kufanya usaili wa TRA jijini Dar es Salaam.

Leo asubuhi kwenye mitandao ya kijamii zilikuwa zinazagaa baadhi ya picha na video vikionyesha mamia ya watu waliojitokeza kufanya usaili wa kazi za TRA ambapo wengi wao walionekana kuzongana kwenye eneo dogo kufuatilia majina yao kama yapo kwenye karatasi zilizobandikwa ukutani jambo ambalo limemfanya Naibu Waziri kujiuliza maswali kwamba nchini Tanzania nafasi za kazi zimekuwa ni chache sana au watu wamekuwa wakichagua kazi za kufanya.

"Kuna mtu ananiambia hii ni maeneo ya TRA ambapo wataalamu walijitokeza kwa usaili wa ajira. Maswali yameniijia kichwani. Ni kwamba kuna nafasi chache sana za ajira nchini ama watu wetu wanachagua sana kazi za kufanya? Je, hakuna utaratibu bora zaidi, wenye staha na heshima, unaoweza kutenda haki kirahisi zaidi kuliko huu? aliuliza Kigwangala

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ilitangaza kufanya usaili kwa waombaji kazi waliochaguliwa kwa ajili ya usaili wa mchujo wa nafasi mbalimbali za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) zilizotangazwa hivi karibuni na kutaarifiwa kuwa usaili wa hatua ya mchujo utafanyika katika Mikoa/kanda 10 kuanzia 30, 31 Agosti na tarehe 2 Septemba, 2017.

EATV
 
Back
Top Bottom