Dr. George Kahangwa kugombea urais kupitia Upinzani

Dr. Kahangwa ni mt makini sana lakini nafasi anayoitaka ni kubwa mno kwake maaana sina uhakika hata kama ameshawahi kuwa mkuu wa Idara anapofanyia kazi zaidi ya vyeo vya UKANJANJA kwenye NCCR SACCOS
 
Dr. Kahangwa ni mt makini sana lakini nafasi anayoitaka ni kubwa mno kwake maaana sina uhakika hata kama ameshawahi kuwa mkuu wa Idara anapofanyia kazi zaidi ya vyeo vya UKANJANJA kwenye NCCR SACCOS
amesawahi lihombea urais wa Daruso.ameshakaimu
ukuu wa idara kwa miezi sita,sasa no mmoja wa viongozi wa udasa
 
Anhaaa, sasa nimeelewa. Kama sikosei huyu aligombea Ubunge karagwe safari iliyopita (Kama nimekosea nirekebishwe).
My take: Kuna mtindo umeibuka kwa wana siasa wengi (Orodha ni ndefu.....Kigwala ngwala, WaHasira, Ma Kamba ya Katani, Gereza, Rahisi Kabue, ....nk) kutangaza nia ya kugombea URAIS kumbe lengo lao liwe ubunge. Ni kujaribu kujenga taswira KUUUUBWA kwamba ni presidential material, ili kumbe wawe wabunge.......
 
Nimefuatialia kidogo kwa sasa, naambiwa mgombea mtarajiwa huyu
Alikuwa best student UDSM 2004, shahada ya awali,
Ana Masters kutoka University moja huo Finland
Ana PhD kutoka Uingereza, sandwich ya uchumi na elimu

Hapa unamaana Economics of Education? Kwa hapo Mlimani Mtaalamu aliyebobea katika eneo hilo ni Profesa J C J Galabawa, huyu alisoma Ihungo, Bukoba enzi hizo ikiwa inaitwa Thomas Moore... Jina alilolichukua kwa ajili ya shule yake ya sekondari pale Mbezi kwa Musuguli Dar......
 
Anhaaa, sasa nimeelewa. Kama sikosei huyu aligombea Ubunge karagwe safari iliyopita (Kama nimekosea nirekebishwe).
My take: Kuna mtindo umeibuka kwa wana siasa wengi (Orodha ni ndefu.....Kigwala ngwala, WaHasira, Ma Kamba ya Katani, Gereza, Rahisi Kabue, ....nk) kutangaza nia ya kugombea URAIS kumbe lengo lao liwe ubunge. Ni kujaribu kujenga taswira KUUUUBWA kwamba ni presidential material, ili kumbe wawe wabunge.......
Umekosea, aliyegombea ubunge Karagwe sio huyu wa UDSM
 
Wakuu, nimekumbana na hii ikisambazwa kwenye anwanipepe za wakazi wa jimbo fulani

MFAHAMU ZAIDI DKT. GEORGE LEONARD KAHANGWA

Dkt. George Leonard Kahangwa ni mwenyeji wa mkoa wa Kagera, Wilaya ya Missenyi, akitokea katika kata ya Kanyigo, kijiji cha Kikukwe. Alizaliwa tarehe 05 Mei, 1969.

Daktari huyu wa falsafa, kwa sasa ni mhadhiri katika chuo kikuu cha Dar es Salaam, kampasi ya Mlimani. Anafanya tafiti, kufundisha na kutoa huduma kwa jamii katika masuala ya uongozi, sera na mipango ya elimu.

Alipata shahada yake ya awali katika elimu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mnamo mwaka 2004. Alihitimu masomo hayo akiwa na ufaulu wa kiwango cha juu sana, kiasi cha kuibuka kuwa mwanafunzi bora wa kitivo, akiwa ndiye pekee aliyepata daraja la kwanza miongoni mwa wahitimu wa shahada ya BAED. Mwaka huo huo alihitimu mafunzo ya uongozi katika taasisi ya kijerumani iitwayo Fredrich Ebert Stiftung. Huko nako alimaliza akiwa akiwa mhitimu bora zaidi.

Baadaye aliendelea na masomo ya shahada ya uzamili (MAED) katika chuo kikuu hicho hicho cha Dar es Salaam na kuhitimu mnamo mwaka 2007. Amesoma pia masuala ya elimu ya kimataifa katika Chuo Kikuu cha Oulu cha nchini Finland, mwaka 2008.

clip_image002.jpg

Pichani akiwa Chuo Kikuu cha Oulu

Dkt. Kahangwa ni mhitimu wa shahada ya uzamivu (udaktari wa falsafa) katika Chuo Kikuu cha Bristol, nchini Uingereza ambako alitunukiwa pia stashahada ya umahili katika kufanya utafiti mnamo mwaka 2013. Andiko lake la tasnifu ya uzamivu lilihusu Ujenzi wa Uchumi wa Maarifa kupitia Sera na Vitendo katika Elimu ya Juu nchini Tanzania.

clip_image004.jpg

Kauli zake katika magazeti

Aidha Dkt. Kahangwa ameshiriki harakati mbalimbali za kuleta maendeleo, kujenga demokrasia na mageuzi nchini. Mathalani, ametoa mada kadhaa katika mijadala ya kitaifa hususan inayohusu elimu. Miongoni mwa mada alizowahi kuwasilisha ni zile zihusuzo haja ya kuufanyia mabadiliko mfumo wa elimu nchini. Nakala za mada hizi zinapatikana katika kitabu kinachouzwa katika mtandao wa Amazon, kiitwacho; Uchambuzi wa Sera ya Elimu ya Tanzania (pichani chini). Vilevile mada zake zimechapishwa mara kwa mara kama makala katika magazeti ya Mwananchi na RaiaTanzania.

clip_image006.jpg

Kitabu kilichotokana na mada zake

Maandiko yake ya kitaaluma ni pamoja na;
· The effects of Knowledge-Based Economy on Higher Education Practices in Tanzania
· Leadership and Management of Change for Education Quality in Primary Schools, Tanzania
· The impact of Teacher-Pupil Ratio on the Teaching and Learning Process, and Learners' Achievement.
· Ideals and Rules of Conduct in Haya Sayings (Emote)

clip_image008.jpg

Mojawapo za makala zake katika gazeti la mwananchi

Kuhusu uzoefu wake katika siasa na uongozi, Dkt. Kahangwa aliwahi kuwa mwenyekiti wa umoja wa vijana wa NCCR-Mageuzi ngazi ya Taifa; Mkuu wa Idara ya Itikadi, Sera na Mafunzo, Makamu mkuu wa chuo cha chama; na mjumbe wa halmashauri kuu ya chama. Kwa sasa ni Makamu mwenyekiti wa kamati maalum ya UKAWA.

clip_image010.jpg

Akiwa Ikulu (wa tatu kushoto) katika mazungumzo na Rais Kikwete kuhusu katiba mpya. Picha inayofuata ni wa pili kushoto.
clip_image012.jpg


Aliwahi pia kuwa Rais mwanzilishi (mhasisi) wa chama cha walimu-wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Kuhusu familia, Dkt. Kahangwa ni mtoto wa saba wa Mwalimu Gabriel Kahangwa (Marehemu) na Mama Anastazia Kokunyeta. Daktari ni mume wa mke mmoja na baba wa watoto wawili.

Dkt. Kahangwa anaamini kwamba haki huinua Taifa. Ana nia ya dhati ya kufanya kila linalowezekana ili wilaya ya Missenyi na Taifa la Tanzania kwa ujumla liwe na maendeleo yanayowalenga watu zaidi kuliko vitu; kukuza uchumi unaotafsirika wazi katika ustawi wa jamii; kuwapatia wananchi wote elimu bora na huduma nyinginezo za kijamii; na kumtokomeza adui ufisadi nchini.
Mawasiliano yake;
Baruapepe: kahangwagl@udsm.ac.tz
Simu: 0713 563212
 
Dr. George Kahangwa akichambua juzi akichambua sera mpya ya elimu aliipa daraja C baada ya kubaini mapungufu makubwa, na kuishauri serikali wakajipange upya ndipo waitumie sera hiyo. Hata hivyo ni mzuri ila uraisi bado. Apewe jimbo tu
 
Back
Top Bottom