Washawasha
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 16,976
- 13,434
Magufuli wale wote watakapatikana Na Hata ya ufisadi wawekwe kwenye blacklist wafilisiwe waporwe vyeti vyao
Nalog off
Nalog off
Hakika. Lakini,nimelenga hawa 'hazina' za taifa.
Mzee Tupatupa
Hivi tumewai kufikirisha vichwa vyetu kuwa waziri mkuu zile taarifa alipewa na kina nani? Au tumekuwa watu wa kusifia bila kujua taarifa zilipatikana patikana vipi?
Hii nchi ukiona mtu anaacha kazi ya kitaalam na yenye maslahi mazuri basi mtizame mara mbili mbili. Ukimchunguza utagundua harufu ya wizi na rushwa au uchotwaji wa mali za umma au kufanikisha wizi wa fedha za umma au yote kwa pamoja.
Mpaka leo bado najiuliza ni kwa nini binti mdogo kama Dr. Tulia alikimbilia siasa wakati alikua ana nafasi kubwa ya kutumia elimu yake kuisaidia serikali kama naibu mwanasheria mkuu wa serikali?
Bila shaka alikua anajua kuwa wanasiasa wanabebana hata pale wanapokua wameharibu hivyo akaenda kuungana na wenzake.
Mwingine ni Mwigulu na Makamba hawa walikua kwenye nafasi nyeti za kulitumikia taifa kwa kutumia elimu zao lakini ghafla wakaacha kazi na taaluma zao na kukimbilia siasa. Hawa nao wakichunguzwa sio watu wema hata kidogo. Umri wao na Mali zao zichunguzwe na marafiki zao kabla ya kupewa madaraka ndani ya serikali.
Kwa muda mrefu siasa zimekua ni kama mlezi wa majipu. Sasa umefika wakati wa kuyatumbua tu.
Tena aliukosa Uspika kamili kidogo sana.
Otherwise ndiyo angekuwa spika leo yule dada.
Nchi hii akiendelea kufukua bila shaka hata yeye mtumbua majipu ataishia kujitumbua, vinginevyo nauona mwisho wa aibu katika hizi sarakasi.
Huyo Msambichaka ni InjiniaMzee Tupatupa umemsahau Prof. Msambichaka aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi. Huyu ni msomi aliyebobea kwenye masual ya uchumi sijui alitumia vipi taaluma yake kuisaidia nchi.
Nyinyi wote ni wasomi wa ngazi ya Shahada ya Uzamivu. Nyinyi wote ni Wahadhiri wa UDSM. Nyinyi wote mmeanza kusikika na kuonekana wakati wa Bunge la Katiba. Nyinyi wote mlikuwa Wajumbe wa Bunge hilo. Wote mkawa na nyadhifa kwenye Bunge la Katiba.
Nyinyi wote mliteuliwa na aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi,Samwel Sitta kuwa Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania. Kutokana na imani kubwa kwenu na weledi wa kusaidia taifa katika nyanja zenu,mliteuliwa. Bodi ya Shirika au Kampuni ndiyo serikali ya mahali husika.
Bodi huamua,hung'amua,huchuja,huchunguza,huanzisha na hata kusitisha masuala mbalimbali kuhusu shirika au kampuni husika. Ndiyo watawala wenyewe. Mambo yote ya kimaamuzi,mema au mabaya,hufanywa na bodi. Pale Bandarini,watawala wa juu na pekee ni Bodi ya Mamlaka ya Bandari.
Mlikuwa Wajumbe wa Bodi iliyovunjwa hivi karibuni. Dr.Michael,kama mtaalamu wa biashara,ulikuwa wapi kuepusha makandokando ya kibiashara Bandarini? Dr. Tulia,kama mtaalamu wa sheria,ulikuwa wapi kudhibiti makandokando ya kisheria Bandarini kama Mjumbe wa Bodi?
Nyinyi mmechafuka. Mmetoa taswira mbaya kwa wasomi wanaopaswa kuaminiwa na kutumiwa. Mnapaswa kuwajibishwa katika kulinda chama,wasomi na hata uaminifu kwa watu weledi kama nyinyi. Mmechafuka!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Uko sahihi kabisa lakini kwa kuwa hawa ni wasomi wachumia tumbo watajifanya hamnazo!
Hili la dr Tulia ni wake up call kwa Rais achukue tahadhari sana katika teuzi zake mbali mbali! Nji hii imeoza, kwa jinsi alivyofast track uteuzi wa Tulia hadi kufikia unaibu spika inambidi JPM azinduke!
Mzee Tupatupa nadhan una Maana Hazina ya Chama