Teana wamechafuka kweli kweli....
Weewee unachanganya mambo. Kuna Prof. Msambichaka wawili: mmoja mchumi na mwingine mhandisi. Aliyekuwa bandarini ni injinia!Mzee Tupatupa umemsahau Prof. Msambichaka aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi. Huyu ni msomi aliyebobea kwenye masual ya uchumi sijui alitumia vipi taaluma yake kuisaidia nchi.
Uko sahihi kabisa lakini kwa kuwa hawa ni wasomi wachumia tumbo watajifanya hamnazo!
Hili la dr Tulia ni wake up call kwa Rais achukue tahadhari sana katika teuzi zake mbali mbali! Nji hii imeoza, kwa jinsi alivyofast track uteuzi wa Tulia hadi kufikia unaibu spika inambidi JPM azinduke!
Sisi tulijua chama chao sasa mafisi basi kumbe bado!.... Ndo maana ni bora baraza likachelewa kidogo ili kila idara imulikwe na isafishwe- pasiwepo na kasoro kama hizi, Mbobezi ataleta maelezo yake mareeeeeeefu kwa swali dogo-
Hasa mbobezi kachafuka kwelikweli!
Mzee Tupatupa umemsahau Prof. Msambichaka aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi. Huyu ni msomi aliyebobea kwenye masual ya uchumi sijui alitumia vipi taaluma yake kuisaidia nchi.
Nyinyi wote ni wasomi wa ngazi ya Shahada ya Uzamivu. Nyinyi wote ni Wahadhiri wa UDSM. Nyinyi wote mmeanza kusikika na kuonekana wakati wa Bunge la Katiba. Nyinyi wote mlikuwa Wajumbe wa Bunge hilo. Wote mkawa na nyadhifa kwenye Bunge la Katiba.
Nyinyi wote mliteuliwa na aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi,Samwel Sitta kuwa Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania. Kutokana na imani kubwa kwenu na weledi wa kusaidia taifa katika nyanja zenu,mliteuliwa. Bodi ya Shirika au Kampuni ndiyo serikali ya mahali husika.
Bodi huamua,hung'amua,huchuja,huchunguza,huanzisha na hata kusitisha masuala mbalimbali kuhusu shirika au kampuni husika. Ndiyo watawala wenyewe. Mambo yote ya kimaamuzi,mema au mabaya,hufanywa na bodi. Pale Bandarini,watawala wa juu na pekee ni Bodi ya Mamlaka ya Bandari.
Mlikuwa Wajumbe wa Bodi iliyovunjwa hivi karibuni. Dr.Michael,kama mtaalamu wa biashara,ulikuwa wapi kuepusha makandokando ya kibiashara Bandarini? Dr. Tulia,kama mtaalamu wa sheria,ulikuwa wapi kudhibiti makandokando ya kisheria Bandarini kama Mjumbe wa Bodi?
Nyinyi mmechafuka. Mmetoa taswira mbaya kwa wasomi wanaopaswa kuaminiwa na kutumiwa. Mnapaswa kuwajibishwa katika kulinda chama,wasomi na hata uaminifu kwa watu weledi kama nyinyi. Mmechafuka!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Mzee Tupatupa umemsahau Prof. Msambichaka aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi. Huyu ni msomi aliyebobea kwenye masual ya uchumi sijui alitumia vipi taaluma yake kuisaidia nchi.
Hatutavumilia Bunge liendeshwe na mtuhumiwa wa "UHUJUMU UCHUMI"!Huyo Tulia ajiuzuru nafasi yake ya unaibu spika maana ni aibu