VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,006
Nyinyi wote ni wasomi wa ngazi ya Shahada ya Uzamivu. Nyinyi wote ni Wahadhiri wa UDSM. Nyinyi wote mmeanza kusikika na kuonekana wakati wa Bunge la Katiba. Nyinyi wote mlikuwa Wajumbe wa Bunge hilo. Wote mkawa na nyadhifa kwenye Bunge la Katiba.
Nyinyi wote mliteuliwa na aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi,Samwel Sitta kuwa Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania. Kutokana na imani kubwa kwenu na weledi wa kusaidia taifa katika nyanja zenu,mliteuliwa. Bodi ya Shirika au Kampuni ndiyo serikali ya mahali husika.
Bodi huamua,hung'amua,huchuja,huchunguza,huanzisha na hata kusitisha masuala mbalimbali kuhusu shirika au kampuni husika. Ndiyo watawala wenyewe. Mambo yote ya kimaamuzi,mema au mabaya,hufanywa na bodi. Pale Bandarini,watawala wa juu na pekee ni Bodi ya Mamlaka ya Bandari.
Mlikuwa Wajumbe wa Bodi iliyovunjwa hivi karibuni. Dr.Michael,kama mtaalamu wa biashara,ulikuwa wapi kuepusha makandokando ya kibiashara Bandarini? Dr. Tulia,kama mtaalamu wa sheria,ulikuwa wapi kudhibiti makandokando ya kisheria Bandarini kama Mjumbe wa Bodi?
Nyinyi mmechafuka. Mmetoa taswira mbaya kwa wasomi wanaopaswa kuaminiwa na kutumiwa. Mnapaswa kuwajibishwa katika kulinda chama,wasomi na hata uaminifu kwa watu weledi kama nyinyi. Mmechafuka!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam