zomba
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 17,240
- 3,910
Sijamuelewa Zomba,anataka tuwe na CT scan au anataka tuendelee kununua mashangingi ambayo mwaka 2010 moja likuwa siyo chini ya $100,000 ukiweka na ushuru na blablah.Mwaka jana mbeya imepoteza mwanafunzi aliyemaliza kidato cha nne kwa kukosa CTscan,kama tunaweza kuhamisha pesa kwenda Uswis kwa nini tuzinunue vifaa muhimu vya hospitali?Tusiangalie jana ilikuwaje,bali leo tunafanyaje?
Viongozi wa Serikali yetu inatakiwa kuwa wakali na walaji pesa za watanzania.Hivi kama wakiondoa sitting allowance za wabunge kwa miezi hii mitatu tutaserve kiasi gani ili tuweze kuboresha hospitali zetu?
Hivi ni haki mbunge tuliyemtuma kutetea maslahi yatu yupo kwa ajili ya maslahi yake zaidi?
Mie nadhani tuangelie hili kwa mapana zaidi tukalijadili badala ya kulaumu madaktari,kuwatukana na hata kuwatesa bila sababu.Tuone ni kwanini tusiwe na huduma bora za afya na siyo bora huduma?
Kwa nini keki ya taifa tuzigawane kwa haki?
Wanasema hivi ukila na kipofu usimshike mkono............
Wewe unakuja na mada mpya, soma kichwa cha habari na post #1 inasemaje. Kama una mada mpya anzisha nyuzi tutakuja amma kukupa darsa amma kukuunga mkono, usiwe na shaka na usibadili hoja, tutakuwa hatufiki.