Dr. Chitage: Mashine moja ya CT scan ni sawa na bei ya Toyata shangingi moja! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Chitage: Mashine moja ya CT scan ni sawa na bei ya Toyata shangingi moja!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Salary Slip, Jul 1, 2012.

 1. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #1
  Jul 1, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,993
  Likes Received: 37,683
  Trophy Points: 280
  Katibu wa jumuiya ya madaktari nchini ameweka wazi kuwa bei ya mashine moja ya CT scan ni sawa na bei ya kununulia shangingi moja.Alisema kama serikali ingekuwa na nia ya kununua mashine hiyo isingeshindwa. kwa habari zaidi soma gazeti la mwananchi la leo.

  Binafsi habari hii imichefua na kunisikitisha kuona ni jinsi gani serikali yete inavyoendekeza anasa wakati inashindwa kutoa huduma za msingi kwa watu wake.Mashine ya CT scan pale muhimbili kwa mujibu wa vyombo vya habari imekuwa mbovu kwa muda wa miezi saba ila serikali inapiga dana dana kuitengeneza na matengenezo yake ni kama milioni mbili hivi kama sikosei.Kama nimekosei hiyo gharama ya matengenezo mwenye uhakika atujuze.

  Mbali na mashine hiyo kuna hospitali zingine hapa nchini hazina hata x-ray machine.Kama uliangalia taarifa ya habari ya ITV juzi usiku tatizo la kukosekana kwa mashine ya x-ray liliripotiwa ktk hospitali ya serikali mkoani Tanga ambapo mtu aliepata ajali alishindwa kuhudumiwa kutukona na kukosekana kwa mashine hiyo.

  Nasema hii ni aibu kwa serikali na inabidi kwenye katiba mpya tupitishe uamuzi wa kutaka viongozi wa serikali nao watibiwe hapa nchini na ipige marufuku viongozi kutibiwa nje ya nchi.Labda hii itasaidia kuondoa dhuluma hii. Sasa madaktari wanapogoma nani wa kulaumiwa kama sio serikali?Hivi haya ndio maisha bora kwa kila mtanzania!
   
 2. PPM

  PPM JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 839
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu haujapanda shangingi ukaona raha yake, hata hizi ndege za precisian hazina raha kama mashangingi
   
 3. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2012
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  My GOD!
   
 4. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  inasikitisha sana...kwa gharama tu serikali iliyotumia kusheherekea miaka 50 ya uhuru sijui wangenunua ct scan ngapi?
   
 5. kelvito

  kelvito JF-Expert Member

  #5
  Jul 1, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 388
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni udhaifu tu wajamaa!
   
 6. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #6
  Jul 1, 2012
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Ningependa kujua bei za mashine mbalimbali za afya ili nilinganishe na vitu ambavyo serikali inavipa kipaumbele km. mashangingi na matamasha.
   
 7. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #7
  Jul 1, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,544
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  haya ndio mambo ya msingi yakuongea .
   
 8. Kambaku

  Kambaku JF-Expert Member

  #8
  Jul 1, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 1,985
  Likes Received: 2,894
  Trophy Points: 280
  Kaka we umepinda si kidogo aisee.........
   
 9. kibol

  kibol JF-Expert Member

  #9
  Jul 1, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 3,137
  Likes Received: 379
  Trophy Points: 180
  Kwenye ishu ya vipaumbele (priorities) tulisha fail siku nyingi sana,hatujui kipi tufanye na kipi tuache ktk muda fulani,kupanga ni kuchagua km umeshindwa kuchagua unafikir kuna kitu gani tena?

  Kulikuwa na umuhimu gani wa kufanya sherehe ya miaka 50 ya uhuru kw gharama kubwa kiasi kile?

  Kulikuwa na umuhimu gani wa kukimbiza mwenge kwa mwaka huu wkt hata azma yake haieleweki?

  Kulikuwa na umuhimu gani wa kuongeza ukubwa wa baraza la mawazir badala ya kuincrease efficience ktk mawaziri wachache?kulikua na ulazima gani wa kuongeza mikoa na wilaya ktk kipindi hiki?

  Haya ni machache lakini yako mengi sana ya kiuendawazimu yanayofanywa na serikali hii DHAIFU naya KICHOVU.
   
 10. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #10
  Jul 1, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,393
  Trophy Points: 280
  hata hospital ya rufaa mkoa lindi haina x ray eti mbovu,govt haina pesa
   
 11. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #11
  Jul 1, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Huyo Daktari ni muongo wa kutupwa, siku hizi kila kitu kiko wazi, gharama ya CT scan hii hapa:

  the compute tomography machine costs depends upon the technology systems
  siemens ------------------200000 usd approx
  toshiba -------------------180000 usd approx
  beckam coulter------------250000 usd approx
  sharp------------------------200000 usd approx
  ge----------------------------300000 usd approx
  phillips ----------------------140000 usd approx  Plus software and technician time. We just got a new siemens definition and its costing 450k (minus software upgrades) so that 200k is really low ball.

  There is also the cost of the Tomography room where the unit sits in. It consists of specialty HVAC system that provide perfect humidity and temp.control. Also specail independent electrical circuits to power the equipment, and RAM (radio absorbent)materials for the walls. The cost of a CT room can varry from $250,000- $750,000.
   
 12. d

  davidfrance82 Member

  #12
  Jul 1, 2012
  Joined: Feb 13, 2012
  Messages: 55
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  mkuu umeilewa hiyo paste yako? angalia vizuri ulipocopy...........si lazima uchangie kitu ambacho huna ujuzi nacho..dr.dee
   
 13. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #13
  Jul 1, 2012
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Inasikitisha kuwa wewe unaonekana mtaalam lakini bado unatetea upuuzi. Rpoti ya CAG iliweka bayana kuwa mashangingi yaliyopo serikalini kwa sasa yanagharimu kama Tshs. 5 trillioni na bado wanendelea kununua kila kukicha. Kama wangekuwa wanaweka vipaumbele vizuri, kila Hospitali ya mkoa ingekuwa na CT scan yake pamoja na vifaa vingine muhimu.

  Kwa hili serikali haina pa kujisitiri, UDHAIFU unajionesha waziwazi...:hat:
   
 14. F

  FJM JF-Expert Member

  #14
  Jul 1, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  zomba, kwa bei hizo chukulia philips 140,000 x1600 = Tshs 224,000,000/- Shangingi bei gani?
  Hata hivyo unaweza kuishi bila shangingi, lakini kama hakuna vifaa stahiki vya kutibu/kujua ugonjwa badi uhai unakuwa hatarini.

  Serikali ina miliki magari yenye thamani ya Tsh 5 trillion. Wangetoa hapo trillion moja tu ikaelekezwa kununua vifaa kwenye hospitali zetu tungeokoa maisha ya watu wengi. Ukishinda Muhimbili hata kwa siku moja tu utaona ni jinsi gani mambo ni magumu. Huko mikoani ndio usiseme. Nilikuwa Mara kwa kweli inatia huruma. Madaktari wanatumia vibaratari kusaidia wamama wanaojifungua. Hata maji hakuna!

  Kama kuna mtu anaweza kuweka idadi ya hospitali kubwa za serikali (Wilaya & Mkoa) halafu tukawa na list ya vifaa muhimu vinavyokosekana including x-machines na vitanda, then tupige hesabu. Pengine wabunge wanatakiwa wafanye hii kazi na kujua walau pa kuanzia ni wapi.
   
 15. Mama Mdogo

  Mama Mdogo JF-Expert Member

  #15
  Jul 1, 2012
  Joined: Nov 21, 2007
  Messages: 2,866
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Niliwahi pitia taarifa moja toka Wiizara ya Afya kwa mwaka 2010 iliyoonyesha kuwa;

  kati ya X-ray machines 350 zilizokuwepo nchini mwaka huo, 75 zilikuwa mbovu (21.4 %), na kati ya utra Sound machine 251 zilizokuwepo nchini mwaka huo, 8 zilikuwa mbovu (3.2 %). Vilevile kati ya viti 477 vya kutumia kutumia kutibia meno, 77 vililikuwa vibovu (16.1 %), na kati ya X ray machine 58 za kuchunguzia meno, 17 zilikuwa mbovu (29.3 %).

  Takwimu hizi hazioonyesh dalili njema kuhusu upatikanaji wa huduma za vipimo vya huduma za afya kwa watanzania. Kwa mwaka jana, na huu sijui kama ndiyo hoi zaidi au nafuu maradufu. Nendeni Wizara ya Afya mukawaulize, au tembelea website yao (http://www.moh.go.tz) labda waweza ambulia kitu, (mimi nimejaribu nimeshindwa kupitia simu yangu ya kizamani).
   
 16. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #16
  Jul 1, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mtu akikuita zombi au zomba bora ujiue
   
 17. C

  Chintu JF-Expert Member

  #17
  Jul 1, 2012
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 3,403
  Likes Received: 857
  Trophy Points: 280
  Ok Zomba, lets say upo right. sasa tupe faida ya shangingi over CT scan kwa waTz.
   
 18. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #18
  Jul 1, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Utasikia mijinga kule bungeni inasimama na kusema kwanza naunga mkono 100 kwa 100....wakati issues zinazo matter the most hazipewi kipaumbele. SHAME Bunge la viti maalum.
   
 19. Root

  Root JF-Expert Member

  #19
  Jul 1, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,242
  Likes Received: 12,963
  Trophy Points: 280
  huyo jamaa alie paste hizo bei inaonekana anajua kuwa ni tsh pili dollar rate ya xchange ni 1585-1590 inategemea na bureau
   
 20. k

  kajima JF-Expert Member

  #20
  Jul 1, 2012
  Joined: Dec 5, 2009
  Messages: 865
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Kutokana na utafiti huu mdogo....ni wazi kuwa Serikali yaweza kutatua maswala ya vitendea kazi
  Lakini kwanini Serikali haifanyi hivyo?

  Lakini hapana, swali latikiwa kuwa: Nani ananufaika na ukosefu wa vitendea kazi hospitali za Serikali? Ufisadi mwengine huu
   
Loading...