Unachoshindwa kuelewa ni kuwa nchi hii iliuliwa kifo kibaya sana, toka tulikuwa wasafirishaji wa kwanza wa mazao ya kilimo katika Afrika mpaka kuwa maskini wa kwanza katika Afrika, kwa miaka 24 tuliyafanya hayo tu, ya kuibomoa bomoa nchi. Leo hii tunaona yanayofanyika, leo Tanzania ya Kikwete tuna miradi ya barabara kuliko nchi yoyote ya Afrika Mashariki na kati na pengine ni Afrika nzima. Leo Tanzania hii iliyokuwa hohehahe tuna CT scan na MRI za bure.
Leo Tanzania hii iliyokuwa maskini wa mwisho duniani tuna akiba ya chakula. Leo Tanzania hii hii tuliokuwa tunaletewa msaada mpaka unga wa uji (wa manjano) leo tuna uwezo wa kuuza mahindi nje ya nchi.
Nakuhisi ni mtoto mdogo sana na hujui tulipotoka na ndio maana huwezi kuthamini leo tuko wapi.
kubomoa rahisi kuliko kujenga. Nyumba inayobomolewa kwa siku moja inachukuwa mwaka kuijenga. Sasa fikiri nchi iliyobomolewa kwa miaka 24 itakuchukuwa miaka mingapi kuijenga? ukipata jibu ukubali kuwa, Kikwete anafanya miujiza kwa jinsi anavyotuletea maendeleao ya haraka haraka na ya rekodi katika kila nyanja. Ukweli ubaki kuwa ukweli na tuwache uongo.
Wengi roho zinzwauma kwanini leo huyu aweze waliposhindwa tunaifkiri kuwa ni watakatifu. Hakuna zaidi ya hilo, ni roho za kichawi tu.
Tuongelee afya kabla ya Kikwete na leo. Takwimu tu zinawasuta.
zomba, unaongea vizuri kuliko Wassira!
Ninavyojua mimi huko nyuma tulikuwa na ATC na ilikuwa na ndege zinaenda nchi za nje, elimu ilikuwa bure, bure, bure kabisa, huduma za afya zilikuwa bure, 90% ya watanzania walikuwa wanajuwa kusoma na kuandika, tulikuwa na viwanda ya kubangua korosho, tulikuwa na Tanganyika Packers, General Tyre, National Milling, Ranchi za taifa, Mwatex, Mutex, Machine Tools, Tanneries, usafiri wa reli na kubwa zaidi hatukuwa na mashimo makubwa kama yale ya Bulyanhulu, au Nyamongo
Pili, kama nchi tulijua tunasimama wapi kwenye ulingo wa kimataifa. Mambo ya kukodisha bendera hayakuwepo na mtu alipojaribu kuleta kiburi na mipaka ya nchi yetu tulimtandika vilivyo - kaulize wajukuu wa Idd Amin. Sasa hivi wazamiaji wanakuja hadi Dodoma hakuna mtu wa kuwazuia, Kibondo watu wanachwapa kila siku na watu toka nchi jirani (fedheha).
Tatu, kwenye red: Sijui mwenzetu wewe unapata data toka wapi ila kaa ukijua kwa sasa Tanzania ni ya tatu duniani kwa kupata misaada!