Utasikia mijinga kule bungeni inasimama na kusema kwanza naunga mkono 100 kwa 100....wakati issues zinazo matter the most hazipewi kipaumbele. SHAME Bunge la viti maalum.
zomba, kama nimekupata vizuri ni kwamba unasema baba aendelee kula hotelini kwa sababu jiko ni bovu!
Kama taifa ni lini tutaacha kuhemea kwa wanaume wengine waliowekeza kwenye CT-Scan machine na makorombwezo mengine? Omba omba kuanzia vyandarua mpaka vipimo/matibabu! Lakini ni kweli Tanzania haina uwezo huo? Ulishaona magari wanayotumia viongozi wa India?
Na hizo safari anakwenda kucheza huko? leo hii una mashine ya CT scan, kabla ya Kikwete ulikuwa hata huijui ni nini? leo hii una mtambo wa MRI ambao kabla ya Kikwete ilikuwa ni lazima uende Nairobi, au hilo hulijui? Leo unachuo cha kufundisha namna ya kutibu na kufanya upasuaji wa moyo, au hilo hulijui? leo Muhimbili una jengo la "outpatient" bora katika Afrika Mashariki, au hilo hulijui? leo Muhimbili una chumba cha matibabu ya meno bora katika afrika mashariki, kwa vifaa, urahisi na utaalaam, au hilo hulijui? unajuwa kuwa watu wanatoka Afrika mashariki nzima kuja hapa kutibiwa meno? au hilo hulijui? Unajuwa kuwa watu wanatoka Afrika mshariki na ya kati na maka Middle East kuja hapa kutibiwa baddhi ya kansa> au hilo hulijui? na hayo yote ni wakati wa Kikwete. Au hilo hulijui?
Tazama hii:https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/136909-ct-scan-mri-muhimbili-buree.html
Ukimaliza, fananisha na hii: How much does an MRI scan cost?
Huyo ndio Kikwete na hizo ndio safari anazozifanya, kwa faida yako na yangu na ya Watanzania wote.
Leo MRI hata US inagharimu si chini ya $ 500 kwa kipimo Tanzania ya Kikwete unafanyiwa kwa ngapi? fata link hiyo ya kwanza, halafu uje kuniambia wale waliokuwa kabla ya Kikwete walikuwa wapi? wamekaa tu ofisini wana saini makaratasi?
Wabunge wengi wa CCM wamekuwa kama madodoki, wananyonya kila kitu! Ni vigumu kuwatofautisha kielimu na wanafanya kazi kama "robot". Wamesumishwa na rushwa na wanafikiri kwa kutumia matumbo na kwato! Wangekuwa makini wasingeiunga mkono bajeti ya kijinga hii kwa "asilimia mia kwa mia" na baadhi yao "mia tatu." Shame unto them!!!
hapana nimeisoma zile shule zetu za al-haramain al-multaz al-queda na al-Shabab tumejifunza kugomea sensa kudai kadhi mkuu, kula pilau na juice ya miwa kuvaa gobazi Pamoja na visuruali vifupiTatizo lenu huwa mnaongea kama vile hamjaenda shule za St. Kayumba, au ndio NECTA?
Hivi ni nini unachotaka kukisema.
Upo sahihi kiasi, lakini unakosea pale unapoegemea matokeo bila ya kujumuisha 'nguvu' iliyotumika kupata hayo matokeo. Chochote tulichonacho kwenye hospitali zetu kinalangana na uwezo tulionao? Hapa nataka nikumbushe mashimbo (madini), uvuvi, wanyama hai, EPA etc. Na hata hiyo CT-scan serikali ina deni kubwa na mbaya zaidi haifanyi kazi.
Na kama kweli tunaamini kuwa tuna hatua nzuri kwenye sekta ya afya i.e best outpatient building in EAC ni vema tukajiuliza, hii traffic ya wakubwa kwenda India na Ujerumani wamepotea njia?
Mkuu haujapanda shangingi ukaona raha yake, hata hizi ndege za precisian hazina raha kama mashangingi
ati kabla ya jk hukua na ct scan
naona mtu analazimisha technology advancement iwe imeletwa na jk
mwisho utasema ipads zimekuja coz jk yupo madarakani
hapana nimeisoma zile shule zetu za al-haramain al-multaz al-queda na al-Shabab tumejifunza kugomea sensa kudai kadhi mkuu, kula pilau na juice ya miwa kuvaa gobazi Pamoja na visuruali vifupi
ati kabla ya jk hukua na ct scan
naona mtu analazimisha technology advancement iwe imeletwa na jk
mwisho utasema ipads zimekuja coz jk yupo madarakani
Huyu nae eti kabla ya kikwete kulikuwa hakuna Ct scan!!! Kabla ya Kikwete kulikuwa hakuna miaka hamsini ya uhuru.
Nimependa hii. Bajeti ya uhuru tungepata CT Scan angalau mpaka wilayani! Hawa jamaa wantia kinyaa sana.inasikitisha sana...kwa gharama tu serikali iliyotumia kusheherekea miaka 50 ya uhuru sijui wangenunua ct scan ngapi?
Maktari nao pia ni NUKSI SANA. Mara ngapi nao wanauza madawa yetu! Wao na serikali wote ni tatizo tu.Kingine hapa kwetu madokta wana tabia ya kuharibu mashine ili watu watumie za kwenye kliniki zao binafsi, hilo la CT ya muhimbili ni mfano mzuri tu...wao madaktari mbona hawajairekebisha hiyo CT miezi yote hiyo ilivyokuwa mbovu? au hilo swala hadi serikali kuu ihusike vilevile kwa mshine za Xray swala ni hilohilo...sasa kama wanaletewa vifaa halafu utunzaji inakuwa issue nani alaumiwe hapo?