Napenda nikiri kuwa mi ni mfuasi mzuri sana wa mada kama hizi fikirishi na natambua mchango wa kila alieshiriki na ninawashukuru mno,maana kwa namna moja au nyingine mnanijenga.
Hivi ni kwanini tumefikia kuwaza haya yote?
1.Je tunahisi kuna mahali tumekosea?
2.Au kuna watu wanatuonea?(kwa maana kwamba kuna mahali tulitakiwa kuwepo na haijawa hivyo?)
Mwisho,nafikiria kwamba kabla ya kulaumu mtu au kitu chochote ni vema tukaanza na nafsi zetu,ni sisi ndio tunapashwa kijitengenezea ustawi bora wa maisha bila kuwaza nani alifanya nini,na je alikosea au alipatia.Tusiwe watu wa kuhukumu na kudharau mambo yaliyofanywa na wengine waliopita.Na pia tusisahau,hakuna alietayari kuharibu maisha yake kwa ajili ya mwengine,kwahyo hata hao tunaowalaumu leo,yote waliofanya ni kwa ajili yao na watu wao.Kwahiyo kitu cha msingi ni kujijengea mitazamo itayotuimarisha kifikra na kiuchumi maana ndio adui mkubwa tunaepambana nae ukiacha huyo wakuitwa shetani anaesingiziwa kila leo.
Naomba kuwasilisha
wasalaam