Dr. Bashiru: CCM itashinda kwa kishindo

Dr. Bashiru: CCM itashinda kwa kishindo

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
Joined
May 13, 2018
Posts
439
Reaction score
742
TAARIFA

01 Novemba, 2019

Dkt. Bashiru Ally Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Asubuhi ya leo, ametembelewa na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba Jijini Dar es salaam.

Viongozi hao wa Baraza la Wawakilishi pamoja na mambo mengine, wamempongeza Katibu Mkuu kwa kuendelea kufanya kazi ya kukiimarisha Chama na hasa kusimamia misingi ya haki na usawa katika kipindi hiki cha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa upande wa Tanzania Bara, ambao unatarajiwa kufanyika tarehe 24 Novemba, Mwaka huu.

Aidha, akizungumza na viongozi hao, Dkt. Bashiru amewahakikishia kuwa, CCM imejipanga kuhakikisha inashinda kwa kishindo na ushindi wa awamu hii utakuwa ni ushindi wa kihistoria katika Chama Chetu.

"Hakuna wa kuizuia CCM kushinda kwa kishindo awamu hii, Chama kimetimiza wajibu wake na wananchi wanaona mafanikio makubwa yanayoendelea kupatikana kupitia serikali ya awamu ya tano, hivyo ushindi wa kishindo ni hakika." Dkt. Bashiru

Wajumbe hao kutoka Baraza la Wawakilishi ni Ndg. Rashid Shamsi Jimbo la Magomeni Zanzibar, Shaibu Ali Said (Chonga), Mtumwa Yusuph (Bumbwini), Masoud Masoud (Bububu), Bihindi Khamis Mkoa wa Kaskazini Pemba (viti maalum).

Imetolewa na;
CHAMA CHA MAPINDUZI
OFISI NDOGO LUMUMBA.
IMG-20191101-WA0066.jpeg
 
He is very right.

Maana kwa sasa upinzani haupo.
So tu upinzani haupo bali UKawa haupo,Dr Slaa hayupo na Lowasa hayupo ambao ndio walikuwa main factor ya ushindi wao kwa miaka yote
 
So tu upinzani haupo bali UKawa haupo,Dr Slaa hayupo na Lowasa hayupo ambao ndio walikuwa main factor ya ushindi wao kwa miaka yote

Unadhani ukiwataja hao ndio utatupoteza maboya? Tunajua hakuna ushindani bali kuna ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura, ndio maana watu tunaojitambua hatuko tayari kushiriki huo ushenzi. Pikeni idadi ya wapiga kura, lakini ukweli wa kuwa ccm haikubaliki utaonekana chini ya idadi ndogo sana ya wapiga kura kupata kuonekana.
 
Back
Top Bottom