Dr. Bashiru: CCM itashinda kwa kishindo

Dr. Bashiru: CCM itashinda kwa kishindo

Ccm wakae wakijua kuwa matendo anayotenda MTU kwa makusudi na akijua adhali zake mbele ya Mungu ni dhambi. Tunayaona MA CCM yanaingia kutawadha eti yafanye SWALA TAKATIFU Msikitini yananyoosha Mikono na kufunika vifua hapo hapo ndo ma 'master mind' was wizi was kura na mipango yamakusudi ya kudhurumu wenzao wapinzani. Oneni Woga kwa Mwenyezi Mungu, wewe muumini, kuna hukumu yako wenzio tunawashitakia.
Wa Kristo wengi unawaona makanisani wamefumba macho lakini ni washirika kuandaa plan ovu dhidi ya wapinzani Mungu anawaona!
Katika dhuruma tunazozisikia na kuziona mitandaoni na ripoti mbali mbali kuelekea uchaguzi huu we mitaa huwezi sikia kiongozi yeyote anaikemea Ccm na wale wanaofanya faulu zote hizi dhidi ya wapinzani MUNGU ANAWAONA CHEZA NA MENGINE YOTE SIO HAKI ZA WATU.
Cha ajabu Maaskofu, Mashehe, maimamu,mapadre, wachungaji, waijiristi, hatuwasikii. Hivi ninyi ...???

CCM wasomewe Albadiri mapema kwa faulu wanazowafanyia wapinzani huko mikoani wilayani
 
Tangu awamu ya pili hakujawahi kuwa na CCM dhaifu kama hii.
Wakijiandaa kusherehekea kwa ushindi wa kishindo, Kwa mwendelezo huu wa dhuluma, natamani wananchi waanze kampeni kuzodoa kijani mtaani, sauti ya umma ina nguvu kubwa sana.
Ujinga mikutano rasimi ya kiserikali mkuu wa nchi, kijani mavazi na salamu za kichama as if kikao cha chama.
Zomea zodoa kijani mpaka pale haki na katiba ya nchi ikiheshimiwa.
 
TAARIFA

01 Novemba, 2019

Dkt. Bashiru Ally Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Asubuhi ya leo, ametembelewa na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba Jijini Dar es salaam.

Viongozi hao wa Baraza la Wawakilishi pamoja na mambo mengine, wamempongeza Katibu Mkuu kwa kuendelea kufanya kazi ya kukiimarisha Chama na hasa kusimamia misingi ya haki na usawa katika kipindi hiki cha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa upande wa Tanzania Bara, ambao unatarajiwa kufanyika tarehe 24 Novemba, Mwaka huu.

Aidha, akizungumza na viongozi hao, Dkt. Bashiru amewahakikishia kuwa, CCM imejipanga kuhakikisha inashinda kwa kishindo na ushindi wa awamu hii utakuwa ni ushindi wa kihistoria katika Chama Chetu.

"Hakuna wa kuizuia CCM kushinda kwa kishindo awamu hii, Chama kimetimiza wajibu wake na wananchi wanaona mafanikio makubwa yanayoendelea kupatikana kupitia serikali ya awamu ya tano, hivyo ushindi wa kishindo ni hakika." Dkt. Bashiru

Wajumbe hao kutoka Baraza la Wawakilishi ni Ndg. Rashid Shamsi Jimbo la Magomeni Zanzibar, Shaibu Ali Said (Chonga), Mtumwa Yusuph (Bumbwini), Masoud Masoud (Bububu), Bihindi Khamis Mkoa wa Kaskazini Pemba (viti maalum).

Imetolewa na;
CHAMA CHA MAPINDUZI
OFISI NDOGO LUMUMBA. View attachment 1250990
Huo ni ukweli usiopingika.
Na hakuna sare za kugawa kila mwanachama ajinunulie yake
 
Wajingaa sana nyie bila aibu mnaingia ulingoni na watu mliowafunga vitambaa usoni na vizingiti kibao, kisha mnajisifu

Ruling part differs from opposition party campaigns
 
TAARIFA

01 Novemba, 2019

Dkt. Bashiru Ally Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Asubuhi ya leo, ametembelewa na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba Jijini Dar es salaam.

Viongozi hao wa Baraza la Wawakilishi pamoja na mambo mengine, wamempongeza Katibu Mkuu kwa kuendelea kufanya kazi ya kukiimarisha Chama na hasa kusimamia misingi ya haki na usawa katika kipindi hiki cha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa upande wa Tanzania Bara, ambao unatarajiwa kufanyika tarehe 24 Novemba, Mwaka huu.

Aidha, akizungumza na viongozi hao, Dkt. Bashiru amewahakikishia kuwa, CCM imejipanga kuhakikisha inashinda kwa kishindo na ushindi wa awamu hii utakuwa ni ushindi wa kihistoria katika Chama Chetu.

"Hakuna wa kuizuia CCM kushinda kwa kishindo awamu hii, Chama kimetimiza wajibu wake na wananchi wanaona mafanikio makubwa yanayoendelea kupatikana kupitia serikali ya awamu ya tano, hivyo ushindi wa kishindo ni hakika." Dkt. Bashiru

Wajumbe hao kutoka Baraza la Wawakilishi ni Ndg. Rashid Shamsi Jimbo la Magomeni Zanzibar, Shaibu Ali Said (Chonga), Mtumwa Yusuph (Bumbwini), Masoud Masoud (Bububu), Bihindi Khamis Mkoa wa Kaskazini Pemba (viti maalum).

Imetolewa na;
CHAMA CHA MAPINDUZI
OFISI NDOGO LUMUMBA. View attachment 1250990
Hivi mtoto wake k'm hua anajisikiaje baba ake anavopelekeshwa jamani.
 
Back
Top Bottom