Dr. Bashiru: CCM itashinda kwa kishindo

Dr. Bashiru: CCM itashinda kwa kishindo

TAARIFA

01 Novemba, 2019

Dkt. Bashiru Ally Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Asubuhi ya leo, ametembelewa na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba Jijini Dar es salaam.

Viongozi hao wa Baraza la Wawakilishi pamoja na mambo mengine, wamempongeza Katibu Mkuu kwa kuendelea kufanya kazi ya kukiimarisha Chama na hasa kusimamia misingi ya haki na usawa katika kipindi hiki cha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa upande wa Tanzania Bara, ambao unatarajiwa kufanyika tarehe 24 Novemba, Mwaka huu.

Aidha, akizungumza na viongozi hao, Dkt. Bashiru amewahakikishia kuwa, CCM imejipanga kuhakikisha inashinda kwa kishindo na ushindi wa awamu hii utakuwa ni ushindi wa kihistoria katika Chama Chetu.

"Hakuna wa kuizuia CCM kushinda kwa kishindo awamu hii, Chama kimetimiza wajibu wake na wananchi wanaona mafanikio makubwa yanayoendelea kupatikana kupitia serikali ya awamu ya tano, hivyo ushindi wa kishindo ni hakika." Dkt. Bashiru

Wajumbe hao kutoka Baraza la Wawakilishi ni Ndg. Rashid Shamsi Jimbo la Magomeni Zanzibar, Shaibu Ali Said (Chonga), Mtumwa Yusuph (Bumbwini), Masoud Masoud (Bububu), Bihindi Khamis Mkoa wa Kaskazini Pemba (viti maalum).

Imetolewa na;
CHAMA CHA MAPINDUZI
OFISI NDOGO LUMUMBA. View attachment 1250990
CCM jiamini tu Toa fomu mshindane na upinzani kwa hoja
 
Ccm inashindana na nani?
 
Ukiwa unakimbia peke yako lazima ushinde. Mmezuia wenzenu kufanya siasa mnafanya ninyi tu kwanini msishinde na ninyi ndio mnaosimamia uchaguzi na kutajitangaza washindi
 
Kwa staili hii ya watendaji kukimbia ofisi zao ili wasiwape fomu wagombea Wa upinzani, kwa staili hii ya wagombea Wa upinzani waliobahatika kuchukua fomu kulundikwa ndani kwa amri za wakuu Wa wilaya, kwa staili hii ya jeshi LA polis kukamata wagombea Wa upinzani, ccm itashinda kwa 99%
 
Hawa watakuwa wanashindana na maluweluwe siyo bure, kwa mtu mwenye akili timamu hawezi akashinda kwa kishindo kwa kushindana na wapinzani ambao hata fomu za uchaguzi wamenyimwa, wanapokwenda kuchukua fomu wanaishia mikononi mwapolisi na kupelekwa jela, waliofanikiwa kupewa fomu wanapozirudisha fomu zinachanwa, labda kama watashinda kwa kishindo kwa kuwafunga wapinzani hapo atakuwa sahihi.
 
Hii nchi ni yetu wote.acha tusubiri Olympic ya nchi za waongo na wanafiki pengine tutaambulia medali.
 
Subiria mbwembwe za kina polepole, utasikia ccm imepita kwa kishindoooooo, tena bila kupingwa.Kiukweli ccm ni mashetan
 
TAARIFA

01 Novemba, 2019

Dkt. Bashiru Ally Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Asubuhi ya leo, ametembelewa na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba Jijini Dar es salaam.

Viongozi hao wa Baraza la Wawakilishi pamoja na mambo mengine, wamempongeza Katibu Mkuu kwa kuendelea kufanya kazi ya kukiimarisha Chama na hasa kusimamia misingi ya haki na usawa katika kipindi hiki cha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa upande wa Tanzania Bara, ambao unatarajiwa kufanyika tarehe 24 Novemba, Mwaka huu.

Aidha, akizungumza na viongozi hao, Dkt. Bashiru amewahakikishia kuwa, CCM imejipanga kuhakikisha inashinda kwa kishindo na ushindi wa awamu hii utakuwa ni ushindi wa kihistoria katika Chama Chetu.

"Hakuna wa kuizuia CCM kushinda kwa kishindo awamu hii, Chama kimetimiza wajibu wake na wananchi wanaona mafanikio makubwa yanayoendelea kupatikana kupitia serikali ya awamu ya tano, hivyo ushindi wa kishindo ni hakika." Dkt. Bashiru

Wajumbe hao kutoka Baraza la Wawakilishi ni Ndg. Rashid Shamsi Jimbo la Magomeni Zanzibar, Shaibu Ali Said (Chonga), Mtumwa Yusuph (Bumbwini), Masoud Masoud (Bububu), Bihindi Khamis Mkoa wa Kaskazini Pemba (viti maalum).

Imetolewa na;
CHAMA CHA MAPINDUZI
OFISI NDOGO LUMUMBA. View attachment 1250990
NDUMBA TUPU ZIMEJAA HAPO
 
He is very right.

Maana kwa sasa upinzani haupo.
Acha kuvuta Bangi kisha kujidanganya, upinzani ungekuwa haupo mngehangaika kuwanyima form? Kuwapiga mapanga kuwakata kuwabambikia kesi kuwapiga risasi kuwapora ushindi kwenye chaguzi mbalimbali
 
TAARIFA

01 Novemba, 2019

Dkt. Bashiru Ally Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Asubuhi ya leo, ametembelewa na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba Jijini Dar es salaam.

Viongozi hao wa Baraza la Wawakilishi pamoja na mambo mengine, wamempongeza Katibu Mkuu kwa kuendelea kufanya kazi ya kukiimarisha Chama na hasa kusimamia misingi ya haki na usawa katika kipindi hiki cha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa upande wa Tanzania Bara, ambao unatarajiwa kufanyika tarehe 24 Novemba, Mwaka huu.

Aidha, akizungumza na viongozi hao, Dkt. Bashiru amewahakikishia kuwa, CCM imejipanga kuhakikisha inashinda kwa kishindo na ushindi wa awamu hii utakuwa ni ushindi wa kihistoria katika Chama Chetu.

"Hakuna wa kuizuia CCM kushinda kwa kishindo awamu hii, Chama kimetimiza wajibu wake na wananchi wanaona mafanikio makubwa yanayoendelea kupatikana kupitia serikali ya awamu ya tano, hivyo ushindi wa kishindo ni hakika." Dkt. Bashiru

Wajumbe hao kutoka Baraza la Wawakilishi ni Ndg. Rashid Shamsi Jimbo la Magomeni Zanzibar, Shaibu Ali Said (Chonga), Mtumwa Yusuph (Bumbwini), Masoud Masoud (Bububu), Bihindi Khamis Mkoa wa Kaskazini Pemba (viti maalum).

Imetolewa na;
CHAMA CHA MAPINDUZI
OFISI NDOGO LUMUMBA. View attachment 1250990

Kura hewa uchakachuaji labda lakini kwa kura za wapiga kura ni vigumu CCM wapate ushindi, hakuna mpiga kura mwenye Akili timamu ataipigia CCM kura yake.
 
Back
Top Bottom