Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,982
- 218,918
Bado sijajua hasa mwaka ambao Bashiru Ally aliingia kwenye siasa , lakini baada ya kumfuatilia kwa undani nimegundua kwamba huyu ni miongoni mwa WANASIASA WACHANGA SANA ambaye hana uwezo wa kuongoza CCM ya sasa , ameshindwa kujua kama ile CCM iliyofufuliwa na Kinana imekufa na kusambaratika kabisa.
Mwaka 2014 kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ndipo hasa kifo cha CCM kilipoasisisiwa, ukiua chama katika ngazi ya matawi ufahamu kwamba unaua chama chote hadi juu. Kwa mfano, Mtaa wa Keko Magurumbasi A kulikuwa na kiongozi wa CCM aliyeitwa Fundi , huyu aliondolewa kwenye kinyang'anyiro cha serikali za mitaa kwa mizengwe, akahamia CHADEMA.
Hakugombea chochote lakini alitumika kusambaratisha kabisa CCM Kata ya Keko, ambapo katika mitaa mitano CCM iliambulia mmoja tu tena kwa wizi. Nafahamu kwamba lengo la Bashiru Ally kuagiza marudio ya uchaguzi ni kujaribu kuondoa makovu yaliyosababishwa na uonevu lakini amesahau kwamba CCM Makao Makuu ndio chanzo cha uchafu wote huu wa kuondoa michakato halali ya kura za maoni na kukumbatia Wasaliti " walionunuliwa " ama kusaliti kwa hiyari.
CCM makao makuu imesimamia kikamilifu uvunjwaji wa katiba ya chama chao ya kupiga marufuku kura za maoni ili kuwapitisha tena Wasaliti ikiwa ni masharti ya mikataba ya ununuzi, ambapo Mwenyekiti wao Mh Magufuli alichukua nafasi ya Yesu Kristo na kuonekana akiwaambia wahamiaji kwamba " Njooni kwangu msumbukao na mizigo ya dhambi nami nitawapumzisha " Astaghafillulah ! wala hakuna mtu yeyote ndani ya ccm aliyelikemea hili , walishangilia na kupiga makofi mengi .
Sasa leo wanaCCM halali waliopigania chama chao kikamilifu wakati Bashiru akiwa UDSM, wakati wanaCCCM wanapambana kuinua chama wakishirikiana na Migiro na Kinana Bashiru hakuwepo wala wasaliti wake anaotaka kuwabeba hawakuwepo.
Nakuhakikishia Bashiru kwamba ukitaka kuimalizia CCM endelea kuwabeba wasaliti wako.
Itaendelea ...