Dr. Azaveli Lwaitama: Hakuna Tanganyika!

Dr. Azaveli Lwaitama: Hakuna Tanganyika!

Yote nimajina tu suala la msingi ni kwamba tar 9 december 1961 tulipata uhuru
Haswaaaa ! na kwa maneno haya mazito ukiwauliza watu hawa, Tulipata Uhuru mwaka gani bila shaka hawatakuwa na jibu..
 
Ni ukweli usiopingika kwamba tunasherehekea uhuru wa Tanganyika ambayo ilipata uhuru 9/12/1961, a.k.a Tanzania Bara baada ya kuungana na Zanzibar 1964.

Tanzania haikuwepo miaka 50 iliyopita, iliyokuwepo ni Tanganyika. Kama tungependa kuienzi Tanzania inavyostahiki, basi tungelenga kufanya sherehe kubwa wakati wa miaka 50 ya Muungano.

Ndugu yangu Sizwe na wenzako,
Hivi kwa akili yenu ya kawaida mnadhani Tanzania au Tanzaganyika ni nchi au jina la nchi? Nchi na jina la nchi ni vitu viwili tofauti. Kilichopata uhuru mwaka 1961 siyo jina la nchi bali ni nchi iliyokuwa ikiitwa Tanganyika; baadaye, kwa kuzingatia matukio ya kisiasa, ilibadili jina na kujiita Tanzania. Kubadilika kwa jina la nchi hakukuwa na maana ya kubadilsha nchi yenyewe, wafahamu?

Sasa kama kuna mtu anataka kujenga hoja kuhusu uhuru wa nchi yetu, mantiki ya True or /False kutoka Kinunda ONE, hapa siyo mahala pake. Nchi siyo jina. Majina ya nchi hubadilika. Historia huandikwa. Nchi haibadilishwi na jina ila nchi inaweza kubadilisha jina na ikabaki nchi ile ile. Mwafahamu. Hapa kuna political siyo mathematic logic! Mwafahamu?
 
Wakuu, wengine mnakurupuka tu na kutoka mapovu. Jiulize ni Tanzania au Tanganyika ndio iliyopata uhuru 1961? Ukipata jibu utajua kama Prof au mchangiaji ndio mpuuzi. Watu milioni 1 bado wanajiita Wazanzibar na wimbo wao wa Taifa, Bunge na Bendera yao. Kwanini isiwe hivyo kwa upande wa pili/Tanganyika? Acheni utumwa wa mawazo kwa kuwa amesema mtu eti kwa sababu ni Dk. ama Prof. huo ndio upuuzi kupita wa huyo mzee mimi nathubutu kumwita mamluki.

Alipokuwa anatoa maelezo pia alitoa mfano kuwa mwanamke anapokuwa ameolewa wakatimwengine huwa anabadili jina! lakini huwezi kuhesabu umri wake kuanzia pale alipobadili jina.
 
Fe Lady unatukana wa Tanganyika. Ina maana Tanganyika ilibadili jina baada ya kuolewa na Zanzibar?
Tanganyika hayupo,yeye alibadili jina na kuwa Tanzania bara.Sielewi kwa nini hakuretain jina la mwanzo as Zanzibar did,
 
FF aliwahi andika hapa kwamba Mwanamke wa Kiislam akiolewa hatakiwi kubadili Jina lake la asili(Zanzibar Ni nchi huru ya kiislam haikubadili jina baada ya kuolewa na Jamhuri),Tanganyika simnasemaga ya Kikristo labda ndio maana baada ya Kuolewa na Jamhuri ikaona isiwe nongwa ikabadili jina na Kuwa Tanzania Bara!!!!!!!Kwa kadri ya mfano wa Lwaitama.
 
Faiza Fox aliwahi andika hapa kwamba Mwanamke wa Kiislam akiolewa hatakiwi na haruhusiwi kubadili jina lake la asili(Zanzibar nchi huru ya Kiislam haikubadili jina baada ya kuolewa na Jamhuri ya Muungano), Nasikiaga Tanganyika ni nchi ya Kikatoliki that means ni nchi ya Kikristu so labda ndio maana ilibadili jina na kuwa Tanzania Bara baada ya Kuolewa na Jamhuri!!!!!!!!:hatari:
 
Kwa hilo si jina kama CRDB ya zamani na CRDB yaleo je maana ni ileile??funguka Azavel Lwaitama hawezi kuwa mpuuzi kwawatu wenye uwezo kiakili ni mmoja wapo!!wewe ndo unawezakuwa mpuuzi watu wanaomjua Azavel lwaitama na hii thread yako haiitaji kuwa jiniasi!!!dairekiti wewe ndiye mpuuzi!!!

Nashangaa anawashangaa wenzake kufanya yale yaliyokuwa hayafanyiki wakati wa Nyerere huku yeye binafsi amekuwa mtu wa mstari wa mbele kuikosoa Serikali.
Hivyo hiyo elimu aliyonayo unamuelekeza kupinga uhuru wa kutowa maoni kwa mwananchi? Kama usomi ni undumila kuwili wa kutaka kuonekana wewe tu ndiye unaeweza kukosoa jambo basi usomi huo ni tatizo badala ya kuleta faraja.
 
Mimi sitambui Uhuru wa tanzania bara bali nautambua Uhuru wa Tanganyika. Tulipokuwa tunapewa Uhuru nchi yetu ilikuwa inaitwa Tanganyika na bendera yetu ipo. Sasa ni wendawazimu kuipandisha bendera ya Tanzania wakati uhuru ni wa Tanganyika
Nimekupata, kumbe sherehe za uhuru wa miaka 50 ni ya uhuru wa Tanganyika ambayo hatujui ikowapi?
 
Hapy birthday Tanganyika. Japo inaonekana hakuna nchi ya Tanganyika lakini iliyopata uhuru ilikuwa ni Tanganyika na siyo Tanzania au Tanzania Bara. Nashangaa hata wanahabari wanapotangaza kuwa ni miaka hamsini ya Tanzania, hivi 1961 Tanzania ilikuwepo, lakini pia wazanzibar wanasemaje tunapopandisha bendera ya jamhuri ya muungano wakati wa sherehe ya uhuru wa tanganyika?
Tanganyika ipo....
 
Nadhani hapa unataka kusema kwamba unataka Serikali tatu. Opponents wa idea ya kuwa na serikali 3, huma wanasikika wakisema ni kwamba gharama zitakuwa kubwa sana. Au mada hapa siyo kwamba serikali au tatu,isipokuwa unacomplain kuhusu maamuzi yanayofanywa na serikali ya zanzibar which is making the island increasingly to float away from the mainland,na kusababisha muungano ulegelege? Halafu wakati wa muungano idadi ya watu ilikuwa haijafikia 1 milion. What do political scientists say about this? Nchi si inapaswa kufikia at least the 1 million mark threshold ili iitwe nchi?
 
Hajakosea lolote huyo mkuu, ni ukweli usiopingika kuwa cc wenyewe tumeiua tanganyika na kubaki na Tanzania na Zanzibar. Yule ni msomi ambaye unapaswa kufikiri sana hadi uyaelewe anachokisema!
 
Wazanzibar husherekea sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar na wala hatujahi sikia wakisema sherehe za Mapinduzi ya Tanzania Visiwani!! Sasa kwa nini huku ni sherehe ya Uhuru wa Tanzania Bara???

By the way, hivi Tanzania Bara na Tanzania Visiwani zipo kikatiba??
 
Wazanzibar husherekea sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar na wala hatujahi sikia wakisema sherehe za Mapinduzi ya Tanzania Visiwani!! Sasa kwa nini huku ni sherehe ya Uhuru wa Tanzania Bara???

By the way, hivi Tanzania Bara na Tanzania Visiwani zipo kikatiba??

I wonder myself!
 
sio kila wazo atakalo toa Dr Lwaitama ni sahihi si kweli ! hata Nyerere amewahi kusema huwa anakosea na alikuwa tayari kukosolewa.kwa hili amekosea. kwani muungano hatuwezi kuuvunja? je tukiuvunja tutatumia jina gani ? alilinganisha muungano wetu na huu wa afrika mashariki na hatimaye iwe Afrika yote je kwa kufanya hivo kunaua majina ya nchi husika? mbona umoja waafrika mashariki ulikufa na nchi zetu zikaendelea? nampinga. leo ni siku ya tanganyika wazanzibari watuunge mkono ila haiwahusu!
 
Intelijensia iko makini..au inakuwaje? Hakuna taarifa zozote kwani...
 
Inachanganya kimsingi Tanganyika haipo ilikufa 1964, lakini tunaweza KUIFUFUA kwa sasa tukubali haipo. Kuhusu Uhuru wa miaka 50 ni ya iliyokuwa Tanganyika na sasa (baada ya ubatizo) Tanzania Bara
 
Inachanganya kimsingi Tanganyika haipo ilikufa 1964, lakini tunaweza KUIFUFUA kwa sasa tukubali haipo. Kuhusu Uhuru wa miaka 50 ni ya iliyokuwa Tanganyika na sasa (baada ya ubatizo) Tanzania Bara
 
tanganyika haijawahi kufa , kila unapotamka muungano lazima utamke Tanganyika na Zanzibari pls tofautisha kubadili jina na kuunganisha nchi , sisi hatujabadili jina mpaka tulisahau la kwanza ndio hii NDOA inaweza ikavunjika muda wowote na tukarudisha Tanganyika yetu na Muda c punde inarud. tofautisha kuitwa john baadaye ikajiita musa hakuna atakaye kubughudhi. nakupenda TANGANYIKA.
 
Back
Top Bottom