Cynic
JF-Expert Member
- Jan 5, 2009
- 5,144
- 1,648
Azaveli Lwaitama ni bora angeamua kukataa kuhojiwa kuliko kutamka vitu ambavyo mdomo wake unalitamka lakini moyo wake hauliamini. Muda si mrefu atapoteza heshima aliyojijengea kwenye jamii ya wasomi.
Rais mwenyewe juzi juzi akizungumza na wazee wa DSM alitamka wazi wazi bila kuuma maneno kwamba tunasherehekea miaka 50 ya Tanganyika.
Halafu BBC siwaelewi. Lwaitama amespecialize kwenye linguistics, wao wanamtumia kama mchambuzi wa mambo ya kisiasa. BBC nao ni wababaishaji ..