Dr. Azaveli Lwaitama: Hakuna Tanganyika!

Dr Matola PhD

Platinum Member
Joined
Oct 18, 2010
Posts
61,558
Reaction score
109,095
Wakuu nashindwa kumuelewa huyu Dr Lwetama nae amejiunga na kundi la wapotoshaji kwamba eti tunasherehekea Uhuru wa Tanzania bara na kwamba wanaosisitiza ni Tanganyika wana ajenda za kisiasa, je ni huyu Dr Lwetama ninayemfahamu mimi amekua mpuuzi kwa viwango hivi?

Source: BBC Swahili sasa hivi iko live

 
Tanganyika hakuna, imewekwa kwenye kichupa na kuwa delisted!!!
 
Matola, ni vema ukubali kuishi na ukweli kuwa Tanganyika ilishachinjiwa baharini 1964
 
Mimi sitambui Uhuru wa tanzania bara bali nautambua Uhuru wa Tanganyika. Tulipokuwa tunapewa Uhuru nchi yetu ilikuwa inaitwa Tanganyika na bendera yetu ipo. Sasa ni wendawazimu kuipandisha bendera ya Tanzania wakati uhuru ni wa Tanganyika
 
Ila tuna Tanganyika Law Society!
Kwa hilo si jina kama CRDB ya zamani na CRDB yaleo je maana ni ileile??funguka Azavel Lwaitama hawezi kuwa mpuuzi kwawatu wenye uwezo kiakili ni mmoja wapo!!wewe ndo unawezakuwa mpuuzi watu wanaomjua Azavel lwaitama na hii thread yako haiitaji kuwa jiniasi!!!dairekiti wewe ndiye mpuuzi!!!
 
Unauliza Tanganyika, je Unguja na Pemba zipo?
 
yes, basi sherehe za miaka hamsini ya Tanzania zianze kuhesabiwa from 1964

je tunatimiza miaka 50 ya Uhuru ? in which Tanzania did not exist in 1964

au

tunatimiza miaka 50 ya Tanzania, in which it is not true
 
Labda KakaKiiza tu ningependa kukufahamisha kwamba mimi nina mawazo huru na ninadadisi, sijamkabidhi Dr Lwetama kufikiri kwa niaba yangu, Kama wewe unadhani au unafikiri kwamba analowaza Dr Lwetama ndio sahihi basi hata chama cha siasa atakachojiunga au kushabikia unapaswa umfuate, maana wewe tayari ni mateka wake.
 
Unauliza Tanganyika, je Unguja na Pemba zipo?
Kwahiyo unataka kutuaminisha kwamba Unguja ilikuwa ni Jamhuri na Pemba ilikuwa ni Jamhuri wakati Tanganyika Huru inaungana na Zanzibar? nahitaji kuelimishwa hapa.
 
Wakuu, wengine mnakurupuka tu na kutoka mapovu. Jiulize ni Tanzania au Tanganyika ndio iliyopata uhuru 1961? Ukipata jibu utajua kama Prof au mchangiaji ndio mpuuzi. Watu milioni 1 bado wanajiita Wazanzibar na wimbo wao wa Taifa, Bunge na Bendera yao. Kwanini isiwe hivyo kwa upande wa pili/Tanganyika? Acheni utumwa wa mawazo kwa kuwa amesema mtu eti kwa sababu ni Dk. ama Prof. huo ndio upuuzi kupita wa huyo mzee mimi nathubutu kumwita mamluki.
 
Zanzibar inaishi, Tanganyika ilikufaje?

Katiba ya Muungano

Joseph Mihangwa

NCHI yetu inaingia kwenye mchakato wa kuandika Katiba mpya. Tayari Bunge limepitisha muswada wa kuanzisha mchakato huo.

....... (Updated on 1st post)
 
Tanzania isubiri miaka 50 ya Muungano,swala la miaka hamsini ya Uhuru linaihusu Tanganyika,Hakuna nchi inaitwa Tanzania isipokuwa ni Jamhuri Ya Muungano,Tanzania ni zao la Zanzibar (Nchi) na Tanganyika (Nchi) ndizo zilizounda Jamhuri ya Muungano wa TZ. Sherehe za uhuru wa Miaka 50 inabidi bila kumung'unya maneno za Uhuru wa Tanganyika,unaweza kusherehesha kuitafuta ndani ya Tanzania,Uhuru ulitolewa kwa TANGANYIKA na si kwa TANZANIA BARA
 
Reactions: ram
Ni ukweli usiopingika kwamba tunasherehekea uhuru wa Tanganyika ambayo ilipata uhuru 9/12/1961, a.k.a Tanzania Bara baada ya kuungana na Zanzibar 1964.

Tanzania haikuwepo miaka 50 iliyopita, iliyokuwepo ni Tanganyika. Kama tungependa kuienzi Tanzania inavyostahiki, basi tungelenga kufanya sherehe kubwa wakati wa miaka 50 ya Muungano.
 
Matola, ni vema ukubali kuishi na ukweli kuwa Tanganyika ilishachinjiwa baharini 1964
Labda mkuu si unakumbuka kulikuwa na nchi inaitwa Congo? lakini wakaja wahuni kama hawa wa hapa kwetu wakaipachika jina la Zaire! je Zaire bado ipo au wananchi wamerudisha jina lao la Congo?
Tusiwe wavivu wa kukumbuka, maana ukitaka kumtawala mtu milele mnyime Historia yake. its matter of time but Tanganyika will rise again.
 
Hata mimi najua hakuna Tanganyika kwa sasa ila ikuwepo kabla ya april 1964.
Mimi pia najua Tanganyika now haipo ila kuna swali linaniumiza kichwa kweli, ivi hizi sherehe za uhuru tunasherehekea Tanzania bara au Tanzania au Tanganyika? Najua hakuna taifa la Tanzania bara duniani na halijawahi kuwepo. Kama tunasherehekea Tanganyika i wapi? au ni mchezo wa kuadhimisha kifo cha marehem? Maana nasikia kuna maadhimisho ya kuzaliwa hadi kina Bob Marley na wakati hawapo
 

nafikiri mkuu "jamaa kaamua kubisha kwa kwenda mbele"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…