Dozy Mmobuosi - Mnaijeria aliyetaka kununua Sheffield United kwa kujifanya bilionea

def_xcode

JF-Expert Member
Jul 25, 2023
596
1,620
Kama kuna watu wamesoma na wanajua mambo ila wanatumia elimu yao kutapeli ni wanaija.

Dozy ni mnaija anayedai kuwa ni CEO na Mwanzilishi wa Tingo Mobile. Jamaa alianzisha tingo mobile ikiwa na model ya kuwakopisha wakulima wa naijeria smartphones, ila baadaye akaanzisha soko la kidijitali ambapo hao wakulima wanaweza kuweka mazao yao na wanunuzi wakanunua.

Kwa madai yake akawa anadai Tingo mobile ina wakulima milioni 9 na inaingiza mapato in millions of dollars.
Move yake iliyofuata ilikuwa kusajili kwenye soko la hisa la Marekani lakini akakataliwa.

Akaona isiwe kesi, atajaribu njia nyingine.

dozi.jpg
Jamaa akaiuza Tingo Mobile kwa kampuni ya Thailand iliyojulikana MCT ambayo ilikuwa ni kampuni inayodai inaunda na kuuza mifumo kwa serikali ya Thailand. Ila kwa kipindi hicho ilikuwa haipati tenda tena so iakwa iantafuta sehemu nyingine pa kuwekeza. Wakati anaiuzia Tingo Mobile, Tingo Mobile ilithamanishwa kuwa na na thamani ya dollar bilion 3.

Kimsingi hakuna pesa aliyolipwa ila ilikuwa ni merger ambayo alipata share nyingi na akawa CEO wa hiyo kampuni ambayo hiyo merger ilifanya ile kampuni iitwe Tingo na yenyewe.

Hakuishia hapo akaenda mbali zaidi na kumerger na kampuni ya china, ambapo yeye akawa ndiye mmiliki wa 75% wa share za hiyo merger na kampuni ikaitwa Tingo Group.

Baada ya hapo ikatangazwa kwamba kampuni inaingiza faida ya zaidi ya dollar milion 250.

Baada ya muda akatangaza kuwa Tingo group itanunua Tingo Foods ambapo ni kampuni ambayo inalenga kuunda kiwanga cha kuchakata vyakula Nigeria na ndio kitakuwa ni kiwanda kikubwa Afrika. Akadai kuwa kampuni hiyo inachukua products za hao wakulima milion 9 na kuzichakata na kwa wakati huo ndani ya miezi akdhaa toka ianze imetengeneza zaidi ya dollar milion 400 na ina assets sawa na dolalr milion 225.

Jambo la kuchekesha kumbe Tingo foods mwanzilishi ni yeey Dozy na ikanunuliwa na Tingo Group kwa dollar milion 200 yani chini hata ya faida na asset ambazo walida Tingo foods inazo.

Sasa muda ulikuwa uemfika wa kuingia kwenye soko la hisa la Marekani maana haya makampuni na story zote zilikuwa kwenye makaratasi so alihitaji kuingia kwenye soko la hisa ili aweze ku cash out share zake.

Na kweli this time akafanikiwa na kampuni ikaingia ikiwa na value ya dollar bilion 1 na kila share ikwia na value ya dollar 5.

Jamaa aka cash out dollar milipon 250. Kawa anaishi high life UK London anasukuma ndinga za maana.
Shida ilianza alipotangaza kununua hiyo team ya mpira. Hakuna aliyewahi kumsikia huyu bilionea wa Afrika. Waandishi wakaanza kuchunguz ani nani.

Ndipo mambo ya kaanza kuja hadharani. Tingo mobile ilikuwa inadai ina wakulima milion 9, lakini kwenye Google play app yao ina downloads 5 tu.

Ilikuwa inadai inafanya kazi katika eneo fulani ambapo kumbe hata statistics za serikali inadai population ya eneo hilo ni watu milion 3.5.

Mambo yakawa mengi alikwua ameanzisha na Tingo Air ikaja kugundulika ahta ndege moja hawana na picha za ndege kwenye page ya social media ziko photoshoped kuweka logo tu.

Board of directors wa kampuni walikuwa watu waliokuwa wanafanya kazi online wakiwa marekani, CEO akiwa London au Nigeria na auditing ikifanywa na Delloite tawi na Israel kwa CEO kuwatumia photoshoped bank statements.

Si hivyo tu, delloite walipokuwa wanataka kuwasiliana na supply wa simu amabye ilidaiwa yuko china jamaa alilwapa email kumbe alinunua email ambayoni @ jina la kampuni aliyodai iko china an kuwapa, kumbe walipomtumia akawajibu yeye wmenyewe ndiye mwenye email.

Jamaa alikuwa amelipia emails kibao anafanya kuwajibu yeye mwenyewe na wanampitisha with green color.
Hata email za wakulima zilikuwa za kwake mwenyewe.

Baada ya taarifa kutoka share zilianguka na kampuni ikaondolewa kwenye soko kwa ajli ya uchunguzi. Jamaa yuko UK anakula maisha ya pesa alizo cashout sijui atakamatwa au la!

Wanaija ni wezi ila wezi wao wa kitaalamu hadi mzungu anapigwa kitaalamu akiamini kitu genuine.
Jamaa aliwahi tokea kwenye jarida la Forbes afrika kumbe ni unalipia tu wanakuweka.

Kuna jamaa maarufu aliwahi tokea kwenye video akipongeza Tingo mobile kusambaa afrika nzima, wachunguzi wakagundua kumbe kuna mtandao unalipia dollar 90 wao wanadeal na watu maarufu kuwafanya wajirekodi chochote uanchotaka.
 
Back
Top Bottom