DOWANS waisamehe TANESCO deni lote!

tutakuja kulia kwa hii ishu ya dowans mpaka basi mi nawambi

tukitumia tu mitambo yao twafa....maana lazima deni lijilipe....kama tunasema bigi no na tuseme sasa na sio kusubiri
waiingie mkataba mpya
 
Ni mambo mengi JK kateleza ila hili nchi inajiendesha yenyewe...hatuna Rais
 
Si uliiona nyomi ya jana Mwanza?
Unafikiri hawana hakiri kabisa?
Sasa wametambua kuwa upepo unawaendea vibaya wanajaribu kujiosha.
Msimamo uleule kwa CHADEMA mpaka kieleweke.

kweli waliona ndio maana wame-act effectively.

lakini huo msamaha ni wa kweli?
lazima kuwe na reason behind the scene.
Either wameona wapretend kuwa wamesamehe then wainunue kwa bei maradufu huku wakilipana deni lao juu kwa juu

Jamani Nothing goes with Nothing
 

Huo ndio mpango halisi uliopo kwa sasa kwa hiyo kama hujui basi elewa hilo ndilo lililopo kwenye table
Unadhania jamaa ni wajinga wasamehe tu na waondoke?
lazima wawe wamepewa donge jingine nono la kuwekeza zaidi kwenye nchi ya wadanganyika
 
Mi sasa hivi sitaki kusikia ishu ya hela, ninachotaka ni umeme. Walipe, wasilipe, najua hakuna kitakachobadilika chini ya serikali ya mafisadi...
Mjukuu wangu acha kukata tamaa mapema hata jioni haijafika wee
A coward people always die before their time
We will fight till the end,
Dr.Slaa amewapa siku 9 lasivyo ataitisha maandamano nchi nzima

 
wanazodai ni zaidi ya walizosamehe,sasa wangetaka walipwe yote ingekuwaje?kweli siasa ni mchezo mchafu
 
Ahsante sana Gurudumu kwa kutuhadithia Hadithi nzuri na ya kupendeza
basi nakwenda kulala salama etiii
 
Huyo munai ni wa wapi hapa Tanganyika??? Natamani tuanze kuwapiga mawe hawa wahusika wote, sababu mambo yao ya gizagiza tu. Anaishi wapi huyo?
usiwe na hofu mjukuu tutakupa taarifa ASAP baada ya intelijensia yetu kupata majibu kamili
tutamchunguza toka anaingia na anapotoka
we are still monitoring the situation
 

Nimeukubali uchambuzi wako. Hiyo siasa iliyochezwa bungeni ya kubadilisha maana ya kambi rasmi haikuwa bure. Ni kutokana na maana mpya ndio tukawapata kina John Cheyo na Lyatonga kama wenyeviti. Na Cheyo alisema atampigia debe mmoja kutoka CDM ambaye naamini ni huyu dogo kibaraka wao Zitto. Mmmh - Mambo ya mafisadi hayo! natamani kufa ...!
 
Suala sio kusamehe, lazima kuna kitu kimefanyika ili mambo yapoe. Kuna siri hapo imefichwa usikute tumelazimishwa kuwatumia Dowans kwa miaka kibao.
 
Nakumbuka TRA walizuia mitambo hiyo isihamishwe kwa vile Dowans wanadaiwa kodi. Nina uhakika hilo deni la kodi bado hawajalipa na tukawabana huenda hata hayo wanayosamehe hayafikii kodi hiyo.
TRA najua mnapitia humu jamvini, watembeleeni hao matapeli tujue kama wamelipa kodi yetu.
 
Kwani tuliwaomba watusamehe; tumewaambia hatuwalipi na majenereta yao hatununui wakitaka wakayauze Oman huko. Kwani wanogopa nini wakati kuna kesi zimefunguliwa mahakamani kupinga hiyo tuzo? Wanaogopa kushindwa kwenye mahakama zetu?
 
Hapa JahK, hapa Lowesha,
Hapa Rost, hapa Al Adaiwi
Hapa kiiNgeleja hapa Jahnuwari
Hapa chao, hapa zao!
Wapi chetu walwa!?
a?
 
Hii inawezekana ikawa danganya toto tu. Watanzania tuwe macho, wanaweza kutoa taarifa hizi but behind the curtain wakalipwa.
Maandamano ya wananchi nayo yamesaidia kutoa changamoto kwa serikali ya kishikaji ya CCM.

Tanzania kila kitu kinawezekana kabisa, tatizo ni maamuzi. Watanzania wameandamana kupinga ongezeko la bei ya sukari, serikali imesharukia na kudai itapunguza. Tuyaongeze haya maandamano hadi kieleweke, sisi ndiyo wenye nchi. They have to obey what we WANT.
 
Kwani tuliwaomba watusamehe; tumewaambia hatuwalipi na majenereta yao hatununui wakitaka wakayauze Oman huko. Kwani wanogopa nini wakati kuna kesi zimefunguliwa mahakamani kupinga hiyo tuzo? Wanaogopa kushindwa kwenye mahakama zetu?

Mkuu uliwahi kusoma simulizi za gaidi mmoja zamani anaitwa Carlos? Nahisi ama kuna jambo kubwa tayari hawa mafisadi wameshafanya kupata pesa yao hivyo sasa wanajisiemea "bakini na hiyo tuzo yenu sisi tumepata zaidi"
 
Wamesamehe sababu wamesoma alama za nyakati. They couldn't keep up with the lies as paying them would have compromised a lot. a lot that had been built on unnecessary lies.
Hili ni fundisho kwa mafisadi na vibaraka vyao.
 
Kwa taarifa ya Radio Tumaini, leo asubuhi saa 3, Dowans wamekubali kusamehe shirika la TANESCO deni la Bil 94. Hii naona ni habari njema. Kitu ninachojiuliza ni sababu ipi iliyopelekea hatua hiyo kutoka kampuni ya DOWANS kufikia uamuzi huo kwa sasa.

Mimi naona ni kichekesho tu ila kuna 'hidden agenda' kubwa si bure, na ulaji kama kawaida kwa wakubwa wa wizara na wengineo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…